ok, vipi hicho kizazi ni endelevu kweli? maana niliwahi zungumza na reseacher mmoja akanieleza hivyo.
still in learning phase.
Asanteni sana.
Asante, Kariakoo bei yao kwa kilo ni sh. ngapi maana naona bei yao ni juu. Manzese huwa ndo nanunua pumba ila mashudu sijawahi ona manzese labda nijaribu ku-check vizuri.
Kuhusu hizo mbegu labda nikufanyie mpango wa kuzipata
mimi nahitaji vifaranga, wanapatika lini?
Vifaranga wanapatikana na kwa sasa pia wapo wa siku 1, 1wk & 2wks. Unaweza toa oda kabisa
Vipi naweza pata mayai ya kuatamisha kama 1000 hivi? na also nitakutafuta kuhusu vifaranga wa Kuku wa kienyeji, ok
Mama Joe
Hawa kuku ni wa kienyeji, ninazo mbegu tatu tofauti (Kienyeji asili, Kuchi chotara na Rhode red island)
Kuhusu chakula kuna mtu alitaka mchanganuo kwa style hiyo ili apate mwanga kidogo ila kawaida kuku wa kienyeji hawaitaji chakula cha dukani japo wakila hicho cha dukani haina shida yoyote. Ndo maana pia nikasema gharama ya chackula itapungua kulingana na mahali na mahali, kulingana na upatikanaji.
Asante
Kuku wa "kienyeji asili" andiyo lakini asili ya wapi? Tanzania, Malawi, Msubiji au nchi nyingine yoyote ya africa, maana hawa wote ni asilia wanaotofautiana tu kwa sifa flaniflani kutokana na nchi husika mfano wengine wanene, wanataga tu hawaatamii, wanataga na kuatamia, miguu mirefu n.k.
Naomba pia kujua vifaranga vyako ni majike tu au na majogoo. Je unawtofautishaje majike na majogoo katk vifaranga vya umri wa siku moja?
Asante
Kitu kimmoja nashindwa kuelewa. Hawa ni kuku wa kienyeji lakini naona malisho ni sawa na hao wa kisasa, sasa tofauti inakua vipi?
vipi vifaranga wa siku moja watapatikana lini, nipo tayari kwa oda sasa