ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,151
Najua leo ni Valentines day, watu mmejiandaa na wapendwa wenu kutoka mara baada ya kazi ili mkabadilishane mawili-matatu,. sasa basi si vyema ukaenda outing yako ukiwa tumbo wazi, ni vyema ukaweka chochote cha chapchap ili tumbo liwe poa kupokea vinywaji na chomachoma kama za ng'ombe,mbuzi au kuku. karibuni mtupie hiki maana tumbo halitakiwi kushiba sanaaaa...
HAPPY VALENTINES DAY JF Chef funs!!!!
MAYAI YA SOSEJI

Hapa ni mayai na soseji kwa pamoja na pia kuna aina mbili za kutengeneza kulingana na unavyopenda.
YA KWANZA
unakuwa na kitunguu maji unakata kwa style kama inavyoonekana au ukitaka umbo la duara zima(ring) ni sawa.
Unachukua soseji zako hapo mimi nilitumia 4 na kuzikata mara tatu kwa kila moja.Unaweka chumvi kidogo kulingana na mahitaji yako halafu unakoroga vizuri.
Wakati huo frying pan yako ipo jikoni na mafuta kidogo yamepata moto unamiminia humo mayai yako.Kubwa hapo ni mayai yaive na soseji zako pia ziive kimtindo.Hivyo utayageuza na kuhakikisha yameiva na kuweka kwenye sahani yako.
Unaweza kunyunyizia pilipili manga kidogo ili kuleta ladha kwenye mayai yako ya soseji.
Hapa mambo yanakuwa tayari

YA PILI
Hii ni kama unavyotengeneza spanish omlet unakuwa na nyanya moja,hoho nusu,kitunguu nusu,unaweza kuongeza na karoti pia.Ukisha viosha vizuri unakata vidogovidogo muundo wa cubes(pembe nne) unaweka kwenye bakuli lako.
Chukua soseji zako hapa pia mimi nilitumia 4 zikate ndogo ndogo zote halafu weka kwenye bakuli lilelile lenye mchanganyiko wa awali.Baada ya hapo vunjia mayai yako mie nilitumia matatu na koroga vizuri mchanganyiko wako pasipo kusahau chumvi.
Frying pan itakuwa jikoni na mafuta yakisha pata moto miminia mayai yako kaanga vizuri ili yakauke na soseji ziive.
Vikiwa tayari weka kwenye sahani na tayari kuliwa na chai au juisi pembeni unaweza kuwa na mkate sio mbaya.
ENJOY IT!!!