Mayai yaliyo gandishwa

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Mimi sio mpenzi wa mayai au ndege aitwaye kuku kabisa. Lakini nimekuja kugundua chakula chochote kukipenda au kutokukipenda inategemea na kilivyopikwa na kilivyotayarishwa.

Sipendi mayai yawe ya kukaanga au kuchemsha. Lakini nikaja kukutana na upishi wa tofauti wa mayai.

Hatua 1. Gandisha mayai yako kwenye freezer. Yaache kabisa hadi yagande. Yawe hivi

.

Baada ya kuyagandisha yamenye. Kisha utabaikiwa na kitu kama hiki




Kisha kata vipande vidogo kama ukatavyo viazi vya chipsi. Bahati mbaya nilisahau kuchukua picha ya hivi vipande.

Kisha tia kwenye pan anza kukaanga unaweza kutumia mafuta yoyote...olive ni nzuri zaidi. Tayari kwa kuliwa [emoji116]

Mayai yako yapo tayari kwa kuliwa....unaweza kutengeneza sauce yoyote kulingana na taste yako.


Faida ya upikaji huu ni kwa wale wasiopenda ile harufu ya mayai hasa haya ya kisasa. Inapotea kabisa.
 
Mayai yako yapo tayari kwa kuliwa....unaweza kutengeneza sauce yoyote kulingana na taste yako.

View attachment 1436537
Mkuu hicho unakula kushiba au kuipagawisha minyoo tu..?😅
Maana kuna viumbe hapa tunaminyoo mpaka ya mzimu wa babu yake babu aliekuwa babu wa babu yake babu alikuwa babu ambae bado ni babu wa mababu😅

Ukila kama hicho ni shambulio lisilochukua sekunde wajeba wanaanza kuita Tena🤣
 
Hahaha...kukata hamu mkuu.....hicho hakishibishi aseeh.
 
Nitajaribu pishi hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…