Mayanja aipa Yanga nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu wa nne mfululizo!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
KOCHA Jackson Mayanja ambaye amejiengua kwenye kikosi cha timu ya Simba kwasababu zisizojulikana, amesema kwamba pamoja na mwenendo wa timu hiyo katika Ligi Kuu bara lakini nafasi ya Yanga kutetea ubingwa ni kubwa kuliko watu wanavyofikiri.

Mayanja amesema kuwa kiufundi timu ya Yanga inaimarika kadri siku zinavyosonga mbele hivyo hataona ajabu akiona wametwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

“Nisingependa kuzungumzia namna nilivyoondoka Simba kwasababu yale yalikuwa maamuzi yangu binafsi na wala sikushinikizwa na mtu yeyote, lakini kwa mwenendo wa Ligi ninavyoona Yanga inaweza kushangaza watu mwishoni mwa msimu,” alisema Mayanja.

“Mimi kama kocha naweka karata yangu ya ubingwa Yanga kwasababu kila siku naona wanabadilika na kuboresha maeneo yenye upungufu,”aliongeza.

Mayanja alitangaza kujiuzulu kuifundisha Simba baada ya kuiongoza kwenye mechi sita za mzunguuko wa kwanza wa Ligi na taarifa zilizopo ni kuwa ataelekea kujiunga na timu ya Kagera Sugar.
 
Yanga ni timu tulivu yenye maamuzi ya busara si ya kukurupuka, zaidi timu hii hucheza mpira uwanjani si sawa na timu inayojiita simba kumbe ni nyau...simba wanacheza mpira mezani na mdomoni lkn uwanjani hamna kitu
 
Hiyo iko wazi mbona inaeleweka

Sikuwahi kujua Mtu niliyemuheshimu kama Wewe humu JF utakuwa ni Mshabiki wa Klabu ' mbovu ' na ninayoichukia kuzidi hata Shetani Lucifa kama ya Yanga SC. Umenisikitisha mno Mkuu. Great Thinkers wengi ni Mashabiki wa Mnyama Mnyamani Simba Sports Club hivyo jitafakari na karibu haraka Msimbazi.
 
Nipo Yanga na siondoki ng'oo ukiwa mtani wangu sio mbaya mkuu
 

Ungeelewa maana na dhaa nzima ya ' mind game ' wala usingehamanika / usingekurupuka hivi ila tatizo ni kwamba ' Mashabiki ' wengi wa Yanga SC wana ' akili ' ndogo sana katika ' brains ' zao na ndiyo maana hata hawajaweza kung'amua / kutambua huo ' mtego ' wa Jackson Mayanja. Jidanganyeni hivyo hivyo ila naweka ' nadhiri / kiapo ' leo hii hii kwamba kwanza Simba SC haitoifunga Yanga Jumamosi tarehe 28 nitaenda kupanda Mlima Kilimanjaro nikiwa ' Kifua wazi / Kidali po ' na kama haitoshi kama msimu huu wa 2017 / 2018 Klabu ya Simba SC haitokuwa Bingwa wa VPL basi nitaenda ' Kuoga ' mchana kweupe pale Posta ulipo ule mnara wa Askari huku ' Kadamnasi / Nyomi ' lote la down town likinikodolea hasa sehemu zangu Kuu za ' Kibaiolojia ' nilizojaaliwa nazo.
 
Nipo Yanga na siondoki ng'oo ukiwa mtani wangu sio mbaya mkuu

Una bahati sana kwamba nimekujua kuwa Wewe ni Mwana Chura Churani Yanga SC leo wakati tayari tumeshakuwa Marafiki kwa muda sasa ila laiti kama ningeujua huu ' msimamo ' wako mapema Mimi na Wewe nadhani hivi sasa tungeukuwa kama Palestina na Israeli au Marekani na Korea ya Kaskazini. Nisikufiche Mkuu naichukia mno Yanga SC na wala sifichi na hata nikiambiwa nivalishwe ' bomu ' niende kujitoa nalo ' mhanga ' jengo la Yanga pale mitaa ya Twiga na Jangwani lilipuke na liharibike beyond repair Mimi GENTAMYCINE nipo tayari muda na wakati wowote ule.
 
Hahaha usifanye hivyo....Tuendeleze utani wa jadi mkuu
 
Naona sasa "unawashwa" tulia dawa iingie wewe eboh!!
 
Acha uongo na kupotosha mkuu
Mkia hauwezi kuwa kichwa hata siku moja
 
Haya maneno misimu mitatu mfululizo huwa mnayatoa lkn mnaangukia pua na papara zetu za kitoto
Mnaanza kwa mbwe mbwe nyingiiii mara mezani , mara FIFA, mara pooh mwisho wa mnakubali kupokea mahari na kukaa wanawali
Mnaacha vidume tunanyanyua kwapa huku mkishuhudia masharubu ya kwapani kwa mwanaume
 
Mbona kwenye uzi mwingine hapo juu umejinasibu kuwa wewe ni mwanajangwani mkuu! Angalia tutakudharau na wewe kama unaongea kama uko unsound mind!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…