Mayele hafai kucheza kama striker wa mwisho kwenye mfumo wa mshambuliaji mmoja mbele

Jbst

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2020
Posts
1,971
Reaction score
4,085
Mayele ni mchezi mzuri sana ni mmoja wa wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza ktk ligi yetu, katika top 3 ya washambuliaji bora zaidi kutoka nje ya nchi mayele ni mmoja wapo.

Kwa namna anavyocheza mayele binafsi kwa maoni yangu naona hafit kwenye mifumo ya ya striker mmoja mbele mfano 4-5-1, na pia mfumo anaoupenda sana nabi ndo huo yaani mayele ni striker anayekuwa mbele pale.

Maoni yangu kutokana na kwamba mayele sio mzuri kwenye finish, yani mayele ni mchezaji anayependa sana kukaa na mali ndo afunge na pia mayele sio mzuri kwenye mashuti ya kufunga huwa anajaribu sana unakuta ktk mashuti 5 moja ndo linakua la hatari.

Maoni yangu kutokana na uchezaji huo wa mayele anapendezea kucheza ktk mifumo ya washambuliaji 3 mbele 4 3 3 , kutokana na kasi ya mayele na nguvu anapaswa kucheza kitokea pembeni ktk mfumo huo au mfumo wa 4 4 2 ila mayele awe nyuma ya striker wa mwisho.ktk hao wawili.

Mayele anakosa sana magoli pale kwenye box kutokana na kuwa makini, namshauri nabi ajaribu hiyo mifumo na mayele asiwe striker wa mwisho. Mfano ktk 4 3 3 hao watatu wa mbele aanze na mayele kutokea kushoto, maize kutokea kulia na musonda katikati watafunga magoli mengi sana kama wataambiwa wasicheze kibinafsi.
 
Kweli kabisa. Na musonda alisajiriwa Ili amsaidie pale mbele ila kafeli.
 
Umejitahid I babu KwA huu uchambuzi wako kama asipokuwA mbinafsi na mzinze pia pale Kuna magori mengi tu
 
Hii ni kweli kabisa, Mayele akiwa mbele peke yake naona anakosa sana usaidizi na anabaki kuzunguka tu kama pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…