Mayele ashindanishwe na Mayele maana ukishindwa kumla utamnywa tu goli anafunga Nkane watu wanashangilia Mayele style!,
hata ukileta jeshi zima la waasi wa M23 wamdhibiti yeye hatafunga ila lazima atatoa assist kwa Feisal, Nkane, Chiko, Ambundo au Makambo!
Kiufupi anajua maana ya kucheza kitimu , ameshindikana na hakabiki!!
Washambuliaji wetu wazawa wajifunze kwa Mayele haji uwanjani kutafuta sifa za kufunga yeye tu ili ateteme bali anakuja kusaka ushindi wa Yanga nyie mkamieni mkabeni na kifaru na makombora ila dkk hazitaisha mtalia tu!
Ni haki yake kuwa NBC player of the year, mtz gani hamjui Mayele? mtoto gani mtaani hamjui Mayele? Nani asiejua kutetema kati yetu? Nani kaleta hamasa ya ligi mwaka huu? timu gani inakutana na Yanga bila wachezaji kujadili jinsi ya kumdhibiti Mayele? Mabeki wangapi wana injury kwa kuumia katika vita yao na Mayele mmoja Ame!!! Mayele kama Star wa Yanga ukiuuliza watu mtaani je Makolo FC nani star wao wengi watajibu ni Barabarani, MOooon na Matofali au wachache watasema Boko Haram, Sokoni au Magari labda!!