Mayele, Sopu na Mpole ndio wangeshindanishwa mchezaji bora msimu huu

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Bodi ya ligi, sikieni kilio cha watanzania, kumweka Bangala, Inonga na Mayele kuwania uchezaji bora ni kukosa weledi, mnaonekana nyie sio watu wa mpira, mpira wa miguu na hata ngumi ni mchezo wa wazi sana, Mayele alitakiwa kushindanishwa na Mpole na Sopu ili tujue mbivu na mbichi, mnauaibisha mpira wa Tanzania, msitafute migogoro isiyokuwa na msingi, msiturudishe enzi zile za marehemu Muhiddin Ndolanga.
 
Mayele alitakiwa kushindaninishwa na
1 Mayele
2 Mayele
3 Fiston Kala Mayele
Kwa ujumla Hana mpinzani, kumwekea washindani ni unafiki tu wakati ukweli mna ujua.
 
Acha mihemko
 
Kituko kingine ni meneja wa manungu turiani kuwepo kwenye tuzo wakati uwanja ulikuwa hautumiki kwa kipindi kirefu ila tff kuna vilaza sana inaonyesha.
 
Mayele alitakiwa kushindaninishwa na
1 Mayele
2 Mayele
3 Fiston Kala Mayele
Kwa ujumla Hana mpinzani, kumwekea washindani ni unafiki tu wakati ukweli mna ujua.
Hakuna kitu hapo anabebwa tu sopu kamuonyesha nini maana ya ufungaji, jamaa kapiga goli 3 kwenye fainali kitu amabacho huyo fala wenu hatokaa haweze
 
Mayele alitakiwa kushindaninishwa na
1 Mayele
2 Mayele
3 Fiston Kala Mayele
Kwa ujumla Hana mpinzani, kumwekea washindani ni unafiki tu wakati ukweli mna ujua.
Mayele ashindanishwe na Mayele maana ukishindwa kumla utamnywa tu goli anafunga Nkane watu wanashangilia Mayele style!,

hata ukileta jeshi zima la waasi wa M23 wamdhibiti yeye hatafunga ila lazima atatoa assist kwa Feisal, Nkane, Chiko, Ambundo au Makambo!

Kiufupi anajua maana ya kucheza kitimu , ameshindikana na hakabiki!!

Washambuliaji wetu wazawa wajifunze kwa Mayele haji uwanjani kutafuta sifa za kufunga yeye tu ili ateteme bali anakuja kusaka ushindi wa Yanga nyie mkamieni mkabeni na kifaru na makombora ila dkk hazitaisha mtalia tu!

Ni haki yake kuwa NBC player of the year, mtz gani hamjui Mayele? mtoto gani mtaani hamjui Mayele? Nani asiejua kutetema kati yetu? Nani kaleta hamasa ya ligi mwaka huu? timu gani inakutana na Yanga bila wachezaji kujadili jinsi ya kumdhibiti Mayele? Mabeki wangapi wana injury kwa kuumia katika vita yao na Mayele mmoja Ame!!! Mayele kama Star wa Yanga ukiuuliza watu mtaani je Makolo FC nani star wao wengi watajibu ni Barabarani, MOooon na Matofali au wachache watasema Boko Haram, Sokoni au Magari labda!!
 
Kama umaarufu ndiyo sababu ya mtu kuwa mchezaji bora hata balotel angeshachukua Ballon D'or
 
Kama umaarufu ndiyo sababu ya mtu kuwa mchezaji bora hata balotel angeshachukua Ballon D'or
assists na magoli mengi , kujituma kwake rejea mechi na Polisi kule Arusha alipochomoka goli akafunga Ambundo ilikuwa mechi ngumu sana kwa Yanga kisha jazia na umaarufu wake Mayele!
 
Hakuna kitu hapo anabebwa tu sopu kamuonyesha nini maana ya ufungaji, jamaa kapiga goli 3 kwenye fainali kitu amabacho huyo fala wenu hatokaa haweze
Sopu anakabwa kama Mayele? Sopu siku akiifunga tena Yanga hat trick niambie nichangishe pesa ujengewe gorofa!

Hivi tunavyoongea Kaze anarudia video za magoli ya Sopu nakuhakishia hataona tena nyavu za Yanga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…