Mayowe ya Viwanda na Mawakala wa Saruji yanapoundiwa tume. Ni kiashira cha ……

Mayowe ya Viwanda na Mawakala wa Saruji yanapoundiwa tume. Ni kiashira cha ……

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,605
Reaction score
1,085
Nimeona kwenye taarifa za ITV Viwanda vya ndani na mawakala wa saruji wanapiga mayowe soko limeingiliwa na saruji toka nje. Wanasingizia ya nje inakwepa kodi. Kwani wawekezaji wao si wageni (Norway nk)?.

Ni kiashiria mwanachi ameanza pata ahueni ya bei. Mawakala wamepata faida siku nyingi kwa ukiritimba (monopoly).
Iweje kila kukicha wanajenga mashule lukuki, majumba na vituo vya biashara kama wao hawakwepi kodi?

Iweje Serikali (Mh. Kigoda) kuunda tume kuchunguza ushindani huu?

Serikali ipo kumlinda mwananchi au?
 
alichofanya kigoda ni sahihi kwani wakati wenye viwanda wanadai soko la ndani lilindwe wanashindwa kueleza inakuwaje saruji inatoka nje na bado inakuwa bei ya chini kuliko inayozalishwa ndani
 
alichofanya kigoda ni sahihi kwani wakati wenye viwanda wanadai soko la ndani lilindwe wanashindwa kueleza inakuwaje saruji inatoka nje na bado inakuwa bei ya chini kuliko inayozalishwa ndani

hata ubora...twiga cememnt hukauka haraka ina unapasuka pasuka hovyo, ni nzuri kwa finishing na kuremba nyumba si kwa kujenga.
 
hata ubora...twiga cememnt hukauka haraka ina unapasuka pasuka hovyo, ni nzuri kwa finishing na kuremba nyumba si kwa kujenga.

Mkuu unashauri sement ipi ni bora zadi kwa kujengea?
 
naunga mkono hatua ya kuruhusu saruji kutoka nje tumeteseka sana, tumenyonywa sana na tumepuuzwa sana labda sasa huu ni mwarobaini wa upumbavu wa viwanda vya ndani, Mbeya Cement wanauza saruji yao mkoani Mbeya Tshs 16500/= wakati saruji ya kiwanda hicho mkoani Dar es salaam inauzwa 14,000/= manake mwananchi wa Mbeya ndiye anayelipia nafuu ya saruji hiyo kuuzwa Dar es salaam huo si ujinga?? Bora tu vifungwe tusubiri hiyo ya nje manake hakuna nafuu yoyote ya kuwa na viwanda mtaani na kutokuwa navyo! Coorporate social responsibility haitekelezwi kabisa na viwanda vya ndani kwa wananchi wake mfano zaidi kwangu ni kiwanda cha saruji cha Mbeya wapo wapo tu!!!
 
twiga cement(portland)ni mbaya ,(non salt resistant) ni bora kutumia cement ya nje kutokana na mahktaji yako.pakistani ni nzuri kwa maeneo yenye chumvi.
 
Tume ikomae na ubora tu kukazia TBS bei iachwe kwa soko tutaamua wenyewe
 
Tatizo jingine ni tume ya ushindani wanajua kabisa kabisa makampuni ya saruji hapa nchini yanakaa na kuafikiana kuuza saruji bei moja lakini yanashindwa kuyadhibiti kwani yanakiuka sheria ya ushindani lakini waziri husika anatakiwa kujua sehemu kama tume ya ushindani wanatakiwa kukaa watu waliosomea mambo ya cost accountant kwani wana utaalamu wa kujua kama bei zilizopangwa zinaendana na gharama ya uzalishaji ni bora iko kitengo kikawa chini ya hazina
 
twiga cement(portland)ni mbaya ,(non salt resistant) ni bora kutumia cement ya nje kutokana na mahktaji yako.pakistani ni nzuri kwa maeneo yenye chumvi.
Acha ngonjera, toa sababu za kitaalamu kwa nini cement ya Pakistani ni Bora. Kwani cement nyingi zinazouzwa hapa nchini ni 32.5R
 
Kama tuko kwenye soko huria, hao wenye viwanda wanalia lia nini, wapunguze bei tutanunua yao. Serikali mtulinde na sisi makapuku, msiwalinde wenye viwanda peke yao!
 
Mbaya zaidi, Twiga Cement wanachafua mazingira maeneo ya Wazo Hill na Boko.

Hawachukuliwi hatua zozote na NEMC. Watu wamkimbia nyumba zao, watoto wanaathirika mapafu. Watu wanabadilisha shuka na curtain mara dufu kwa siku.
 
Market forces should allowed to take its own course without interference.

Huyu Kigoda si ndiye aliyesimamia na kuhamasisha uwezekezaji wa ndani na nje? Iweje leo anakuwa upande mmoja wa shilingi?.

A tiger watching a chicken house.
 
Back
Top Bottom