naunga mkono hatua ya kuruhusu saruji kutoka nje tumeteseka sana, tumenyonywa sana na tumepuuzwa sana labda sasa huu ni mwarobaini wa upumbavu wa viwanda vya ndani, Mbeya Cement wanauza saruji yao mkoani Mbeya Tshs 16500/= wakati saruji ya kiwanda hicho mkoani Dar es salaam inauzwa 14,000/= manake mwananchi wa Mbeya ndiye anayelipia nafuu ya saruji hiyo kuuzwa Dar es salaam huo si ujinga?? Bora tu vifungwe tusubiri hiyo ya nje manake hakuna nafuu yoyote ya kuwa na viwanda mtaani na kutokuwa navyo! Coorporate social responsibility haitekelezwi kabisa na viwanda vya ndani kwa wananchi wake mfano zaidi kwangu ni kiwanda cha saruji cha Mbeya wapo wapo tu!!!