Kama ni lazima ulime Chalinze,basi fuata maelekezo haya, ukitoka Dsm kwenda Chalinze, kabla hujaingia Chalinze mjini mkono wako wa kulia kuna misufi mingi na petro station fulani hivi. Kuna kiukuta na njia/barabara ndogo inaingia ndani. Pembeni yake huwa wanapaki basikeli za kukodi. Ukifika pale uliza njia ya kwenda Talawanda/magurumatali. Ni km 20 toka Chalinze mpaka Talawanda. Eneo lote kuanzia pale chalinze mpaka Talawanda linafaa sana kwa kilimo cha ufuta,mahindi,alizeti,karanga, korosho,mtama na ufugaji wa mbuzi, na udongo wake ni mzuri sana. Mvua za pwani unazijua vizuri. Ardhi bado kubwa sana na haijatumika vilivyo. Moja ya ahadi ya rais ni kupeleka maji toka wami.
Tahadhari ukifika Maguru matari,kuna pori la watu pale la eka 500. Kama ni kilimo cha mvua za Mungu huko kunafaa.