Kigamba
Member
- Feb 10, 2021
- 5
- 2
Mazao mkakati ni mjumuhisho wa mazao ambayo uzalishaji wake umekua hafifu"mdogo" kulingana na huitaji wake sokoni yanaweza kua ya chakula au biashara. Hivyo serikali kuandaa mikakaati kwaajili ya kukuza na kuamasisha uzalishaji wake. Mfano; pamba, korosho, chai, karafuu, mkonge, michikichi na tumbaku.
Uzalishaji wa mazao haya hukabiliwa na chanangamoto zifuatazo
1. Ukosefu wa elimu juu ya mbinu, kanuni, uvunaji, na hufazi umekua chachu kubwa ya kudidimiza uzalishaji wa mazao haya hasa pale maafisa wanapo kua wachache na wale wanao pangiwa vituo vya kazi kuamia mjini kutokana na changamoto za makazi na usafiri hivyo kusababisha wakulima kupata taarifa potofu juu ya mazao haya ya kimkakati.
2. Mfumko mkubwa wa bei za pembejeo za kilimo ni miongoni mwa vichocheo vya uzalishaji mdogo hasa mkulima anapo lazimika kununua bidhaa kama Mbegu,mbolea na sumu kuvu hivyo kukatisha tamaa na kuchangia uzalishaji wa mazao mengi yasio na ubora wa kimataifa na mkulima kukosa huaminifu na serikali take hivyo kukata tamaa kabisa.
3. Ukosefu wa mitaji umekua ukichangia uzorotaji wa uzalishaji hasa ukizingatia wakulima wengi Tanzania awanamitaji yakutosha hivyo kufanya kilimo cha mazao haya kama mazoea ya kila siku ambapo wengi wa wakulima hawana fedha za kununua pembejeo za kisasa kama matrekta,machine za umwagiliaji,sumu kuvu,mbolea hivyo kuchangia uzorotaji wake.
4. Utendaji usio mbovu wa wa Sera na mikakati ya serikali kuhusu mazao haya mkakati kunaibuka ubabaishaji mwingi ambapo serikali huaidi mambo mengi ambayo kimsingi utekelezaji wake ni mgumu kutokana na uwepo wa viongozi wasio wazalendo na wenye tamaa za fedha za umma, ruzuku zitolewazo na serikali kwaajili ya wananchi kujimilikisha wao.
5. Ukosefu wa masoko ni changamoto kubwa hinayo kabili wakulima hasa wa mazao mkakati pindi inapotokea uzalishaji umepanda kuliko matarajio hivyo kuchangia uporomokaji wa bei, pia serikali kununua mazao haya baadhi ya mikoa na utngevu pungufu wa bajeti za serikali kwenye ununuzi.
6. Usimamizi mbovu wa vyama vya ushirika. Yaliyo tokea kwa wakulima wa korosho ni matokeo ya uongozi mbovu wa taasisi husika ambapo kumekua na mianya mingi ya ufisadi na upotevu wa pembejeo unaofanywa na viongozi.
7. Mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi ni miongoni mwa sababu zinazo changia uzorotaji wa mazao haya ya mkakati kutokana na shughuli za kibinadamu kama uchomaji misitu, uchomaji mikaa na uchafuzi wa viwanda hili linachochewa zaidi na viongozi wengi kupenda njia za kando na upokeaji wa rushwa viwandani na kwa mtu mmoja mmoja kwa ngazi zote hivyo kuzorotesha kilimo.
NINI KIFANYIKE;
1. Utowaji wa elimu ya mazingira na umwagiaji. Hapa serikali inajukumu kubwa la utowaji wa elimu kuhusu mabadiliko ya hali ya nchi na njia za kukabiliana kama upandaji wa miti,sharia za misitu pamoja na sheria Kali za viwandani na hetekelezaji wake bila kuruhusu mianya ya rushwa, ujenzi wa skimu za umwagiliaji wa kisasa hii itachochea wakulima wengi kuepukana na kilimo cha utegemeaji wa mvua za misimu na kuboresha sekta ya kilimo za uzalishaji wa mazao haya mkakati.
2. Utowaji wa ruzuku na utengaji wa bajeti stahimili .serikali inajukumu kubwa la kurahisisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo hasa kwa wakulima wa mazao mkakati hii inajumuisha utengaji wa bajeti elekezi itakayo simamiwa vyema na utowaji wa ruzuku kwa wakulima pamoja na kushusha kodi kwa wazalishaji wa pembejeo kama mbolea, sumu kuvu na mbegu itachangia hitarahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakati.
3. Utowaji wa Elimu kwa wakulima ianyohusu maswala ya uzalishaji huifadhi na njia za masoko ikowemo serikali kuakikisha usimamizi mzuri wa maafisa kilimo wanapo pangiwa vituo vya kazi na tutatua changamoto wanazo kumbana nazo ikiwemo miundo mbinu mibovu ya Barbara na mazingira magumu ya kazi hii itachangia uzalishaji kuongezeka vyema.
4. Uboreshaji wa miundo mbinu kwani miundo mbinu hiliyoko ni duni amabayo inakwamisha maendeleo ya kilimo.serikali inapaswa kutengeneza barabara na njia zitumikazo kupitisha pembejeo na mazao hili kurahisisha usafirishaji wake.
5. Utowaji wa mikopo. Wakulima wanapaswa kuwezeshwa na serikali mikopo ya kifedha kama kupunguza riba kwenye mikopo inayo husu kilimo, pembejeo,mbugu,miche na mbolea inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao haya mkakati.
6. Ujenzi wa viwanda vya uzalishaji bizaa na uchakataji. Hili kutoa kero ya masoko na poromokaji wa bei za mazao mkakati serikali ingepaswa kujenga viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa na kukabialiana na soko la dunia pindi linapo dorora.
Mwisho kabisa serikali inapaswa kusimamia Sera na mikakati ambayo kimsingi inaweza kuleta chachu yamaendeleo hasa kwenye sekta hii ya kilimo ikiwemo uandaaji wa machapisho na makongamano mbalimbali na utowaji wa ajira unao zinamgatia uwezeshwaji wa maafisa hili elimu iweze kuwafikia wakulima pamoja na serikali kujifunza kutoka nchi zilizo endelea pamoja na kukubali mabadiliko ya zama na njia za kukabiliana nayo.
Note; kura yako ni muhimu kwangu asante

Upvote
1