Mazao yanayolimwa katika jimbo la Alaska huwa ni makubwa sana

Mazao yanayolimwa katika jimbo la Alaska huwa ni makubwa sana

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,475
Mwanga wa Jua unacheza katika nafasi kubwa sana katika ukuwaji mzima wote wa mimea kuanzia nyakati za mbegu, udogo wake na mpaka nyakati zile za ukomavu wake.

Katika kuhakikisha ukuwaji wa mmea ni lazima mchakato wa kisayansi unaoitwa " Photosynthesi " ufanyike ambapo ni kitendo cha mmea kubadiki maji pamoja na mwanga wa jua na carbondioxide kuwa oxygen na sukari ambapo mmea hutumia kama nishati ya kuendesha maisha yake ya kila uchwao.

Nchini Marekani katika jimbo la Alaska hali ni tofauti kabisa na maeneo mengine kwasababu eneo hili la ncha ya kaskazini mwa dunia yetu baadhi ya vipindi vya majira ya mwanga huweza kupokea mwangaza wa jua kwa zaidi ya masaa 20.

Mwangaza wa jua hupotea kwa muda mchache sana halafu huendelea kudumu kwa muda mrefu zaidi , Kwa kitendo hicho mmea hupata faida kubwa sana ya ukuwaji wake tofauti na maeneo mengine ambayo mwangaza wa jua huwa kwa masaa 12 tu basi.

Kutokana na utenge uliopo katika dunia yetu katika nyakati fulani za misimu yake husababisha ncha moja kati ya ile ya kaskazini au ile ya kusini kupata kipindi kirefu sana cha jua tofauti na ncha nyengine, kwa mfano kama kaskazini watapata vipindi virefu vya jua basi kusini kule kwenye bara la antanka watapata vipindi virefu sana vya jua the sama kama majira yatabadilika upande wa kusini basi itaenda sawa kwa kule kaskazini.

Suala hili husababisha mazao mengi sana katika eneo hilo kuwa super big big sana.

Mazao kama maboga, matango, ndimu, pilipili, karoti, na mengineyo huwa yana maumbo makubwa sana tofauti na meneo mengine ya dunia yetu kama huku kwetu Tanzania.

FB_IMG_1665502911408.jpg
 
Hiyo ni Alaska tu? Maana hata juu maeneo ya Norway, Finland na Russia hili ni tukio la kawaida katika mzunguko wa mwaka.

Ukubwa wa tunda hauna uhusiano na photoperiodism, phenomenon hii huwa inasaidia kwenye flowering.
 
H MB
hiyo ni Alaska tu? Maana hata juu maeneo ya Norway, Finland na Russia hili ni tukio la kawaida katika mzunguko wa mwaka.

Ukubwa wa tunda hauna uhusiano na photoperiodism, phenomenon hii huwa inasaidia kwenye flowering.
Ok
 
Fafanua vzri , inawezekana una points..
 
Fafanua vzri , inawezekana una points..
Unataka nifafanue nini? Ikiwa ni photoperiodism hii haina uhusiano na ukubwa wa tunda. Hii hata kwenye mazao kama ya mpunga pia inapatikana. Kuna baadhi ya mbegu huwa haziwezi kutoa maua mpaka daylight iwe kwa masaa fulani.
 
Kwahyo akili zako ndio zimeishia hapo ...[emoji47][emoji47][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom