Maziko ya Ahmed Rajab London Nimekumbuka Mengi

Maziko ya Ahmed Rajab London Nimekumbuka Mengi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU YANGU NIKIANGALIA MAZIKO YA AHMED RAJAB

Allah ana shani yake.
Naangalia hii clip ya maziko ya Ahmed Rajab na imenirejesha nyuma na kunikumbusha mengi.

Namuona hapo Talal mwanae marehemu sasa kijana.

Nakumbuka siku moja asubuhi nimetoka kwangu Finsbury Park hadi Oakwood nyumbani kwa Ahmed Rajab tuna safari ya kwenda Milton Keynes nyumbani kwa Bwana Mjasir ilikuwa khitma yake.

Bwana Mjasir alikuwa kafariki kabla mimi sijafika London.
Talal alikuwa mtoto mdogo labda miaka mitano au sita hivi.

Tukiwa ndani ya treni mtu nzima mmoja tuliokuwa jirani kumuona Talal mtoto mdogo akatoka pakiti ya chocolate akampa.

Talal akapokea akaifungua na kuanza kula.

Tulipofika safari yetu Ahmed Rajab akamwambia mwanae kuwa akipewa kitu chochote na mtu asiyemfahamu asipokee.

Nami nikawa nimepata funzo katika maisha ya Ulaya na kuna mkasa mfano wa huu ulinifika.

Katika khitma alikuwapo Sheikh Mohamed Mlamali Adam na jamaa wengi katika jumuiya ya Zanzibar iliyoko London na wengine wamekuja kutoka mbali.

Baada ya kisomo ikaanguka biriyani.
Mimi nimekaa pembeni ya Ahmed Rajab na Talal.

Nakumbuka Ahmed anamwambia mtoto wake kwa upole, "Talal why are you not eating?"
Talal nami nikimuona alikuwa akidonyoa punje moja moja.

Talal akajibu, "Dad it's greasy."
Talal alikuwa akizungumza Kiingereza kama Mzungu.

Chama Omari Matata alikuwa akisema yeye anasikia raha sana kumsikiliza Talal na ile "accent" yake ya London.

Leo namuona hapo Talal kwenye maziko ya baba yake kijana mtu nzima.
Talal alipooa baba yake alinipigia simu kunieleza kuwa rafiki yangu anaoa.

Namuona hapo Abdilatif Abdalla na Ali Saleh.

Allah ana shani yake sikujua katika miaka ile kuwa rafiki zangu wawili Balozi Ramadhani Dau na Hamza Rijal walikuwa wameoa dada zake Ahmed Rajab.

Allah atupe subra sote.
Amin.


View: https://youtu.be/8HhI58DXY6w
 
Mwenyezi Mungu ampokee mja wake, ndugu yetu Ahmed Rajab. Lakini pia awajalie moyo wa subra familia yake, ndugu, jamaa na marafiki. Sote ni Mwenyezi Mungu na Kwa Mwenyezi Mungu tutarejea.
 
Back
Top Bottom