SoC02 Mazingira na Afya yetu

Stories of Change - 2022 Competition

Proffessa

New Member
Joined
Jul 10, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Mazingira; Ni vitu vyote vinavyo mzunguka kiumbe hai.Tunayategemea mazingira, tunaishi ndani yake, hapana Shaka bila ya mazingira maisha yetu hayawezekaniki, pengine niseme, Sisi ni watoto wa mazingira, nayo ndiyo Mama yetu anayetulea Kwa kutupatia kila tunachokihitaji, hata hivyo katika Mazingira vipo vitu vingi hasa, vingine hata hatujui kazi na matumizi yake.

Mazingira na wala sio mazingara, hapa tunazungumzia vitu vyote vinavyotuzingira, vinavyotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku, vitu hivyo vyaweza kuwa vya asilia au vilivyoundwa na binadamu. Ila vyote huitwa mazingira.

Vitu vya asili vinavyotuzunguka(tukiviita mazingira asilia hatukosei) ni Kama vile uoto wa asili ndio hiyo Mimea, Wanyama wa mwituni na wakufugwa, Ardhi na maumbo ya Dunia Kama vile milima, mabonde, miinuko n.k, Bahari, Mito, maziwa , Tabia ya nchi, Hali ya hewa, miongoni mwa mengini.Kwa upande wa vitu vilivyoundwa na binadamu ni Kama vile Nyumba, barabara, magari, viwanda miongoni mwa vitu vingine.

View attachment 2338281

Pasipo mazingira maisha hayawezekaniki Kwa sababu:

i) Mazingira hutupatia chakula ndio maana tunaitumia Ardhi kujipatia chakula kupitia kilimo.
picha: www.chrome.com

ii) Hutupatia hewa Safi ya Oksijeni (wanyama) na hewa ya makaa/Carbon monoxide (Kwa wanyama)

iii) Hutupatia mahali pakuishi , mahali pa kuendeshea shughuli zetu na malighafi za ujenzi wa makazi yetu.www.chrome.com

iii) Hutupatia Dawa kutoka kwenye Mimea
iv) Hutupatia Hali ya hewa na tabia ya nchi nzuri Kwa kutupatia, mvua, upepo mwanana, mwangaza mzuri wa jua unaotupa vitamini D na kutupatia nishati ya umeme wa jua.

picha:www.chrome.com
v) Hutupatia chakula na malighafi kutoka Kwa wanyama

vi) Hutupatia maji ambayo huendesha maisha yetu.


picha:www.chrome.com


Miongoni mwa faida nyingine:

Mazingira yanafaida kubwa kwetu ikiwa tutayatunza. Tofauti na hapo mazingira huweza kugeuka jinamizi baya litakalotuathiri Kama sio kutuangamiza Sisi wenyewe.

Utunzaji wa Mazingira huchangia Kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na Kisiasa katika maisha yetu.

Kutokunza Mazingira ni Kama kusema kutokuitunza maendeleo ya nchi yetu. Kutunza mazingira ni kuyaweka mazingira katika hali itakayoleta manufaa Kwa kizazi kilichopo na kinachokuja

Mambo makuu yanayoathiri mazingira Kwa sehemu kubwa ni Kama ifuatavyo;

1. Ongezeko kubwa la watu
Nimeipa hoja hii nafasi ya Kwanza kwani, Ongezeko kubwa la watu husababisha mahitaji makubwa ya Rasilimali katika Mazingira.Kama Ongezeko kubwa la watu lisipodhibitiwa ni wazi hatutoweza kudhibiti uharibifu wa mazingira.



picha;www.chrome.com

2. Shughuli za kibinadamu
Kama vile kilimo, usafirishaji, ujenzi wa makazi na miundombinu, uvuvi, uchimbaji Madini, huchangia Kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira. Kwa kufanya uchafuzi wa mazingira,mmomonyoko wa Ardhi, ukataji miti n.k


picha:www.chrome.com

3. Migogoro na Vita
Kugombania Rasilimali ni moja ya mambo yanayoathiri mazingira.Vita na migogoro mingi dunia imechangiwa na watu kugombea Rasilimali.Vita huathiri mazingira moja Kwa moja kutokana na Ulipuaji na uchomaji Moto unaofanyika wakati wa mapambano.

4. Majanga ya kiasili
Kama vile mafuriko, Tufani na vimbunga, Ulipukaji wa Volcano miongoni mambomajangamengine.
picha:www.chrome.com

''kumbuka''Taifa letu ambalo linashikilia nafasi ya tano Kwa idadi kubwa ya watu ambayo ni takribani milioni 60 kulingana na Worldometer, lazima tuweke mikakati ya kukabiliana na Ongezeko hili katika utunzaji wa Mazingira na Mabadiliko ya tabia nchi.Huku tukijua kuwa Sisi tunaongezeka lakini Rasilimali haziongezeki na Kama zipo zinazoongezeka basi huongezeka polepole.Kama nilivyosema kutunza mazingira ni kutunza maendeleo ya nchi yetu.

Sasa tutawezaje kuyatunza mazingira yetu, na Kwa kivipi utunzaji huo utatupa maendeleo katika jamii na Nchi yetu, embu tuone Kwa kifupi;

1. Serikali itoe elimu ya mazingira ndani ya jamii na umuhimu wake.
Serikali inapaswa itoe elimu ya mazingira Kwa wananchi katika mifumo mbalimbali; mathalani

1.1. Kwenye mtaala wa elimu, serikali iweke mada na kozi ya mazingira Kama moja ya kozi muhimu na yalazima Kwa kila Mwanafunzi kuisoma.Wanafunzi wafundishwe namna ya kuyatunza na kuyatumia mazingira Yao Kwa manufaa yao na taifa Lao.Hii itasaidia wanafunzi kuweza kujiajiri kwani wataweza kuyatumia mazingira yao pindi wamalizapo shule.



picha:www.ubongokids.com

1.2. Serikali iweke sheria Kali Kwa waharibifu wa mazingira.


picha:www.chrome.com

Baada ya kuwekeza kwenye elimu kinachofuata kiwe ni Sheria Kali Kwa waharibifu wa mazingira. Adhabu Kali itolewe Kwa waharibifu wa mazingira.

1.3. Serikali itengeneze matamasha yatakayohamaisha utunzaji wa Mazingira na Usafi wake kupitia vyombo vya habari, na kupitia watu mashuhuri.picha:www.chrome.com

2. Taasisi za Kidini na Asasi za kiraia zihamasishe watu kutunza mazingira.
Kwa nchi yetu watu wengi ni watiifu mbele ya Imani zao, hii ni kusema mpaka kizazi cha sasa bado dini inaushawishi mkubwa Kwa kundi kubwa la watu kwenye jamii. Viongozi wa dini wahamasishe waumini wao kutunza mazingira karibu kila juma waendapo ibada.Makanisa na misikiti iwe mifano hai Kwa kuwa na mazingira mazuri, Kama vile makanisa na misikiti kuzungukwa na miti iliyopandwa Kwa mpangilio mzuri kabisa.Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali, yahamasishe na kutia washaa kuhusu utunzaji wa Mazingira
picha:www.chrome.com

3. Kila serikali za mitaa iweke sheria ndogo zitakazofuatwa Kwa lazima kuhusu upandaji wa miti.
Serikali itoe muongozo na sheria kuwa walau kila nyumba uwepo miti miwili au mitatu, kalingana ukubwa wa kiwanja.



picha:www.chrome.com

4. Mfumo wa utupaji taka uboreshwe na kuwekewa utaratibu mzuri.
Baada ya elimu kutolewa, serikali kuu na serikali za mitaa, iweke sheria na ihakikishe kila nyumba inamfumo mzuri wa utupaji wa taka au Kama kuna makampuni ya Usafi/uzoaji taka yahakikishe kila baada ya siku mbili na zisizidi tano yanakuja kutoa taka kwenye nyumba za watu.

picha:www.crome.com

5. Serikali idhibiti Uhamaji kutoka vijijini kwenda miji mikubwa ambao unasababisha mlundikano wa watu ambao huathiri mazingira kivyovyote vile.Serikali iboreshe miundombinu na Huduma za kijamii nje ya Mji au kujenga kila kanda au Mkoa majarara.


picha:www.crome.com

6. Wasanii na watu mashuhuri.
Wapewe semina ya elimu ya utunzaji mazingira kisha wapewe posho Kwa kuhamasisha utunzaji wa Mazingira.

7. Maafisa Ugavi waajiriwe kila kata na wawe na vipindi maalumu kutoa elimu ya muhimu kuhusu kilimo chenye Tija na kitakachotunza Ardhi, ilitoe mazao mengi na kuwa na rutuba.

8. Serikali itoe fursa Kwa Vijana na kuwaajiri hata Kwa mkataba wa muda mfupi, wapande miti Kando Kando ya Barabara hasa zile highway na kuwapa posho.Kila wilaya iwe na Vijana wa upandaji wa miti Katiba barabara kuu.Mfano, kijana mmoja apewe urefu wa barabara wa kilometa mbili mpaka tatu kupanda miti zenye muachano WA nguzo za umeme. Wapewe posho Kama sio Mshahara.

picha:www.chrome.com

9. Maeneo yote yanayotoa Huduma za kijamii iwe niyaserikali au ya selta binafsi yawe na mazingira mazuri Kama upandaji wa miti na Bustani zitakazovutia na kuhamasisha watu wa eneo husika.Serikali iweke ni lazima Maeneo ya kutolea Huduma yawe za mazingira mazuri na upandaji WA miti kulingana na ukubwa wa eneo.Maeneo Kama ya Hospitalini, makanisani, misikitini, shuleni, mahakamani, vituo vya daladala, masoko miongoni mwa mengine.picha:www.chrome.com

10. Adhabu za faini Kwa watupa taka zipewe nguvu Kwa kila mji.

picha:www.chrome.come

Faida za kutunza mazingira zinazotarajiwa;

1. Tabia ya nchi kuwa mzuri na yakuvutia inayotabirika, Kama uwepo wa mvua za uhakika zisizo na madhara, Hali ya hewa ya joto au baridi, au upepo mzuri kulingana na eneo.

2. Ukuaji wa Kilimo.
Utunzaji wa Mazingira hupelekea kukua Kwa kilimo kutokana na Ardhi yenye rutuba kwani itatunzwa, uwepo wa mvua zinazotabirika.Hii itasababisha nchi kuwa na chakula Kwa uhakika na kujipatia malighafi ya viwandani na chakula cha kuuza nchi zingine.



picha:www.chrome.com

3. Ajira zitaongezeka
Vijana wa sasa huwezi ukawaambia walime kwani wanajua Hali ya hewa haitabiriki,
Lakini mazingira yakitunzwa vizuri moja Kwa moja mambo yatajiweka sawa. Vijana watajiajiri kwenye Kilimo kwani mvua zinaeleweka, Vijana watajiajiri kwenye ufugaji kwani hapatakuwa na magonjwa ya ajabu ajabu ya milipuko Kwa mifugo.Vijana wengine watajiajiri kwenye kuuza miche na kupanda miti kwani itakuwa ni lazima kila nyumba au mahali pakutolea Huduma kuwa na miti.Wengine watajiajiri kupitia ujasiriamali.

4. Maradhi yanayosababishwa na mabadiliko ya Tabia nchi na Magonjwa ya milipuko ya kuambukiza yatapungua.Utunzaji wa Mazingira hupunguza magonjwa Kama ya kipindupindu, Typhoid na minyoo pamoja na Magonjwa yanayotokana na tabia ya nchi.picha:www.chrome.com

5. Kupungua Kwa ujangwa na baa la njaa.
Utunzaji wa Mazingira kutapunguza baa la njaa kwani watu watapata chakula cha kutosha na wanaelimu ya kukitunza chakula hicho. Pia upandaji. wa miti utapunguza Hali ya ukame na ujangwa.
picha:www.chrome.com

6. Mpangilio mzuri wa mipango miji na kupunguza athari za ujenzi holela.
Elimu ya utunzaji mazingira itasaidia pia makazi ya watu kujengwa katika mpangilio mzuri na taaluma za ujenzi.Hasara za watu kubomolewa makazi yao itapungua Kwa sehemu kubwa. Utunzaji wa Mazingira ni pamoja na kujenga makazi katika mpangilia maalum.Pia kutapunguza matatizo ya mafuriko kwani watu watajenga mahali sahihi na sio kujenga mabondeni. Athari za Mali kusombwa na mafuriko na vifo vitapungua Kwa kiasi kikubwa.
picha:www.chrome.com
Vifuatavyo ni baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wa mazingira hasa majumbani kwetudawa za kuulia wadudu na glovesndoo za kudekia na dekio lake
mapipa ya taka na mifagio n.k

makala hii imeandaliwa na frances malima
''mazingira yetu afya yetu''
email:francesmalima.gmail.com
nashukuru sana🙏🙏
 

Attachments

  • IMG_20220829_123534.jpg
    87.4 KB · Views: 3
  • IMG_20220829_125306.jpg
    19 KB · Views: 3
Upvote 1
jamani story of change ya kwangu hiyo naomba saport yenu wadau🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…