DMmasi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 561
- 900
Salamu wanajamvii
Mabadiliko ya kimiundombinu au miji ni sehemu pia inayogusa mazingira yanayotuzunguka moja kwa moja.
Nikigusa moja kwa moja kwenye jiji ambalo nipo na limefanya niwasilishe kero/tatizo/kadhia hii ambalo ni jiji la Dodoma kuna tatizo kubwa la utunzaji wa taka.
Utaratibu wa kutunza taka kwanzia majumbani haueleweki jambo linalopelekea taka kusambaa mitaani hasa kwenye viwanja ambavyo bado havijaendelezwa
Kwa kifupi kabisa Dodoma ni jiji ambalo ndolinakuwa hivyo basi mitaa mingi hukuwa na kuchangamka kutokana na miundombinu iliyopo mfano mtaa unaweza ukakuwa kwa kasi sababu kuna kiwanja cha ndege maeneo hayo au barabara.
Uchangamfu huo hupelekea ongezeko la watu hivyo taka huongezeka pasi na maeneo ya utunzaji taka kuongezeka.
Je? taka raia wanazitupa wapi, mji ukichangamka kuna baadhi ya viwanja ambavyo wenye kuvimiliki huchelewa kuviendeleza huko ndiko hugeuka kuwa majalala ya kutupa taka
Binafsi sijaona utaratibu mwingine ambao tutasema basi umeshindwa kufuatwa yaani sijawahi kuona gari la taka tunapoishi.
Mwisho wa bandiko hili kuna picha ambazo ni mfano wa maeneo yanayogeuka majalala taratibu
Kwa mtizamo wangu na uhalisia tatizo hili limeanzia hapa watu hawaruhusiwi kuchimba majalala majumbani kwa dhana ya kwamba taka zikijaa wachome moto ila taka hukusanywa ikiwa pakupelekwa hapaeleweki.
Mfumo wakuziondoka taka hizo ni watu binafsi waliolichukua kama fursa ambao huzichukua taka hizo wengine kwa kutumia guta, mikokoteni au pikipiki,
na wengi huzichukua majira ya usiku sababu wanaenda kuzitupa maeneo yasiyo rasmi.
Ombi langu kwenda kwa serikali ni nini ikiwa basi wameamua watu wasikae na taka majumbani yani wasichimbe majalala kila mtaa utengewe eneo moja ambalo litatumika kutunza taka, ambapo taka hizo zitakuja kuchukuliwa na magari haya ya kuzoa taka na kwenda kuzihifadhi kwenye maeneo husika.
Hili litawapa fursa wale wanao zoa taka majumbani kwa watu kuwa na eneo rasmi la kuziweka na siyo holela holela, na pia maeno hayo tengefu yawe na usimamizi kwani pesa za kujiendesha zitaanza kutokea uko pia sababu wanao zoa taka hawazoi bure.
Tusisubiri mpaka tatizo liwekubwa ndotuanze kunyoosheana vidole.
Kwa hayo machache naomba kuwasilisha