Mazingira ya biashara Tanzania

Mazingira ya biashara Tanzania

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Salaamu kwenu!

Moja kwa moja kwenye Mada.

Mheshimiwa Rais najua unapitapita humu JamiiForums au hata watu wako wa karibu pia.

Nina ombi moja kwako kuhusu hali ngumu ya Biashara hapa nchi kwa hivi sasa.
Tunajua wewe ni Rais wa wanyonge jaribu kuwa na jicho huruma kwa wafanyabiashara wadogo.

Kodi zimekuwa kubwa mno na kiwango cha juu sana kiasi kwamba hvi sasa watu wanafunga Biashara zao na hakuna zinazoanzishwa. Umaskini unazidi kukidhiri.

Tunakuomba Waziri wa fedha mfikishie salamu mheshimiwa Rais, tunaomba mpitie tena kwa mpango wa dharura hali za Biashara kwa wafanyabishara wadogo. Punguzeni kodi kwnye bidhaa muhimu, za matumizi muhimu ya kila siku, nguo vifaa vya Ujenzi na vyakula.

Ondoeni kodi kulipwa kabla ya kuanza Biashara hapa si kwamba mtu hata lipa la hasha, bali baada ya miezi mitatu kagueni Biashara hiyo mpya na kumkadiria mtu kodi anayostahili.

Tanzania tumebarikiwa bandari, vitu vyote vinaingia hapa ndipo viende nchi jirani kama Uganda, cha kushangaza [emoji853]bidhaa zetu hapa ni ghali kuliko huko uganda ambapo bidhaa hizo zinapita hapa nchini kwetu na kusafirishwa kwa umbali mrefu. Kukuhakikishia hili kuna wafanyabiashara wa Tanzania hufuata bidhaa Uganda na kuja kuuza Tanzania na kupata faida kubwa, hvi kwa nini hamtusaidii tujivunie kuona faida ya kuwa na bandari??

Punguzeni kodi walau kidogo, Tanzania iwe ni centre ya wafanyabiashara toka nchi zinazotuzunguka kuja kununua bidhaa kwetu kama ilivyokuwa Kariakoo ya hvi karibuni. Rwanda hawana bandari lakini bidhaa zao Bei ni kama Tanzania au hata chini ya hapo!
Mafuta ya magari ni Bei nafuu kenya, Mombasa kuliko Tanga, Tanzania.
I
Kodi inatakiwa iwe fair, rate ndogo ambazo mlipaji kufikiri kuzikwepa.

Maisha mnayoishi nyinyi naamini wengi hamfahamu taabu wanazopata wafanyabiashara wadogo.

Mnaumiza watu na kodi zenu kubwa na mazingira mabovu ya Biashara.
 
Atakusikia kweli mkuu....hashauriki ngoja tuelekee Zimbabwe tu hamna namna...[emoji125]
 
[emoji28][emoji28]
Jiwe halitaki kujifunza,mfano Dubai wao ni free port lakini wanavuna mamilioni ya dola kwa visa zitolewazo huku wageni wengi wanaoingia kwa biashara huja kununua hivyo mzunguko wa pesa unaambukiza biashara maelfu kwa mfano ajira ya kufunga mizigo tu madukani,biashara ya vyakula na vinywaji mahoteli na usafiri wa ndani kama taxi nakadhalika baadaye utalii, kampuni za kusafirisha mizigo na clearing agents,madalali nk watu wa maduka nk.hapo sasa ndo unatoza kodi
 
Ngoja nami nichomekee, GETI LA MARENDEGU MKOA WA LINDI NI JIPU KWA WAJASIRIAMALI WANYONGE WA MIKOA YA KUSINI, UKIPITA NA KAMZIGO KA KILO 200 CHA KOROSHO BILA YA USUMBUFU WEWE UNA MUNGU, HATA KAMA UNA RISITI YA USHURU NA UMELIPIA ULIPOTOKA, HAPO LAZIMA UBAKI NA MZIGO WAKO!
 
Salaamu kwenu!

Moja kwa moja kwenye Mada.

Mheshimiwa Rais najua unapitapita humu JamiiForums au hata watu wako wa karibu pia.

Nina ombi moja kwako kuhusu hali ngumu ya Biashara hapa nchi kwa hivi sasa.
Tunajua wewe ni Rais wa wanyonge jaribu kuwa na jicho huruma kwa wafanyabiashara wadogo.

Kodi zimekuwa kubwa mno na kiwango cha juu sana kiasi kwamba hvi sasa watu wanafunga Biashara zao na hakuna zinazoanzishwa. Umaskini unazidi kukidhiri.

Tunakuomba Waziri wa fedha mfikishie salamu mheshimiwa Rais, tunaomba mpitie tena kwa mpango wa dharura hali za Biashara kwa wafanyabishara wadogo. Punguzeni kodi kwnye bidhaa muhimu, za matumizi muhimu ya kila siku, nguo vifaa vya Ujenzi na vyakula.

Ondoeni kodi kulipwa kabla ya kuanza Biashara hapa si kwamba mtu hata lipa la hasha, bali baada ya miezi mitatu kagueni Biashara hiyo mpya na kumkadiria mtu kodi anayostahili.

Tanzania tumebarikiwa bandari, vitu vyote vinaingia hapa ndipo viende nchi jirani kama Uganda, cha kushangaza [emoji853]bidhaa zetu hapa ni ghali kuliko huko uganda ambapo bidhaa hizo zinapita hapa nchini kwetu na kusafirishwa kwa umbali mrefu. Kukuhakikishia hili kuna wafanyabiashara wa Tanzania hufuata bidhaa Uganda na kuja kuuza Tanzania na kupata faida kubwa, hvi kwa nini hamtusaidii tujivunie kuona faida ya kuwa na bandari??

Punguzeni kodi walau kidogo, Tanzania iwe ni centre ya wafanyabiashara toka nchi zinazotuzunguka kuja kununua bidhaa kwetu kama ilivyokuwa Kariakoo ya hvi karibuni. Rwanda hawana bandari lakini bidhaa zao Bei ni kama Tanzania au hata chini ya hapo!
Mafuta ya magari ni Bei nafuu kenya, Mombasa kuliko Tanga, Tanzania.

Kodi inatakiwa iwe fair, rate ndogo ambazo mlipaji kufikiri kuzikwepa.

Maisha mnayoishi nyinyi naamini wengi hamfahamu taabu wanazopata wafanyabiashara wadogo.

Mnaumiza watu na kodi zenu kubwa na mazingira mabovu ya Biashara.

Kwa kweli biashara nyingi zimeyumba sana. Serikali ipo kwa ajiri ya kusikiliza, kuwatumikia na kutatua matatizo ya wananchi wake.

Hivyo natumaini serikali itasikiliza huu wito wako.

Ni matumaini yangu idara na taasisi zote husika zitakaa chini pamoja na kuangalia the whole taxation policy kwa umakini na haraka iwezekanavyo.
 
Hakuna wakukusikiliza awamu hii, bora uwa chinga tu uuzie kando ya barabara ili kukimbia unyanyasaji wa TRA.
 
Back
Top Bottom