The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Mazingira ya kuajiriwa ama kujiajiri Tanzania ni magumu sana.
Kwanza, Serikali imehodhi shughuli karibu zote za kiuchumi, leo kandarasi zote za ujenzi wa ofisi za umma inapewa TBA, NHC, Ardhi University au taasisi nyingine za umma. Kwenye ufundi wa vyombo vya moto na elektroniki ni TEMESA, kampuni binafsi kupata kazi labda TEMESA wazidiwe na hapo itahitajika rushwa nyingi sana.
Ukija kwenye kandarasi kubwa utakutana na makampuni makubwa ya kijerumani kama Strabag, Kenoike ya Japan, na mengine ya Kichina, watanania wanabaki kua ni saidia fundi kwa sababu ya mitaji midogo.
Tanzania kijana akimaliza chuo na ana mtaji hawezi kuanzisha kampuni, mfano engineer hawezi kuanzisha kampuni, sheria ama taratibu zinamtaka kwanza aajiriwe apate uzoefu, yaani hawezi kuaminika hadi aajiriwe kwanza kwa miaka kadhaa ndio aweze kusimama mwenyewe. Taratibu zinataka kwanza mtu aajiriwe wakati huo huo ajira hakuna. Yaani hata ukiwa na mtaji bado changamoto ni lukuki.
Daktari amemaliza mazoezi Muhimbili, ana mtaji akitaka kuanzisha hata chumba cha kuchoma sindano tu haruhusiwi, anatakiwa aajiriwe kwanza apate uzoefu. Taratibu zinamtaka mhitimu kuajiriwa kwanza ndio ajiajiri.
Unaweza kua mhasibu serikalini kwa miaka zaidi ya 20, unaandaa hesabu zako kwenda kwa CAG na anazipoke vizuri, siku ukitaka kuacha kazi ujiajiri NBAA inakukaba koo, inataka uwe na cheti au ngazi ya public practice.
Taratibu nyingi za Tanzania zinamtaka mtu awe amejiriwa kwanza ndio aweze kujiajiri, yaani upate uzoefu kupitia kuajiriwa ndio ujiajiri upate kandarasi za serikali.
Ajira hakuna, serikali imefikia kwenye ceiling haiwezi kuajiri zaidi, private sector iko crippled pamoja na kua siku zote ilikua fragile.
Taasisi ama mifumo ya Tanzania haitambui ubunifu, inatambua zaidi vyeti. Ndio maana unakuta watumishi wa serikali wengi ni bogus, hawana ubunifu wowote lakini kwa kua serikali inajali vyeti mtu anafanya juu chini anapata cheti cha elimu anapanda cheo, creativity sifuri.
Ndio maana utakuta models nyingi na programu nyingi tunaajiri washauri kutoka nje wenye elimu ndogo sana kuja kufundisha maprofesa wetu hapa Tanzania.
Vijana tuchague viongozi watakaotutoa kwenye haya mazoea na kutengeneza fursa kwa ajili ya keho yetu. Kuna watu wametufikisha hapa lazima tuwakatae.