Mazingira yana mchango gani katika kukujenga au kukubomoa?

Mazingira yana mchango gani katika kukujenga au kukubomoa?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Kuna utofauti mkubwa kati ya fursa anazokutana nazo mtoto aliyezaliwa New York(USA) na mtoto aliyezaliwa Dar es salaam(TZ).

Mafanikio ya mtu ni matokeo ya vitu vingi ila miongoni mwa hivyo vitu ni mazingira yanayomzunguka hususani Jamii. Jamii Ina mchango mkubwa sana hususani mitazamo na daily routines ya sehemu husika.

Let's take an example ukiwa mmasai automatically mentality inaanza kuamini kwenye ufugaji the same ukiwa mchaga au mkinga unaanza kuswitch kwenye biashara hiyo ni impact inayotokana na mazingira yaliyokuzunguka.

That's why Kuna baadhi ya Jamii ni ngumu kutoka kwenye umasikini they believe umasikini ni sehemu ya maisha yao. Tatizo linaanzia kwenye mazingira waliyoyakuta.

Sio Kwa ubaya ila Kuna mazingira ukiwa unaishi unajiona kabisa kuwa day after day kuna kitu unapoteza kuliko kuongeza. mfano mzuri mkiwa vyuoni unaweza mtabiria mtu mafanikio kutokana na lifestyle yake mkija kumaliza chuo Kila mtu akarudi kwao unakutana na huyohuyo mtu akiwa kachoka mipango yake yote imekufa mpaka unajiuliza imekuwaje kumbe shida ni mazingira aliyoenda kukutana nayo kwenye Jamii yake.

Why wanamziki wanaamini kuishi Jijini Dar es salaam Kuna waboost katika mziki? Jibu ni mazingira ya Dar es salaam yapo friendly kuwawezesha katika kufanikisha sanaa yao. Mkitaka kuthibitisha hilo waambieni kila msanii arudi Kijijini kwao kuna baadhi ya wasanii umaarufu wao utapotea kama upepo.

Be careful na mazingira uliyopo pengine ndio chanzo Cha anguko lako.
 
Back
Top Bottom