SoC02 Mazingira yetu, afya yetu,wajibu wetu

SoC02 Mazingira yetu, afya yetu,wajibu wetu

Stories of Change - 2022 Competition

C87

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
6
Reaction score
1
MAZINGIRA YETU, AFYA YETU,WAJIBU WETU:

Afya zetu ni muhimu sana kwa ajili ya kesho yetu,kwani afya bora ndiyo chanzo cha uhai bora,tabasamu na bashasha njema kwa familia,ndugu na marafiki zetu.

Afya ya kweli ni lazima izingatie mambo kadhaa kama yafuatayo.

1. ULAJI MZURI WA CHAKULA (KULA KWA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA)
Wapo watu ambao hawazingatii kwa kula kwa mpangilio,kulingana na wataalamu wanavyo shauri,na ulaji huo umekuwa ukisababisha magonjwa,ongezeko la uzito katika miili ya watu,hivyo namna bora ya kuushinda ulaji wa namna hii ni kuzingatia hatua na kanuni kadhaa za wataalamu wa afya.Kwani lishe bora ndiyo chanzo ya jamii yenye afya katika lolote lile.

Hivyo ni muhimu Zahanati,Hospitali zile za Serikali na binafsi kutoa semina,warsha mbalimbali kuhusu lishe bora kwa jamii inayowazunguka mara kwa mara, jamii inayofundishwa mapema lishe bora ina uwezekano mkubwa wa kuwa walimu wa wengine katika siku zijazo.

Kwani kuna ongezeko la Watoto katika jamii wanashida ya lishe kitu ambacho kimesababisha utapia mlo, Wizara ya afya ni muhimu kutoa elimu lishe mara kwa mara.

2. UMUHIMU WA KUPIMA AFYA ZETU MARA KWA MARA:
Umuhimu wa kujali afya zetu ni muhimu sana hasa kwa kuzingatia mara kwa mara, jamii tuliyo nayo wakati Fulani inajitibia yenyewe bila kuzingatia utaalamu wa wataalamu wa afya,mfano wakati mwingine unakutana na mtu kichwa kinamsumbua anakimbilia kunywa Panadol, wakati ugonjwa unaomsumbua ni mwingine,uzembe wa kutokupima mara kwa mara ndiyo chanzo cha vifo vya mapema katika jamii yetu.Ni muhimu wakati wote kuwatembelea wataalamu wa afya na kupima afya zetu,kwani tiba yenye uhakika usababisha kutibu, ugonjwa uliogundulika.

HASARA ZA KUNYWA DAWA BILA VIPIMO HUSABABISHA:

1. Sumu mwilini.

2. Udhaifu katika mwili.

3. Kusababisha tatizo jipya katika mwili wa binadamu.

Hivyo tunapohisi udhaifu wowote katika mwili tusiache kutembelea vituo vya afya ambavyo vina matibabu yenye uhakika kwa kuzingatia upimaji bora wa afya.

3. UNYWAJI BORA WA MAJI SAFI NA SALAMA:
Asilimia 75 ya mwili wa mwanadamu unategemea maji, Mungu ameuumbia hivyo, suala la kunywa maji kila wakati ni muhimu na wataalamu mbalimbali wanashauri hivyo,sasa hili afya ya mtu iwe nzuri kila wakati ni lazima unywaji wa maji safi,uzingatiwe.Yapo maji machafu ambayo yana vimelea mbalimbali vya magonjwa na wakati mwingine kusababisha homa ya matumbo,kipindupindu na “UTI” Hivyo suala la maji safi na kuchemsha kwa ajili ya matumizi ya kunywa ni muhimu sana, Jamii inapaswa kunywa maji safi na salama kila wakati.

4.UMUHIMU WA KUZINGATIA CHANJO MBALIMBALI ZINAZOTAMBULIKA NA WIZARA YA AFYA ILI KUZUIA MAGONJWA NYEMELEZI.
Zipo chanjo kadhaa mfano chanjo za manjano,surua ,pepo punda nk,zipo zinazotolewa wakati wa ujauzito na zile zinazotolewa wakati mtoto amekwisha kuzaliwa, ni wajibu wetu kuzngatia chanjo hizi kadri wataalamu wetu wanavyotoa ushauri kwetu, zipo chanjo nyingine za kumeza vidonge kuzuia matende,mabusha ni wajibu wetu tuzingatie chanjo hizi kila wakati pindi zinapotolewa na wataalamu wa afya wanaotambulika na serikali.

5.TUZINGATIE MUDA MZURI WA KUTOSHA WA KUPUMZIKA KWA AJILI YA KULINDA AFYA ZETU.
Moja ya vitu tunavyopaswa kuzingatia kwetu ni pamoja na kupata muda mzuri wa kutosha wa kupumzika (kulala) kwani ulalaji bora ni sababisho la kuleta afya bora kwa binadamu, wataalamu mbalimbali wanasema muda mzuri wa mwanadamu anapaswa kupumzika masaa sita hadi nane, ulalaji usiozingatia kanuni bora za afya unasababisha magonjwa, ukosefu wa ufanisi bora na hata uvivu.

6.UMUHIMU WA MAZOEZI KWA AJILI YA KUUPA MWILI UTIMAMU WA AFYA BORA.
Wakati mwingine changamoto ya kutokufanya mazoezi inaweza kusababisha mwili kupata magonjwa mbalimbali ya gafla ili kuepuka magonjwa hayo ni muhimu kila wakati kufanya mazoezi ili kuzuia magonjwa hayo ambayo wakati mwingine yanaepukika kwa njia ya kufanya mazoezi mbalimbali, hata kama siyo kwa kukimbia basi ni kwa njia ya kutembea kwa dakika kadhaa au masaa kadhaa ili kuupa mwili utimamu wa kuwa na afya njema .

7.UMUHIMU WA KUSAFISHA MAZINGIRA YETU YANAYO TUZUNGUKA KATIKA JAMII YETU ILI KULINDA AFYA ZETU MARA KWA MARA.
Kusafisha mazingira yanayotuzunguka kila wakati ni wajibu wetu wa kila wakati ili kulinda afya zetu, mazingira machafu ndiyo chanzo cha magonjwa kadhaa mfano “MARALIA”,KIPINDUPINDU, MAFUA NA KIKOHOZI, Jamii yenye maono kwa watu wao ni lazima izingatie suala zima la afya ,Usafi ni suala la kila mmoja,kufyeka nyasi,kusafisha mitaro kila wakati kwa ajili ya kuondoa uchafu, Mazingira machafu ndiyo chanzo cha wadudu wakali na hatarishi, hivyo tuhakikishe tunatunza mazingira yanayotuzunguka.

8. ELIMU YA MAZINGIRA KWA AJILI YA KULINDA AFYA ZETU.
Uchafuzi wa mazingira katika jamii yetu hasa suala zima la kujisaidia barabarani ni jambo linalosababisha mlipuko wa magonjwa na kuua afya ya mimea ,hivyo ni wajibu wetu kutoa elimu kwa jamii ili kutokusababisha uchafuzi wa mazingira,ambao utaathiri afya zetu ,ni wajibu mkubwa kuzingatia hili.
 

Attachments

  • Maji.jpg
    Maji.jpg
    5.7 KB · Views: 5
Upvote 0
Back
Top Bottom