Mazishi/ misa ya Ivani live spark tv

Hii sijui imekaaje nafikiri kisheria kuzika au kuchoma hela jela inakuhusu
 
kuna mama mmoja mkoa flani hapa tz..alikuwa na mibiashara yake ya maana...na kwa bahati mbaya umri ulikua unaenda bila kuolewa lakini akabahatika kupata mtoto wa kike mmoja tu..na mtoto ndo akawa furaha yake....ikawa mama akienda congo au nigeria katika mzigo lazima kuwe na zawadi za mtoto na ni vitu very expensive..akienda dubai anamjia na set za gold..
alimpenda sana mwanae..

siku ghafla bila kutarajia mwanae akiwa na miala kama mitano akapata ajali nakufariki.
mama alishindwa kuhimili aisee.
wakaenda kuzika kijijini kwa bibi na babu..wakati wa kuzika mama huku hajiwez akatoa mfuko una set ya vitenge vya wax vizuri sana alichotarajia kuja kumpa ila mauti yakakwamisha..akatoa na seti za gold halisi nzito...akaviwelka ndani ya jeneza juu ya mtoto.
kuulizwa vipi akasema hivi ni halali ya mwanangu tu..
wananchi wakazika.
WAKAENDA KULALA USIKU KUAMKA ASUBUHI WANALETWWA TAARIFA KABURI LIMEFUKULIWA NAJENEZA LA MTOTO LIMEVUNJWA LIKO PEMBENI.KWENDA KUANGALIA VITENGE NA GOLD HAVIPO.
 
Hivi sheria zetu zinaruhusu suala hilo kwanza? Nilishawahi kusikia kuwa kuchana hela makusudi ni kosa kisheria hapa Tz [sina uhakika na hilo pia]. Vipi kuhusu kuzikwa nazo?
Kama ni kweli basi huo ni uchizi, mkataba (pesa) ni wa kwangu, nimeamua kuu-forfeit (kuuchana), which means ni faida kwa serikali, kwani nime forfeit ile haki yangu ya kudai huduma/bidhaa kwenye soko ambayo hupunguza inflation. Jiulize tu, kwanini serikali inakusanya kodi? Kwanini wasiwe tu wanachapisha pesa na kulipa mishahara, kujenga mabarabara, mashule na mahospitali? Kwanini wanahangaika kukaba watu kodi wakati wanaweza wakachapisha tu hizo pesa??! Jiulize usiwe kama msukule asietumia akili, jiulize hata kidogo tu..!!
 

Pathetic! Nilienda shule, na shule yangu ndiyo ilinifunza kuona vitu katika muktadha wake halisi! Hilo unaloita "karatasi tu" angepewa yatima, mlemavu, nk lingemsaidia kutatua tatizo lake la kukosa mahitaji muhimu, lingemwezesha mgonjwa kulipia matibabu, lingemwezesha kikongwe kujinunulia japo sukari & majani akajipikia chai kuupa mwili joto nk!
 
Haya wenye akili zenu, sisi tunaliangalia katika hali ya kijamii zaidi ni kufuru kabisa, hizo ni theory za kwenye vitabu tu mkuu. Sasa tukisema kila tajiri azikwe na pesa zake vitu ndo havitapanda? Na serikali itakuwa na kazi ya kuchapa pesa tu mkuu kwani kuchapa pesa hakuna gharama kwa Serikali nyie wataalamu?
 
Kuzika mtu na pesa ni uhujumu uchumi mithili ya kuchoma moto pesa kwa maksudi.
Acha kukariri, infact its the opposite ya uhujumu uchumi, mkataba (pesa) ni wa kwangu, nimeamua kuu-forfeit (kuuchana), which means ni faida kwa serikali, kwani nime forfeit ile haki yangu ya kudai huduma/bidhaa kwenye soko ambayo hupunguza inflation. Jiulize tu, kwanini serikali inakusanya kodi? Kwanini wasiwe tu wanachapisha pesa na kulipa mishahara, kujenga mabarabara, mashule na mahospitali? Kwanini wanahangaika kukaba watu kodi wakati wanaweza wakachapisha tu hizo pesa??! Jiulize usiwe kama msukule asietumia akili, jiulize hata kidogo tu..!! (Nijibu kwa ku-counter hoja yangu na sio kukariri na mihemko, kinyume cha hapo sitakujibu tena)
 
Gharama ya kuchapa noti moja sh.10,000/= probably haizidi sh.1/= pengine, ila yule mtu anaondoa 10,000/= nzima kwenye mzunguko, hiyo inapunguza mzigo kwenye huduma/bidhaa sokoni, hivyo matajiri wote wakizikwa na pesa zao lazima demand ya bidhaa/ huduma kwenye soko itapungua na bei itashuka
 
Sikupenda kuchangia lakini comment yako imenivuta. Wale 'madon uchwara' walipokuwa wakielekea kwenye mazishi na magari yao ya personalized numbers na kifahari walisimamishwa sana njiani na vijana waliochoka wakiwaomba pesa na sidhani kama waliwapatia.
Hapa tunajifunza kuwa kuna gap kubwa sana kati ya wenye pesa na wasio kuwa nazo na ni ujinga wa hali ya juu kumnyima pesa anayehihitaji labda kwa mlo then ukaenda kuitupa tu isitumiwe na yeyote ...i.e. kuiondoa kwenye mzunguko wa benki kuu! Unajiuliza wao wanazipata wapi nje ya mzunguko huu huu ...ujinga wa Waafrika!
 

Mkuu ingawa umesoma sheria lakini bado umjinga kwenye ufahamu wa mambo mengine, kumbuka Pesa ni alama ya Taifa kama Ngao, Bendera na Wimbo wa Taifa.

Sasa je tujiulize,

1.Mtu unaweza kununua bendera kwa pesa yako je unaweza kuipeperusha kwenye gari lako binafsi kama siyo kiongozi mwenye hadhi ya kupeperusha bendera au unaweza kuichana?
2. Je unaweza kuimba wimbo wa Taifa bar, harusini au sokoni ? Serikali si ilitufundisha tukiwa shule na sauti ni zetu lakini kwanini hatuimbi hovyo.
Kuna vitu tuna haki ya kumiliki lakini Serikali ndiye mwangalizi wa mwisho.
 
Hivi hizo ni fedha? Kama ni ndiyo? Anazikwa nazoo? Kama ni ndiyo serikali inaruhusu kupoteza fedha au alimradi ni zangu naruhusiwa kuzichana , kuzichoma au kuzipoteza kwa namna yeyote? Naomba wajuvi mnijibu!
Elewa, pesa ni karatasi tu, it is worthless bila kile kitu inachokiwakilisha, lile karatasi ni mkataba baina yako na serikali, kwamba ukiwa na lile karatasi unakuwa guaranteed kupata bidhaa / huduma sawia na kiwango cha karatasi na thamani yake ulizonazo. Kwahiyo kama ameamua kuzikwa na mikataba yake aliyoingia na serikali(pesa) hii inamaana ameipa serikali unafuu kiasi kwamba inaweza kuchapisha noti zingine bila kusababisha inflation. Ni kama mtu alipie kodi nyumba mwaka mzima halafu aamue kutoishi, na kumpa ruhusa mwenye nyumba kuipangisha upya nyumba hiyo bila kumrudishia kodi yake. Hivyo ni kama amezikwa na makaratasi ya sh.100 tu which is nothing. Hivi nyie watu mtu mmeenda shule hata kidogo kweli?!
 
Basi turudi tu kwenye butter trade haahaaa
 
Okay poa. (Ila sijasoma sheria)
 
Huyo mtoto wa nne sio huyo jamaa anajiita King Lawrence sijui nani mkuu!?
king lawrence mbona mkubwa? Pale hawakusema umri wa mtoto ila itakuwa huyo mtoto ni mdogo baada ya zari kuolewa kwa mdogo wake mond wenda ivan kuna sehemu alipita maana hata huyu mtoto pale hakuoneshwa alitoa maelezo kuwa marehemu ameacha watoto 4 na huyo wa nne hawamjui
 
Ooh ok. Nashukuru kwa kunielewesha mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…