Wakili Mwandamizi, Alute Mugwai Lissu, kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, anatarajiwa kuzikwa Jumanne, Novemba 10, 2026, Kijiji cha Mahambe, mkoani Singida, baada ya mwili wake kuagwa jijini Arusha.
Alute alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 1, 2026, katika Hospitali ya Selian jijini Arusha.
Akizungumza leo Jumanne, Novemba 3, 2026, msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni mdogo wa marehemu, Dk Vincent Lissu, amesema ibada ya kumuaga itafanyika Jumatatu, Novemba 9, katika Kanisa Katoliki la St Theresa, jijini Arusha, kuanzia saa 7 mchana.
Amesema baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu utasafirishwa siku hiyohiyo kwenda Singida kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Jumanne, Novemba 10.
Dk Vincent amesema kabla ya ibada hiyo, kutakuwa na ibada fupi nyumbani kwa marehemu Jumapili, Novemba 8, kuanzia jioni.