Mazishi ya mwanamuziki General Defao yafanyika DR Congo

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
View attachment 2060008View attachment 2060009View attachment 2060010View attachment 2060011View attachment 2060012
View attachment 2060013
Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo François Lulendo Matumona, maarufu General Defao amezikwa leo Jumamosi katika mazishi ya kitaifa.

Defao alifariki mwezi Disemba mwaka jana katika hospitali Laquintinie huko Douala, Cameroon, ambako alikuwa akipokea matibabu.

Jamaa zake wanasema mwanamuziki huyu hakuacha mtoto lakini ameacha nyuma vito vya dhahabu vya thamani ya dola 260 za Kimarekani (mikufu ya dhahabu aliyokuwakuwa akivalia shingoni).

Wanamuziki wenzake na mashabiki wake waliohudhuri mazishi hayo wakiwa wamevalia mavazi za bei ghali wakidai pia Defao alikuwa mmoja wao, na wanafanya maonesho ya mavazi.
Pia alicheza kwa muda mfupi na Fogo Stars na Somo West kabla ya kujiunga na Grand Zaiko Wawa na baadaye kuwa sehemu muhimu ya Choc Stars.

Ilikuwa katika kipindi hiki ambapo Defao aliboresha ustadi wake wa uimbaji na uandishi wa nyimbo, akifanya kazi na watu wa nyumbani wakati huo kama Ben Nyamabo na Bozi Boziana.

Defao, katika azma yake ya kujitengenezea nafasi nzuri, aliachana na Choc Stars kuelekea mwisho wa 1990 na kuunda Big Stars na Djo Poster.

Hata hivyo, mambo hayakwenda kulingana na mipango yake na alilazimika kutafuta wanamuziki wapya baada ya Djo kuondoka.

Katikati ya miaka ya 90, Defao alikuwa tayari akitishia kufuta majina maarufu kama Koffi Olomide na Bozi Boziana kutoka ulingo wa muziki lakini hakufaulu kupata umaarufu nje ya nchi.

Zaidi soma
 
RIP Legendary. Nakumbuka miaka ya 1990s alikuja TZ halafu baada ya show host wakamtelekeza.bakahifadhiwa na jimama flani Mtoni Kwa Aziz Ally. Nahisi hapo ndipo alipozoa virusi. Ila ka-survive kitambo
Amemaliza mwendo
 
260 USD ni vito?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…