Mazishi ya Mwanamuziki Radio

Mazishi ya Mwanamuziki Radio

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
301,221
Reaction score
1,172,274
Msanii Radio wa nchini Uganda ambaye alifariki Februari 1, amezikwa leo kijijini kwao Nakawuka nchini Uganda, na kuhdhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo na wasanii wa nchi jirani.

Hapo jana Ijumaa ya Februari 2, wananchi wa Uganda na mashabiki wa muziki walipata fursa ya kufanya ibada ya mwisho ya kumuombea marehemu kanisani, na kisha baadaye mwili wake kupelekwa kwenye uwanja wa michezo wa Airstip, ambapo walikesha nao huku kukipigwa show ya nguvu kutoka kwa wasanii mbali mbali wa nchini Uganda.

IMG_20180203_175716.jpg
IMG_20180203_175724.jpg
IMG_20180203_175730.jpg
IMG_20180203_175736.jpg



Kabla ya mazishi hayo kuliibuka mvutano mkubwa wa nguo ya kuvalishwa marehemu, huku Lilian Mbabazi ambaye ni mama wa watoto wake wawili ambaye mwenyewe alimtambulisha kama mke wake akitaka marehemu azikwe na suti aliyovaa kwenye tamasha la 'Nakudata' ambayo ndio ngoma iliyompa umaarufu na kumfanya atoboe kwenye game, na mwanamke wake mzungu ambaye amezaa naye mtoto mmoja akisema marehemu alitaka akifa azikwe na nguo za jeshi kwani alipenda kuitwa mwanajeshi, na hatimaye akavalishwa gwanda za jeshi.

Asubuhi ya leo mwili huo ulipelekwa kijijni kwao Nakawuka na kuwekwa kwenye makazi yake ya milele, ambapo kwenye tukio hilo watu walionekana kuwa wengi na baadhi wakizimia.

Miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni msanii na mbunge Jaguar wa Kenya, wasanii mbali mbali wa Uganda na viongozi wa serikali.
 
apumzike kwa imani sisi wakristo tunaamini ni mpango wa Mungu, masikini sauti yake anaimba kama kashushwa kutoka mbinguni.
 
Nimeona wasanii wa Kenya walioenda huko, vipi kuna wasanii wa bongo walioenda?
 
hatuna namna zaidi ya kukubali lililotokea, ila jamaa alikuwa vizuri sana
 
Daah niliona clip ya yulebauns alivyomdunda chini duuh jamaalilikuwa linataka sifa zakijinga mbakalimesababisha kifo.
Mabaunsa mengi yanatumiaga nguvu kuliko akili.

R. I. P msanii.
 
Duh!!! Sijui chanzo nini hadi kumuua Kama watu wa mieleka!!!!

Tangulia tuko nyuma yako
 
Back
Top Bottom