Mazishi ya Ustadh Ilunga katika picha

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,147


Maalim Seif akishiriki katika mazishi ya Sheikh wa Ilunga Shekh.Hassan Kapungu yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam. akijumuika na Wanancjiji Dar-es-Salaam.




Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam.


Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam. (Picha na Salmin Said OMKR)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewaongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa wa Mwanza na mwanaharakati wa dini ya Kiislamu marehemu sheikh Ilunga Hassan Kapungu.

Sheikh Ilunga amefariki dunia mjini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.

Katika uhai wake sheikh Ilunga Kapungu alikuwa mwanaharakati ambaye mara nyingi alikuwa akiendesha mihadhara ya wazi ya dini ya Kiislamu, ambapo mwishoni mwa mwaka 2013 alikamatwa kwa tuhuma za uchochezi mkoani Tabora na baadaye kuachiwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa za kimtandao, kabla ya kukamatwa kwake na kuachiwa huru Disemba mwaka 2013, marehemu sheikh Ilunga alikwenda nchini India kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo pamoja na sukari.

Akizungumza katika mazishi hayo sheikh Basaleh wa Dar es Salaam, amesema marehemu sheikh Ilunga alikuwa mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa kuigwa katika harakati za dini ya Kiislamu.

Mazishi yake yameweka historia baada ya maelfu ya waislamu kujitokeza kushiriki kwao, hali iliyopelekea mchanga wa kaburi lake kufukiwa kwa mikono badala ya kutumia mapauro na majembe kama ilivyozoeleka.

Masheikh kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo sheikh Kishki.





 
naam maalim naye alikuwepo ... hata prof lipumba nae alikuwepo
 
Zongwe.
Ccm wanaona aibu kwa kumuua kwa hio hawawezi kuja..
 
Kikwete anaona bora aende msiba wa Kanumba kuliko wa Sheikh!Innalillah Wain illah Rajiun


Lakini JK si muisilam mwenzenu??? Imekuaje tena, au mfumo christo...
 
Watu wachochezi sana sasa Kisukari na CCM wapi na wapi?
 
Kwani msiba una Dini?au ndiyo ccm wamekufundisha hivyo

Sasa mbona unalalamika kwa JK kutokuja... au ni msiba wa ki siasa...
Okay by the way "who is sheikh ilunga" ili JK impase aje kwenye huo msiba!!!
 
mkuu wa kaya anamisiba yake ya kuhudhuria

Sheikh ilunga ni nani ili JK aende kwenye masiba???
He is dead, nothing can bring him back.
Zikeni huyu sheikh. ...
 
Kikwete anaona bora aende msiba wa Kanumba kuliko wa Sheikh!Innalillah Wain illah Rajiun

Kwa hyo Kanumba na huyo sheikh umewaweka kwenye mizani ukaona sheikh ni mzito kuliko Kanumba? Mungu angekuwa kama mwanadamu cjui dunia hii ingekuwaje
 
Kwa hyo Kanumba na huyo sheikh umewaweka kwenye mizani ukaona sheikh ni mzito kuliko Kanumba? Mungu angekuwa kama mwanadamu cjui dunia hii ingekuwaje

Unalinganisha kiongozi wa dini na msanii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…