maziwa makubwa

Sio kila kitu kinapaswa tukifuate kwa kuwa ni maendeleo...Kutumia computer,simu etc its ok..lakn kuna mambo mengine kama njia za uzazi wa mpango,plastic surgery hebu tumuachieni Mungu jamani na nature yake....

Kwa nini hayo tumuachie Mungu mengine tudhibiti sisi wenyewe?

Kuna nini katika hayo ya kuzidi mengine?


Mtoto akizaliwa mguu umepinda tunamfanyia yote kuhakikisha mguu unakaa sawa lakini kupanga lini upate mtoto iwe kosa? Why?
 

Ebola, ndui, ukimwi, surua, tetekuwanga, mapunye, etc, etc... yoooote hayo ni nature na yanasababishwa na virus au bacteria katika asili yake au impact yake ndani ya mwili wa mwanadamu. Na haya yote yanamadhara directly au indirectly kwenye mwili wa mwadamu. Mfano:

-- tetekuwanga inaweza kuleta makovu au madoa-doa ya kudumu kwenye mwili wa binadamu; sasa je, usitibu madoa hayo kwa sababu yamesababishwa na kitu asilia?

-- matiti makubwa yanaweza kusababishwa na hormonal imbalance inayoweza kutokana na mtu kuugua sana, ambako nako kunaweza kusababishwa na kuwa attacked na virus aina fulani. Sasa je, mtu huyo ayaache matiti yake katika hali hiyo eti sababu tu ni mwonekano wa mwili wake?

-- kuna upofu wa watoto unaosababishwa kwa magonjwa ya zinaa nyakati za ujauzito. Je, kusiwepo uchunguzi wa kuweza kuwawezesha watoto hao kuona (kama inawezekana) kwa sababu tu wamezaliwa hivyo?

-- magonjwa mengi na vilema vingi vinaambatana kutokana na hitilafu katika miili ya wazazi kulikosababishwa na virusi, bakteria, ajali, hitilafu za mionzi, urithi na sababu nyinginezo mbalimbali; matokeo yake ni watoto au uzao ambao huonekana unahitilafu za kurithi, i.e. vilema vya maumbile. Sasa, tuache kuchunguza au kurekebisha hitilafu hizo kwasababu tu watu hao wamezaliwa hivyo??

God gave us the wisdom, skill and power to tame our environment. Enendeni mkajaze dunia na kuitawala. Tusipofanya hivyo tutakuwa tunaenda kinyume na maandiko (kwa waaminio maandiko hayo).
 
Waulize hao madaktari walishauri upunguze hayo maziwa wakuambie jinsi ya kutekeleza hilo zoezi.
 
yako stage gani?,Nido,Mtindi au Papai?
 
Kwa nini hayo tumuachie Mungu mengine tudhibiti sisi wenyewe?

Kuna nini katika hayo ya kuzidi mengine?


Mtoto akizaliwa mguu umepinda tunamfanyia yote kuhakikisha mguu unakaa sawa lakini kupanga lini upate mtoto iwe kosa? Why?
ina maana wewe unajifanya hujui madhara yake? panga watoto lakn chagua njia gani unatumia..hayo maendeleo sana yanaweza kuku-cost?
 
Je una tatizo la kiafya?? Je kuna mtu/watu wanakucheka au kukusema (stigmatization)??, Je unaamini kuwa Mungu yupo na alikuumba??. Dada yangu naomba Dunia isikutese kisa eti umekuwa tofauti na wengine. Ulishawahi kuona vilema na kujilinganisha?? Mshukuru Mungu wewe ni mzuri sana dada yangu. Usidanganyike, ukubwa wa matiti hauna madhara yeyote ya kiafya, ila unaweza kujidanganya kuwa unaumwa mgongo kisa tu ulisikia kuwa wenye matiti makubwa wanaumwa mgongo..Kwa taarifa yako hiyo sio sababu. Usiharibu mwili wako kwa kuongeza wala kupunguza sehemu yake. Kwa imani ni Mungu TU alimpunguza Adam ubavu wake akamuumba Eva. Nyama unayotaka kuipunguza ktkt mwili wako unaipeleka wapi??????? Wewe ni mzuri na utapendwa ulivyo.
 
Ni kweli kwamba kama una uwezo wa ku-avoid surgery basi na usifanye. Lakini inategemea na mleta mada hayo maziwa anayoyaongelea yapo katika hali gani. Inawezekana kabisa yakawa na ukubwa ambao yeye unamkera lakini ukawa hauna madhara kwake. Lakini kuna ukubwa ambao huwa unapitiliza kiasi kwamba unaleta matatizo makubwa ya mgongo. Kuna mama mmoja ambaye sasa ni mtu mzima tu, alilazimika kufanyiwa upasuaji kupunguza ya kwake coz yalikuwa extreme case.
 
Hao hao wanaopinga huyo dada kupunguza maziwa...ndio hao hao ambao hutumia viagra ili kukidhi haja. Kwanini basi nao wasiache nature ifanye kazi...? Kama jongoo halipandi mtungi, waliache hivyo hivyo doro...kha!

Kama uwezo unaruhusu sepa fasta Brazil ama kwa wataalam wa India ukaweke mambo sawa...
 
kwa hiyo kufanyiwa plastic surgery ndio maendeleo na ku- control nature....???haya maendeleo yatatuua mwaka huu...
Hata kwa mtutu sikubali wacha nibaki nayo makubwa...
huyo haelewagi anachokiongea hujiona eti yeye anajua mambo yakizungu sana na anayaweza ndio ushauri wake siku zote msamehe bure
 
Cost benefit analysis inahusika kwa kila jambo. Nakubaliana na wewe kuhusu plastic surgery. Kama ina health benefits rather than the looks ama cosmetic, then haina maana. Ila kwenye uzazi wa mpango it is not healthy kuzaa watoto 15 jamani. Wakati huu tunahangaika na protocol za population ni muhimu kuwaza population gani inaweza kuwa supported na resources zilizopo (oxygen, chakula, maji, na hata ardhi na teknolojia). Uzazi wa mpango ni lazima, njia za kuchagua ndo tuangalie zilizo salama zaidi.
Sio kila kitu kinapaswa tukifuate kwa kuwa ni maendeleo...Kutumia computer,simu etc its ok..lakn kuna mambo mengine kama njia za uzazi wa mpango,plastic surgery hebu tumuachieni Mungu jamani na nature yake....
 
Jikubali au kama unaweza waone watalaam wa mambo ya uzazi na lishe maana wakati mwingine vyakula tunavyokula vinaweza kuwa kisababishi
 
Sikumaanisha hivo dear...nilikuwa namaanisha tuepuke njia za kisasa za uzazi wa mpango na vidonge kwani vina madhara makubwa kwa wanawake..badala yake tutumie nature/njia za asili.....
tupo pamoja
 
Nimekuelewa mamito. This week nimebahatika kuspend time kikazi na mama mmoja also black. Akashare nami shida yake, njia za kuzuia mimba. Baada ya first baby alitumia physical barier akazaa na mtoto akatoka na coil yake. Ametumia condoms akabeba mimba. Baada ya kuzaa mtoto wa nne wakakubaliana yeye na mumewe kufunga jumla uzazi. Ni kweli walichagua njia salama. Mungu tu atatusaidia surely, we just play our part. Imagine una ndoto za 2 kids unajikuta una 4 na huwezi lalamika manake wenzio hawana hata mmoja. Challenges hazina mwisho.
Sikumaanisha hivo dear...nilikuwa namaanisha tuepuke njia za kisasa za uzazi wa mpango na vidonge kwani vina madhara makubwa kwa wanawake..badala yake tutumie nature/njia za asili.....
tupo pamoja
 
ina maana wewe unajifanya hujui madhara yake? panga watoto lakn chagua njia gani unatumia..hayo maendeleo sana yanaweza kuku-cost?

Sielewi hayo madhara, nieleweshe

Manake nashangaa sana na Watanzania kuchukulia kuwa njia za uzazi wa mpango zina madhara makubwa sana wakati huko kwenye nchi za Kimagharibi watu wanaanza tokea na miaka 14 kumeza, wala hayo matatizo makubwa hayaonekani
 
UMETUMIA HEKIMA KUBWA SANA KUTOA USHAURI WAKO NDUGU YANGU....HONGERA

MWENYE MACHO NA AONE NA KUSOMA SASA:glasses-nerdy:


 
Nyani Ngabu SIJUI KAMA NITKUWA NIMEKOSEA SANA HII NI MFANO MWINGINE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…