WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:
'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'
Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.
Akhsanteni.
SteveD.
Milk ni maziwa ila kuna wengine wanatumia creme ikimaanisha maziwa pia.
Breasts ni matiti. Mfano mwanamke ana matiti halafu hayo matiti yana chuchu ambazo ndio zinatoa maziwa maranyingi wakati amejifungua mtoto.
Tusikie zaidi kutoka kwa wanaJF wengine.
Bel.
WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:
'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'
Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.
Akhsanteni.
SteveD.
WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:
'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'
Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.
Akhsanteni.
SteveD.
Kiswahili ni lugha iliyorithi kwa asilimia kubwa, tabia na miundo ya lugha ya kiarabu. Mara nyingi tunapozungumza kiswahili huwa tunatumiaaina ya misemo ambayo bila ya kukusudia au kwa kukusudia huwa inaficha au kupunguza makali ya kile tunacho kimaanisha, na hii ni katika kuonyesha heshima kwa mzungumzaji na msikilizaji.
Nikirejea kwenye maneno yalio kusudiwa na mtoa mada "Matiti au Maziwa" Kilugha maneno haya yana maana tofauti. Lakini ki Istilahi huwa neno moja utumiwa kuficha ukali wa neno lingine, hapa tunakuwa tumetumia tamathali za usemi zinazofanya neno liwakilishalo kitu kingine (Tashabiha).
Mara nyingi hali hii ya kutumia tashbiha inapelekea wale wasiokuwa mahili au wanagenzi wa lugha ya kiswahili hususan watoto kupata tabu kutambua kilicho kusudiwa, vile vile husaidia kuonyesha uungwana na heshima kama nilivyodokeza hapo juu.
Kuna maneno ukiyatamka kama yalivyo, yaani kuyatamka kavu kavu, uonekana ni matusi na waliokuwepo watakuona ni mtovu wa adamu.
Tunaweza kutamka neno kama lilivyo pale tu tunapokuwa tumekaa watu wa rika moja. Utashangaza na kuonekana wa ajabu maneno kama haya yafuatayo ukayatamka kama yalivyo mbele ya watoto au watu waliokuzidi umri.
Mfano:
Neno kama Ngono au kufanya mapenzi litamke kwa asili yake, Uume au uke. Nakumbuka sisi tulikuwa tunafundishwa kutamka chini kwa babu (dudu) au kwa bibi. Vile vile tunatumia neno " Haja kubwa na ndogo" lakini tunajuwa tuna maanisha nini.
Vilema tunawaita kwa jina la walemavu wa viungo n.k
Kwa uoni wangu nadhani si vibaya mtumiaji akatumia neno maziwa akimaanisha Matiti, hii inategemea na maali alipo. Ila huwezi kutumia neno matiti ukimaanisha maziwa. (My Milk is standing)
Naomba kuwakilisha
XP
Mkuu X-P kiusahihi ni 'naomba kuwasilisha' na si 'naomba kuwakilisha' kama ulivyondika hapo mwisho wa mchango wako...Heshima mbele mkuu..Be blessed
Akhsanteni wote kwa ufafanuzi murua kabisa wa tafsiri na matumizi ya maneno niliyouliza (ulizia??).
X-P, je matumizi ya neno "nyonyo" au "manyonyo" yaweza kusemeka ni moja ya tashbiha (-euphemistics- kwa jinsi nilivyoelewa tafsiri ya tashabiha/tashbiha kwa maelezo yako juu, sina uhakika kama neno tamathali nalo lina maanisha 'uephemism') za neno matiti au ni mojawapo ya nomino wakilishi tu?