Maziwa ya karanga

Maziwa ya karanga

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Habari Tanzania !

Sasa ile vita ya mfugaji na mkulima mwisho kabisa. Sitegemei kuona tena vita hii hapa Tanzania.

Mahitaji

a) Karanga mbichi kikombe 1 na 1/2.
b) Sufuria na chujio kubwa
c) Jiko la mkaa, kuni, umeme au gesi
d) Brenda
e) Maji lita 2
f) Jagi au chupa kwa kuhifadhia maziwa
g) Kitambaa safi cheupe

Utaratibu

a) Osha karanga zako kwa maji safi.
b) Zichemshe kidogo, ukishamaliza.
c) Ziweke katika brenda na changanya na maji lita 1.
d) Washa brenda yako na fanya mchanganyo.
e) Anza kuchuja maziwa yako ya karanga kwa kitambaa safi ukimimina kwa jagi au chupa.
f) Ukimaliza zoezi la juu, chemsha tena maziwa yako kidogo.
g) Maziwa yapo tayari kwa matumizi

Karibu.
 
Ni Kama pesa au nywele, zinabadilika majina kwa mahali na matumizi, ie mshahara, nauli, sadaka, karo, ada, Kodi, ushuru, tozo, ujira etc. Mavudhing, mustache, ndevu, garden love, mzuzu etc
Sawa mkuu buji buji vipi Matema beach hawajambo?
 
Mkuu hii naona kama ni tui au uniambie juice ya karanga nitakubaliana na wewe au mtalaamu Lenie unasemaje!
Kwakwel hapo hata mimi nimeachwa njia panda, ila labda atuambie matumizi ya hayo maziwa ya karanga yanaweza kua na msaada.

Pia ratio ya kikombe kimoja kwa maji lita 1 naona kama karanga zitapelea sana au kikombe kimoja cha ujazo gani.
 
Back
Top Bottom