Mtoto kwa kawaida anatakiwa kunyonya kwa miezi sita ukishindwa basi angalau miezi minne hadi mitano. Maziwa ya mama ndo chakula pekee yaliyojitosheleza kwa virutubisho.
Maziwa yako yanmsaidia kujenga kinga ya mwili lakini pia kujenga akili yaani iq ya mtoto. Zipo faida nyingi sana ila hizi ndo za mhimu ambazo maziwa ya ng'ombe au formular hayana. Maziwa ya mama yakikamuliwa yanaweza kukaa kwa masaa nane bila kuharibika na bila kuweka kwenye friji. Ninavyofahamu kama mfanyakazi unatakiwa kufanya masaa sita, kwa hiyo ukimkamulia 200mls kila siku zinamtosha sana kunywa mpaka utakapo rudi baada ya masaa 6. Kwa kawaida mtoto anatakiwa kunyonya angalau kila baada ya masaa matatu, mfano kama unatakiwa kazini saa 2 asub ukmnyonyesha saa 1, yale uliyokamua anywe saa tatu/nne baada ya masaa 3 yanayofuta utakuwa umesharudi.
Uzuri siku hizi kama huwezi kukamua vipo vifaa vya kukamulia siku hizi vipo unaweza kamua mpaka 500mls, sioni haja kumwazishia maziwa ya ng'ombe au formular.
Ushuhuda:
mimi ninamtoto wangu wa mwaka 1 na miezi 3, alinyonya mpaka miezi 5 bila kupewa kitu chochote cha ziada.
Alikuwa akiongezeka uzito kila mwenzi na kila mwenzi aliongezeka kwa 0.8kg hadi 1.8kg, hadi sasa anatembea. Baada ya miezi mitano alainza kupewa uji na maziwa ya ng'ombe na baadaye kila chakula anakula.
Hivyo acha kumexpose mtoto na artificial foods ataanza kukusumbua na fever zisizo za maana. Kwa mara ya kwanza aliiugua baada ya kuanzishiwa vyakula vinginne.
Note. Vyombo vya kukamulia hakikisha unaosha mwenyewe na mtoto akinywea chombo hicho asirudie tena kukitumia hicho kinaenda moja kwa moja kwa maandalizi ya kuoshwa kwa matumizi ya siku nyingine. Acheni tabia ya kuwaachia mahouse girls wanawafanyia kila kitu. Mimi kama Baba niliplay part kwa khakikisha kile kinashauriwa na madaktari kinafuatwa. Ingawa mimi mwenyewe na mama yake wote ni madaktari, bibi zake niligombana nao sana wakisema hataongezeka uzito lakini waliona tofauti. Binafsi namlea mwanangu kama kitabu kinavyoeleza na nimeona faida zake. Understanding capacity yake ni nzuri alianza kuelewa akiwa na miezi minne. Nikimwambia piga makofi aliweza. Na hili ndo lilikuwa neno la mwanzo klielewa. Tunzeni watoto wenu msiwaachie house girls.
Kama kuna sehemu sijaeleweka basi naomba maswali coz natumia simu.
Nawatakia siku njema kwa jina la Bwana.