Maziwa ya mama yanapokamuliwa hukaa muda gani mpaka kuharibika?

PistolGang

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
392
Reaction score
44
Habarini ndugu, rafiki na jamaa zangu wa humu?

Nina swali la kupewa ufumbuzi kimsaada zaidi. Hii itawahusu wazazi wote na wataalamu wa maswala la watoto wachanga.

Stori inaanza hivi; Ni takribani miezi miwili na siku kadhaa tangu mke wangu ajifungue mwenetu kipenzi (Alhamdulillah) amejaliwa afya njema na kilo zinaenda vizuri.

Ila swala ni kwamba mimi na mke wangu sote ni wafanyakazi, hivyo mke wangu anakaribia kurudi kazini baada ya kumaliza zile siku za kupumzika.

Hofu kwa mwenetu ambae haipiti nusu saa bila kunyonya pale anapokua macho (hajalala) na mama yake wiki ijayo anaanza kwenda kazini (Atakua anaenda saa2 asbh na kurudi saa6 na nusu mchana) na kuna umbali kidogo mahali tunapoishi na kazini kwake, ni takribani masaa 4 na nusu atakua mbali na mtoto kwa siku zote za kazi ( I hope ndivyo ilivyo kwa wazazi wote ) kwa muda huo mtoto atakua yupo na dada wa kazi nyumbani.

Hivyo, tatizo la njaa litakua kubwa sana na tumeambiwa/inafahamika mtoto atakiwi kula chochote mpaka afikishe miezi sita.

Juzi katika pita pita zangu kwenye BabyShop/KidsCorner nimeona kijidude cha kukamulia maziwa ya mama na contena lake la kuhifadhia kwaajili ya kumnyonyeshea mtoto pale mama atapokua mbali.

Swali linakuja hapa; Je, maziwa ya mama yanapokamuliwa na kutuzwa kwa muda ni salama kwa mtoto? Kama ni salama yakae kwa muda gani kabla ya kuharibika? kama si salama, ni njia ipi ya kum_feed mtoto kwa situation hiyo (hapo juu)?

Nahitaji Msaada:
 
Yakikamuliwa yanaweza kaa masaa matatu bila kuharibika yakiwa hayajawekwa kwenye friji, ukiyaweka kwenye friji baridi ya kawaida ni masaa sita , ukiyagandisha kwenye friza bila kuyatoa yanakaa miaka miwili. Lakini yahifadhiwe vizuri kwenye vyombo safi na salama na yafunikwe, ukitaka kumpa unapasha kiasi kanachotakiwa kwa chombo cha maji ya vuguvugu, yakibaki yamwagwe.
 
At room temperature, upto eight hours.

But frozen breastmilk can stay for months.

Ila umeme wetu wa Tanesco sasa. manake thawed milk should not be refreezed.
 

Shukrani mkuu
 
Masaa nane.. Yakiganda yanaweza kukaa zaidi lakini kuwa makini sana na utunzaji pamoja na usafi wa maziwa hayo, mabinti wengi wa kazi hawazingatii usafi na hii inaweza sababisha magonjwa kwa mtoto wako ambaye ana kinga ndogo
 
Jaribu kukamua ya mkeo ufanyie experment tafadhali.
 
anakwenda kazini masaa manne na nusu, hapo kwenda na kurudi traffic njiani na umbali wa kazi, inaweza kufika masaa zaidi ya masaa nne na nusu,
ushauri wangu kama wewe upo vizuri kikazi bora yeye asifanye kazi mpaka baada ya mwaka ikiwezekana, kama haiwezekani miezi sita akae ili amuimarishe mtoto kiafya pamoja na yeye. ila kama hali ya maisha haikuruhusini mkeo kukaa nyumbani, basi itabidi uweke hidden camera kwa kumuacha mtoto wako mchanga na dada wa kazi, na umwambie kuwa kuna camera inarikodi hapa kila kitu kwa hivyo ujitahidi kukaa na mtoto vizurii.
kuhusu kukamua maziwa inabidi utafute vichupa vidogo vidogo kama sita, usitie yote katika chupa moja. Kila chupa tia 2 to 4 ounces. inategemea mtoto anakunywa ounces ngapi kwa mara moja. kwa sababu akimaliza kunyonya yakibaki ni kumwaga tuu sio kuweka baadae.
unahitajika usafi wa haliya juu wakati wa kukamua haya maziwa mpaka kupewa mtoto.
na ukitoa kwenye friji usichemshe, ni kuchemsha maji ikisha ndio kuitia ile chupa ya maziwa.
kama hujafahamu google

''Storing and Preparing Expressed Breast Milk''

Mwisho namuomba Mungu amhifadhi mtoto wako na amkuze katika makuzo mema. AMIYN
 
maziwa ya mama hayana expire date ww ila huleta maumivu pale mama yanapojaa na kifuani na kutaka kutoka kwa kunyonya kwenda kwa mttt
 

Shukrani za dhati zikufikie mpendwa. Nimependezwa sana na maelezo yako. Ubarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…