Maziwa ya Punda na farasi yananywewa na watu wa mataifa mengi wakiwemo wa Misri wa kale... Inasemekana Cleopatra alikuwa akikoga maziwa ya punda ili aendeleee kuwa na ngozi nzuri na kutunza mwonekano wake... Alihitaji punda 700 ili kuweza kupata maziwa yalio toshereza beseni lake la kuogea.
Maziwa ya punda yamekusanya mafuta kiwango kidogo, hivyo ubora wake unakaribiana na maziwa ya binadamu. Maziwa ya punda yanaendelea hadi leo kutumika kwenye maswala ya urembo. Kuna sabuni na moisturizers zilizotengenezwa kwa maziwa ya punda.
Vile vile yanasaidia kuondoa sumu mwilini, Homa, machovu, kuondoa madoa ya kwenye macho, kuongeza nguvu kwenye meno, kuondoa mikunjo usoni, uvimbe kwenye tezi, asthma na matatizo ya kizazi. Pia usaidia ini kupambana na sumu, utokaji wa damu puani na urahisisha kupona kwa haraka kwa vidonda
XPaster Umesema kweli Swadakta na mimi naongeza Faida ya
`Maziwa ya ngamia huongeza kinga kwa wenye VVU`
Maziwa ya ngamia yametajwa kuwa huongezea kinga kwa wagonjwa wa Ukimwi na kutibu wagonjwa wa kisukari, vidonda vya tumbo, tiba ya fizi zenye kutoa damu na wenye upungufu wa vitamini C.
Kutokana na tabia ya ngamia kula aina mbali mbali za majani ya miti na mbegu, imeelezwa kuwa hufanya maziwa ya ngamia kuwa na vitamini C na kupelekea kuwa tiba kwa binadamu.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa shamba la ngamia kwenye mwambao wa Pwani wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, Bw. Salim Mselem.
Bw. Mselem aliiomba serikali kuhimiza wananchi kufuga ngamia.
Alisema ngamia mmoja hutoa kati ya lita tano na 20 za maziwa kwa siku, jambo ambalo alisema ni la mafaniko makubwa kwa wafugaji hapa nchini endapo wataamua kufuga ngamia.
Akielezea historia ya mradi wa ngamia eneo la mwambao wa Pwani, alibainisha kuwa uongozi wa shamba hilo uliingiza ngamia wanane kutoka nchini Kenya mwaka 1997, ambao wamezaliana na kufikia 70 mwaka 2008.
Mkurugenzi huyo alisema shamba hilo lina ngamia 60 wanaokamuliwa na hutoa kati ya lita 600 na 700 kwa siku ambazo husambazwa kwenye hoteli za kitalii jijini Dar es Salaam.
Alisema ngamia wanaweza kufugwa kwa kuchanganywa na mifugo mingine kwani hawana wivu katika kula majani kama walivyo ng�ombe au mbuzi.
Aidha Bw. Mselem, alisema ngamia ni rafiki wa mazingira kwani hula majani ya miti bila kukwanyua au kubandua na kuiharibu kama walivyo wanyama wengine.
Hata hivyo, alisema miguu yake haina kwato kama wanyama wengine, hivyo hawezi kumomonyoa ardhi kama ng`ombe, mbuzi na punda.
``Faida za ngamia ni nyingi kwani nyama yake ni chakula bora kwa binadamu na ngozi yake kutumiwa katika kutengeneza bidhaa za ngozi,`` alibainisha Bw. Mselem.
Alitaja faida nyingine kuwa ni pamoja na kutumiwa kama wanyama kazi katika kilimo cha jembe la kukokota, kubeba mizigo pamoja na binadamu na kukokota mikokoteni.
http://216.69.164.44/ipp/nipashe/2008/03/08/109920.html