Mazoea chanzo cha vifo

Mazoea chanzo cha vifo

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Ajali ya jana imesababishwa na mazoea, vifo vya jana vimetokana na mazoea. Ule Uwanja hauna Taa za pembeni. Hauna Aproach Tower

Uwanja hauna Zima Moto

Rubani pale anatua kutokana na uzoefu wake, yawezekana huyu Rubani alikuwa mzoefu wa kutua katika hiyo hali, ila jana haikuwa siku yake.

Ajali imetokea Saa 2.30, ila serikali imefika eneo la tukio saa 3 na madakika, hii yote ni kutokana na uzembe au walihisi ni drills za siku zote.

Mazoea yanaumiza watu wasio na hatia. Serikali haina vyombo vya uokozi

Serikali haina vyombo vya kuzamia kutoa watu hadi wazamiaji nao wakafia humo ndani ya ndege

Mazoea
Mazoea
 
Na hata mawasiliano nahisi pia hamna maana kama waongoza ndege walikuwa wanawasiliana na rubani alafu dakika mbili au tatu kabla ya kutua mawasiliano yamekata lazima wangeshtuka na kutoa taarifa na kuifuatilia.
 
Kitu kinaniuma sana tumewekeza kwenye siasa sana mahela kibao kwenye siasa, kusifia hovyo, uongo uongo , ubinafsi wizi yaaani hatuna mwelekeo.

Ni yale yale ya kila siku, zima moto limechelewa au limewahi lakini halina maji, Vita ukraine ndio inapandisha bei ya vyakula, tunarekebisha mitambo ndio maana umeme unasumbua, tumepewa mkopo sijui na nani nani, tumewasiliana na rubani, iombeeni bara bara isilete ajali.

Kama Taifa tuna shida kubwa.
 
Back
Top Bottom