"Mazoea" yako hujenga mwamba mgumu moyoni mwako

"Mazoea" yako hujenga mwamba mgumu moyoni mwako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
"MAZOEA" YAKO HUJENGA MWAMBA MGUMU KATIKA MOYO WAKO

Anaandika Robert HERIEL

Yule Shahidi

Ingawaje maisha yanatufundisha tusiwe na MAZOEA kila siku, hayataki tuzoee lakini Sisi ndio tunalazimisha kuwa na MAZOEA, ndio maana leo ni tofauti na Jana, na kesho itakuwa mbali na siku ya leo. Wala hatujui nini kitajiri kesho, na hata hiki cha leo hatukujua Kama kingekuwa hivi. Ndivyo nilisema, maisha ni mzunguko wa mambo mapya yaliyozaliwa na mambo ya zamani, tena kesho ilitoka katika siku ya leo. Ijapokuwa kila siku yajitegemea na inajitosheleza, lakini kusudi ni moja katika muunganiko wa maisha.

Mazoea ni kufanya Jambo moja, lilelile kila mara, huitwa mazoea, desturi, kawaida na Amali. Kufanya kitu kila mara huzaa mazoea, kisha kikishakomaa na kinatengeneza TABIA, Tena tabia hukua na kukomaa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja mpaka kizazi kingine, wakati mmoja mpaka wakati mwingine, Zama moja mpaka nyingine, na hapo huzaliwa mwamba mgumu uitwao ASILI.

Hii ni kusema, Mazoea hujenga tabia, kisha tabia huleta ASILI. Hivyo ndivyo ilivyo. Hata hivyo hakuna kinachodumu, hata asili huzeeka na kupotea baada ya kukamilisha mzunguko wake.

Basi Siku zaenda wala hazirudu tena, tena zaja na kutuchukua na kutupeleka tusikokujua, tena hatutajua Kama tulikuwepo Kama sasa tusivyojua kuwa tulikuwapo.

Mazoea huumiza pale yanapotaka kuondolewa,tena. Tena yapo maumivu makali katika kuitoa tabia, mwisho ni kifo katika kuondoa asili ya kiumbe.

Mazoea ni mahusiano baina ya mtu mwenyewe, au mtu na mtu mwingine, au mtu na vitu, au mtu na Mazingira yanayomzunguka.

Yapo mazoea ya Mke na mume
Mazoea ya Mzazi na mtoto
Mazoea ya Mtu na Gari au Nyumba au vitu vyake
Mazoea ya Mtu na mahali anapoishi

Kutenganisha Mtu mwenye mazoea ni Jambo gumu linaloumiza Sana.

Hata hivyo Maumivu yatatokana na umri na ukomavu wa mazoea yenyewe.

Kadiri watu wanavyozoeana ndivyo ugumu wa kuwatenganisha unavyozidi kuimarika.

Ikiwa ilichukua siku kuzoea kitu basi itachukua Siku kukitenganisha na mtu huyo kukisahahu.
Ikiwa ilichukua Mwaka au miaka kuzoea kitu ndivyo itakavyo chukua mwaka au miaka kukitenganisha kitu na mtu huyo kukisahau.

Mazoea huishi moyoni na akilini.
Hujenga hisia za upendeleo na Kumbukumbu zilizojichimbia kulingana na urefu wa mzizi wa mazoea yenyewe.

Kumhamisha mtu mahali alipopazoea sio kwamba hataki au hapendi Bali kitakachomfanya apinge ni mazoea.

Sio kwamba wana ndoa au wapenzi hawataki kuachana, bali mazoea ndio huwaletea mushkeli.

Kimsingi, linapokuja suala la mahusiano ya ndoa, Taikon huwaga nashauri kuwa usiruhusu mwenza wako akawa na mazoea na watu wengine kiasi cha kupitiliza.

Pia ni ngumu kumchukua mke/mume WA mtu na kumfanya mwenza wako ikiwa alishazoeana Mume/mke wake. Hapo utawatenganisha kimwili tuu lakini mioyo Yao itakuwa pamoja, sio ajabu wakawa wanakutana bila ya wewe kujua.

Kizazi cha sasa kuna mambo madogo ambayo ni makubwa katika matokeo ambayo kinayapuuzia ndio maana kinalialia.

Hata mtu akifa, watu watalia Kwa sababu sio kwamba aliyekufa ni ndugu Yao au mzazi wake Bali kinacholiza mtu siku ya Msiba ni MAZOEA.

Ndio maana akifa mtu usiye na mazoea Naye, ukaribu Naye huwezi kusikia uchungu.
Au hata akifa Mama au Baba ambaye hajakulea wala haukuwa karibu Naye Huwezi kuhisi uchungu mkali ukilinganisha na Wale waliokuwa na mazoea Naye

Hakuna kitu kinauma Kama Kifo cha mtu wa karibu kabisa yaani mtu uliyemzoea.

Mazoea ni mwamba mgumu unaoujenga moyoni mwako, hivyo ni muhimu kujitahidi kutozoea mtu kupita kiasi Kupunguza makali na maumivu ya kutisha siku mtakapoachana.

Kwa maana Kuachana ni HAKIKA, Iwe Kwa Mauti au kufarakana.

Nipumzike sasa!

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Note: Kuachana ni Hakika ,Iwe kwa kufa au

kufarakana. Ahsante sana Taikon wa Fasihi.
 
Umeandika kwel tupu, ndio mana mimi najitahidi kuwa na kiasi cha kuzoeana na watu wangu wa karibu, mana najua kwenye maisha lolote linaweza kutokea.
 
Kuna ukweli mwingi sana hapa. Kuna jamaa yangu mmoja anafanya biashara moja zaidi ya miaka 25 sasa. Haimuinui kiuchumi kwa maana ya kipato kikubwa. Ila hiyo biashara inamfanya apate pesa za kula na kujikimu kwa mambo madogo madofo. Akishauriwa aachane nayo anasema ameizoea, na hawezi kuiacha.
 
Kuna ukweli mwingi sana hapa. Kuna jamaa yangu mmoja anafanya biashara moja zaidi ya miaka 25 sasa. Haimuinui kiuchumi kwa maana ya kipato kikubwa. Ila hiyo biashara inamfanya apate pesa za kula na kujikimu kwa mambo madogo madofo. Akishauriwa aachane nayo anasema ameizoea, na hawezi kuiacha.


Mazoea ni mabaya.

Hata kiongozi akishazoea Madaraka hudhani ni yake
 
Back
Top Bottom