Davis Abely Nziku
Member
- Jun 3, 2022
- 13
- 13
MAZOEA YANA TABU
Mazoea ni nini Mazoea ni kufanya /kuchukulia vitu au watu kikawaida kawaida. Nini maana ya neno kawaida, Kawaida ni kutotoa heshima inayostahiki juu ya kitu /jambo au watu Fulani ndio maana Utasikia watu wanasema mimi sipendi mazoea Ukiona mtu anasema hivo basi jua anaona heshima yake haipati kama inavyopaswa au kama anavyotaka.
Binafsi mimi sidhani kama mazoea ni mabaya kwa maana mazoea yamegawanyika katika makundi mawili mazoea mabaya na mazoea mazuri lakini watu wengi tunajua tu mazoea mabaya. Ndio maana ukisikia mtu anasema sitaki mazoea unajua kabisa amemaanisha nini. Watu wengi hatufanikiwi katika maisha haya kwa sababu yakuchulia na kufanya mambo kimazoea mazoea ndio maana hatufanikiwi. Leo nataka tuangazie Zaidi Madhara ya kufanya vitu kwa Mazoea.
1. Kupungua kwa Ubunifu katika kazi. Kazi yoyote ile ukiichukulia kimazoea mazoea(kikawaida) hata kama unaiweza kiasi Gani basi ubunifu katika hiyoo kazi lazima upungue hata kama ukiwa unafanya kazi yakusomea hata kama ukiwa na Degree 5 kama utafanya kimazoea basi hautaweza kufanya kwa ubunifu wowote ule.
2.Kupoteza Fursa Zenye Faida kubwa. Kama wewe ni mtu wa kuchukulia vitu kikawaida kawaida Nina Imani kubwa kuwa tayari ushapoteza Fursa nyingi Sana ambazo zingeweza kukuongezea kipato katika maisha yako za kukufanya uwe Tajiri.
3.Kupoteza watu WA msingi na sahihi katika maisha yako kama wewe ushawahi kuambiwa na watu acha mazoea na mimi Ni lazima kuwa ushawappteza watu wengi wenye umuhimu katika maisha yako kwa sababu ya kuwachukulia kawaida kawaida.
4. Huchochea Uvivu. Binadamu yoyote yule ambaye akiiona au kuchukulia kazi Fulani ni ya kawaida basi hata ukimpa hiyoo kazi ataifanya kwa mazoea mazoea Tena kwa Uvivu mkubwa mno bila hata ya kujali kama anaweza kuingiza hasara na ukishafanya kazi yoyote ile kwa Uvivu kinachokuja mbele ni kupoteza mda katika kitu kidogo.
Madhara na Hasara za kuchukulia vitu kikawaida kawaida (mazoea) ni makubwa kuliko kawaida Tena ni nyingi Zaid ya hata nilizozitaja hapo juu maana Unaweza pia kupoteza kibarua chako, kumpoteza mpenzi wake au hata watu wengine wakaribu ambao wanafaida kwetu Unaweza kuwapoteza kwa kuchukulia kawaida kawaida.
Watu wengine pia huwa hawaelewi au hawajijui kama wamemchukulia mtu Fulani kikawaida mpaka waambiwe na huyo mtu Baada ya kuona kuwa sasa atavuka mipaka na tunaweza kushushana CV kama Msanii Billnasss alivyoimba katika wimbo wake "Maana kujuana Sana ndio kuharibiana CV" Leo nataka ujue kuwa utajuaje kuwa mtu X ameona kama umemchukulia kikawaida au unaleta mazoea nae.
1. Unaweza kumtania na yeye akaonesha Dalili yakukwazika ila asikwambie au ukaona anabadilisha Mada hivyo ujue kuwa huyo mtu anaona unataka kuleta mazoea
2.Kupunguza ukaribu na wewe kwa Ghafla. Ukiona hivo jua kabisa huyoo mtu anaona unaleta mazoea au kaona kuwa unamchukulia kawaida
3. Ukimkatisha wakati anasema Jambo lake na Baada ya wewe kumaliza kuongea akanuna Ghafla basi ujue hapo sio mda mrefu atakuondoa katika mzunguko wake wa marafiki maana anaona huthamin mchango wake.
Kama tukiwa na Tabia ya kuchukulia vitu kwa umakini Zaidi na kuvipa thamani yake basi hayo ni moja ya faida ambazo utakutana nazo
1. Unaweza kujiongezea wewe mwenyewe kuheshimika Zaid na kuthaminiwa kama utakuwa na tabia ya kuwapa watu heshima wanayostahili basi ni lazima hata Hao watu kukuheshimu na kukupatia thamani wewe pia.
2.Kujiongezea njia nyingine ya kipato Kuna Fursa nyingi Sana mtaani humu na kama mtu ukiwa na jicho la kuangalia kwa umakini na sio kwa ukawaida nirahisi kugundua Fursa mpya katika jamiii zutu kuliko yule ambaye kila kitu anakichukulia kawaida
3. Itakufanya uwe mbunifu Zaidi ya Binadamu wa kawaida. Binadamu yeyote yule ambaye hachukulii vitu kikawaida kawaida nirahisi Sana huyu mtu kuwa mbunifu wa mbinu nyingi za Kujiongezea kipato katika Fursa moja ambayo anaifanya
4. Nirahisi Sana kuzungukwa na watu sahihi katika maisha yako ambao watakujenga na kukukosoa ili uwe bora Zaid katika kazi zako kwa sababu tu hauchukuliii vitu kawaida kawaida.
Tumezungumza juu ya kuchukulia watu kawaida na kufanya vitu kwa mazoea Lakini pia Kuna kitu kinachoitwa Kujichukulia kawaida Hii ni moja ya sababu ambayo inafelisha ndoto za vijana wengi sana. Utasikia mtu anasema "Ahhhh hivi vitu nivya wasomi bwana mimi Darasa la saba B sitaweza kabisa" Tena Unaweza kuona kazi yenyewe hata haihitaji Elimu ila mtu yeye mwenyewe ashajifelisha na kuiona kama yeye ni mtu wa kawaida.
Nataka ndugu yangu ujue kuwa katika Dunia hii Hakuna mtu wa kawaida wala kitu cha kawaida kawaida Ukiona tu umeanza Kujichukulia kawaida hebu jipige pige na ujikumbushe kuwa wewe sio wa kawaida hata kama watu wakikwabia wewe ni wa kawaida ila mimi DNA nakuambia wewe sio mtu wa kawaida.
Moja ya Hasara ya Kujichukulia kawaida ni kufeli hata kabla ya kufeli kwenyewe Hivo ndugu yangu nakuomba usijichukulie kawaida kawaida na jambo la pili ni kutuaibisha sisi ambao hatukuoni wa kawaida embu assume watu wanakuamini kuwa wewe suala Fulani unaliweza halafu wewe unaona huwezi unadhani Nan hapo atapata aibu ni sisi pamoja na wewe kwahiyo basi naomba usijichukulie kawaida hata Mara moja ili kuweza kufikia ndoto Zetu na matamanio yetu.
Mwisho Ewe ndugu yangu nakuomba mimi kama DNA Unaweza kufanikiwa katika kila jambo unalolifanya na kutamani kulifanya endapo tu utaamua kutokuwa na Tabia ya kufanya vitu kwa mazoea na kuchukulia vitu kwa ukawaida na kawaida na pia usije jaribu kuwachukulia watu kikawaida kawaida na pia usiwe na mazoea yakuzidi na watu maaana Maana MAZOEA YANA TABU.
Mimi ni Davis Abely Nziku
Contact :0755386540
0628488781
Mkazi wa Kigamboni Mjimwema

Upvote
1