kivindo boy
New Member
- Feb 23, 2019
- 3
- 2
MAZOEA YANAVYOONGEZA MIGOGORO YA ARDHI TANZANIA
Ni siku nyengine tena napata wasaa wa kutembelea ndani ya viunga vya mahakama ya Ardhi ndani ya mkoa wa Morogoro kikubwa kinachonileta hapa ni kuja kushuhudia shughuli za kila siku na pia kuja kumtembelea rafiki yangu ambaye ni karani hapa. Nakutana na watu wengi mno Alhamisi ya leo na kila nikilinganisha na Alhamisi iliyo pita, alhamisi hii imekuwa na watu wengi mnoo ikiashiria kesi zitakazo sikilizwa leo ni nyingi kama sinyingi basi kesi hizo chache zimebeba watu wengi. Kwa kumbukumbu tu mwaka jana jumla ya Kesi za Ardhi 1780 zilisomwa na kupatiwa ufunguzi, wakati mwaka huu pekee mpaka kufikia mwezi wa saba jumla ya kesi 695 zishasomwa na kupatiwa ufunguzi huku Kesi zaidi ya 1300 zikisubiri kutatuliwa kisheria.
Nakutana na mzee wa zaidi ya miaka tisini ambaye hata kuona kwake kulikuwa ni hafifu sana, mzee huyu aliletwa kama shahid katika kesi iliyo hairishwa siku hiyo na kutajwa tena mpaka ndani ya miezi mitatu ijayo. Mara ya mwisho kufika katika viunga hivi nilikutana na kijana aliyekuja kufungua kesi ya kuzurumiwa Ardhi yake na baba yake mdogo , kijana alikuwa anamajeraha ya kutosha kwa nazaria kuwa kabla ya kufika mahakamani palitokea mapigano Kati ya kijana huyo na baba yake mdogo .
Kubwa zaidi na la kushangaza nakutana na watu wanne walio uziwa eneo moja na mtu mmoja kwa wakati tofauti tofauti. Najaribu kukuonyesha tu jinsi migogoro ya Ardhi inavyo leta matokeo hasi katika maisha yetu ya kila siku.
Nikiwa na pita katika barabara ya Old Daresalaam road nakutana na nyumba nyingi zilizopo kando kando ya barabara hiyo zikiwa zimepigwa alama ya X na maneno ya BOMOA yakiwa yameandikwa katika kuta za nyumba hizo na nikijaribu kudadisi naambiwa tayari wananchi hao washafungua Kesi mahakamani kupinga ubomoaji huo ,Hali halisi hii. Inafanana kabisa na ile ya wananchi wanaoishi kando kando ya barabara ya Morogoro road.
Mara baada ya kufanya maulizo kwa watu tofauti wakiwemo wataalamu wa taaluma mbali mbali kubwa zaidi linagundulika ni mazoea katika maswala mbali mbali katika sekta ya Ardhi huchochea ongezeko la migogogro ya Ardhi hapa nchini Tanzania.
Mazoea katika maswala mbali mbali katika nchi yetu yamekuwa yakirudsha nyuma jitihada tofauti tofauti za kufanya taifa letu lisisogee mbele na kufanya Taifa letu linyate katika kuyafikia maendeleo ya kweli . Karibu tuangalie baadhi ya mazoea yanayo pelekea changamoto ya migogoro ya Ardhi.
Baadhi ya Mambo muhimu ambayo tukiyafwatilia na kuyafanyia Kazi yanaweza kutusaidia tukaepuka kwa nafasi kubwa migogogro ya Ardhi kwa hapa nchini.
Kivindo lukindo
Muheza Tanga

- Wanasiasa na usimamizi wa masuala ya Ardhi. Viongozi wa mtaa au kijiji kuwa wasimamizi wa mauziano ya Ardhi
- Kuuza na kununua kipande cha Ardhi ndio uti wa mgongo wa chanzo cha migogogro ya Ardhi hapa nchini Tanzania. Ndio naomba ukubaliane na mimi, kesi nyingi zilizopo mahakama za Ardhi ni baina ya mnunuaji na muuzaji au muuzaji na wanunuaji. Kumekuwa na mazoea ya jinsi mchakato wa kuuziana Ardhi unavyokuwa, watu wengi huwatumia Viongozi wa kijiji au mitaa kusimamia zoezi la maudhiano bila kushirikisha wataalamu wengine kutoka taasisi nyengine kama wanasheria na wataalamu wa ardhi. Kumekuwa na Viongozi wasio waaminifu wa mitaa au vijiji ambao wanaweza kuuza maeneo ya watu wengine kwa kumtafuta mtu asimame kama muuzaji na kiongozi huyu kusimama kama shahidi namba moja, jambo ambalo lina mpa mnunuaji nguvu ya kumuamini muuzaji na kisha kuingia makubaliano. Viongozi hao pia hasa hasa maeneo ya vijijini wamekuwa wakiuza vipande vya Ardhi vinavyomilikiwa na serikali ya kijiji bila kushirikisha wanakijiji. Viongozi kama madiwani nao wamekuwa katika nafasi ya viongozi ambao huchochea migogogoro ya Ardhi pale wanapo simamia mabadiliko ya matumizi ya Ardhi kwa manufaa yao binafsi. Kama maeneo yenye matumizi ya uwanja wa wazi kufanyiwa mabadiliko na kuwa matumizi mengine kwa manufaa yao binafsi.Wazi wazi nafasi ya Wana siasa katika kusimamia shughuli za Ardhi imekuwa na matokeo hasi nakuzalisha migogogro mipya ya Ardhi kila kukicha.
- Mazoea ya kununua Ardhi kiholela: Mara baada ya kuvunja kikoba au mara baada ya kudunduliza kamshahara kako Ka miezi kadhaa unapata taarifa jirani yako anakata kipande chake cha Ardhi anakiuza, basi unamtafuta mwenyekiti na kumalizana nae.Unashindwa kufahamu kumbe ununui kiwanja bali una nunua mgogoro. Mnunuaji anaweza akanunua kiwanja chenye mgogoro kama uwepo wa hati miliki wa muuzaji ilihali amekata kiwanja hicho hicho na kukiuza kwako wewe bila kukupa taarifa. Muuzaji anaweza kukupa taarifa kama eneo lake lina hati lakini je unajua kuwa kutakuwa na gharama nyengine za kubadilisha jina .Uwwzekano wa mnunuaji kuuziwa kiwanja chenye matumizi yasiyo rafiki na matumizi unayo yahitaji kama matumizi ya Hifadhi, makaburi, viwanja vya wazi,hili ni kwa viwanja ambavyo havijapima bado. Mazoe ya kununua Ardhi kiholela Mnunuaji anaweza kuuziwa kiwanja kilichokopewa mkopo benki bila yeye kujua jambo ambalo ni lazima liibue migogoro hapo baadae. Ununuaji wa Ardhi kiholela unaweza kuchangia kushuka Kwa uchumi Kwa mtu mmoja mmoja pindi mahakama utakapo toa maamuzi ambayo sio rafiki kwa upande wako.
- Mahusiano Hafifu Kati ya Wizara ya Ardhi na Wizara ya Ujenzi na uchukuzi. Tunashuhudia nyumba nyingi zikibomolewa au kupigwa alama ya X ilihali mmiliki wa nyumba au kipande hicho cha Ardhi ana hati miliki kwa maana anamiliki kisheria.Wizara ya Ardhi kupitia ofisi zake za Halmamshauri ndio msimamizi mkuu wa kupanga mji kupitia idara ya Mipango miji. Ramani za mipango miji pamoja na ramani ya upimaji ndio ramani zinazo muidhinisha mmiliki wa Ardhi kumilikishwa kisheria kwa kupewa hati. Lakini jambo la mtu huyu kuwekewa X au kuambiwa BOMOA linakuja pale barabara iiliyopo Ardhini Kuonyesha ukubwa zaidi katika rekodi za Tanroad huku ikionekana ndogo katika ramani za mipango miji zilizo idhinishwa na Mkurugenzi wa mipango miji na ramani. Unajiuliza kwanini hizi taasisi mbili haziwasiliani katika kupanga miji na vijiji.Bwana Joseph Haule alibomolewa nyumba yake iliyoko kando kando ya barabara ya Morogoro road ilihali ana hati miliki ya eneo lake pia alikuwa na kibali cha ujenzi(Building permit). Taarifa zaidi waulize wa Kazi wa mbezi na kimara waliopo kando kando ya barabara hiyo. Au nenda pale Morogoro itafute barabara ya Old Daresalaam road utakutana na X za kutosha KWA wakazi wa bigwa na Kola ambao tayari wana Hati miliki lakini wanabomolewa nyumba zao Ili kupisha utanuzi wa barabara ya Kisaki.
- Kukosekana Kwa uaminifu kwa watumishi wa serikali.
Baadhi ya Mambo muhimu ambayo tukiyafwatilia na kuyafanyia Kazi yanaweza kutusaidia tukaepuka kwa nafasi kubwa migogogro ya Ardhi kwa hapa nchini.
- Kwanza mshirikishe mtaalamu wa Ardhi kabla ya kununua kipande cha Ardhi. Mtaalamu wa Ardhi ndio mtu wa kwanza atakaye kuhakikishia usalama wa eneo lako kwa upande Wa matumizi husika ya eneo hilo. Kama eneo matumiziki yake ni rafiki na matumizi ya kuishi au matumizi ambayo hayatukiwa na madhara kwa hapo siku za usoni. Mtaalamu huyo eidha ni mtumishi wa serikali au kutoka kampuni binafsi. Kwa namna nyengine mtaalamu ndie atakaye weza kukagua nyaraka za umiliki za muuzaji na kisha kuyatolea ufafanuzi wa kitaalamu eidha kwa kuhakiki nyaraka hizo kama ni nakala halisi au kujihakiki na taarifa zilizopo katika ofisi za Halamashauri juu ya umiliki huo. Pia mtaalamu ndie atakaye kupa muongozo wa kufwata ili kujua eneo lipo salama kiasi gani kwa upande wa kama eneo limechukuliwa mkopo au la.
- Epuka kununua Ardhi kimazoea/Holela. Hapa namaanisha kuna ulazima wa mnunuaji wa Ardhi kutumia njia ambazo ni salama kama kununua viwanja ambavyo vilishapimwa na kisha kutangazwa na Halmashauri au kampuni binafsi inayo julikana kisheria. Mara nyingi viwanja hivi ukishanunua hapo hapo unaanza Hatua ya kumilikishwa kisheria. Njia hii itakufanya uepuke na gharama nyengine kama kumtafuta mtaalamu kwa ajili ya Ukaguzi. Pia njia hii humuweka salama mnunuaji kudai fidia pindi kutakapo tokea changamoto zozote hasa hasa changamoto ya kiwanja kimoja kuuziwa mtu zaidi ya mmoja.
- Rasimisha kiwanja chako. Kwa mtu ambaye anamiliki kiwanja bila kuwa na nyaraka za umiliki (Hati) kuna ulazima wa hali ya juu kuhakikisha kiwanja chako kimepimwa na kumilikishwa. Upimaji wa kiwanja chako unaweza ukafanywa na kampuni binafsi au Taasisi ya serikali(Halmashauri ya kijiji/mji). Na kisha katika Hatua za kumilikishwa hili linasimamiwa na ofisi ya mkurugenzi wa Halamashauri kupitia Afisa Ardhi. Katika kuomba kupimiwa eneo lako nyaraka kama Muhtasari kutoka katika serikali ya kijij au mtaa ni muhimu sana kwa kuthibitisha umiliki wako kwa ofisi ya mkurugenzi ili aweze kutoa kibali cha Upimaji. Pia Muhtasari huu unaweza ukasimama kama shahidi pindi pakitokea changamoto zozote.
Kivindo lukindo
Muheza Tanga
Upvote
3