Mazoezi ya kadiri ya dakika 150 kwa juma au mazoezi makali zaidi ya dakika 75 kila wiki ni tiba...

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Mwanamke akichunguzwa iwapo ana saratani
ya matiti hospitalini.
Mazoezi yanaweza kusaidia kupona baada ya
kuugua saratani ya matiti lakini ni wanawake
wachache sana wanashiriki katika mazoiezi,
utafiti unasema.
Watafiti wa Marekani, katika ripoti
waliyochapisha katika jarida linaloandika
mambo ya saratani, wanasema kuwa
inajulikana wazi kwamba kufanya mazoezi ya
aina moja au nyingine kunasaidia lakini
imegunduliwa kuwa wanawake hawapendi
kufanya mambo yanayowachosha.
Ni thuluthi moja pekee ya wanawake
inayofanya mazoezi kufikia kiwango
kinachopendekezwa.
Makundi ya kuwasaidia wanaougua saratani
ya matiti nchini Uingereza yanasema
wanawake nchini humo wanahitaji kusaidia
wanawake kufanya mazoezi zaidi baada ya
kutibiwa maradhi hayo.
Utafiti huo uliofanywa Marekani
uliwashirikisha wanawake 1,735 wenye umri
kati ya miaka 20 na 74 waliokuwa na saratani
ya matiti kati ya mwaka 2008 na 2011 katika
Carolina Kaskazini.
Marekani na Uingereza zinapendekezwa kuwa
watu wazima wanapaswa kufanya mazoezi ya
kadiri ya dakika 150 kwa juma moja au
mazoezi makali zaidi ya dakika 75 kila wiki.
Lakini utafiti huu uligundua kuwa ni
wanawake 35 pekee waliougua saratani ndio
wanaofuata maagizo haya ya kufanya
mazoezi baada ya kutibiwa saratani ya matiti.
Nchini Uingereza wahamasishaji wa saratani
ya matiti wanasema wanawake wanapaswa
kufanya mazoezi mengi zaidi nchini humo.
Caroline Dalton, kutoka kundi la Breakthrough
Breast Cancer, alisema: " Mazoezi ya maungo
baada ya mtu kuugua saratani ya matiti
yanaimarisha uwezekano wa aliyeugua
saratani kupona kabisa na kuna ushahidi pia
kuwa yanasaidia kuhakikisha kuwa saratani
ya matiti haimrudii aliyeugua tena.
"Kuendelea na mazoezi pia kunasaidia
mgonjwa kustahimili, wakati wa matibabu na
baadaye, kwa kuimarisha afya yake kwa
ujumla na kuisha maisha bora."
Aliongeza: "Ingawa utafiti huu ulifanyiwa
Marekani badala ya Uingereza, matokeo
yanapendekeza kuwa wanawake ambao
wamegunduliwa kuwa na saratani ya matiti
wanapaswa kusaidiwa ili waendelee kufanya
mazoezi."
"Hakuna mwelekezo kamili wakati huu
kutueleza kikamilifu kiwango cha mazoezi
kinachohitajika baada ya kugunduliwa kuwa
una saratani ya matiti, lakini Breakthrough
Cancer inapendekeza kuwa unapaswa kulenga
kufanya mazoezi kwa masaa matatu u nusu
kwa wiki moja, baada ya kushauriana na
matabibu wako kukuelezea kiwango
kinachokufaa."
Baroness Delyth Morgan, Afisa Mtendaji katika
Breast Cancer Campaign, alisema: "Utafiti huu
unapaswa kuwakumbusha wote kuwa ni
muhimu kwa wanawake walio na saratani ya
matiti kuwa kufanya mazoezi kunachangia
pakubwa kama wataishi au kufariki baada ya
kugunduliwa kuwa una saratani.
"Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa
hata nyongeza ndogo ya mazoezi
yanayofanywa baada ya kugunduliwa kuwa
mtu ana saratani yanaongeza nafasi kwa
mwanamke anayeugua kunusurika.
"Hii ndio sababu ni muhimu kwa wakawake
kupewa mpango kamili wa kufuata
ulioandikwa chini ambao utasaidia ushauri
nasaha kuhusu maisha yao juu ya aina ya
chakula na mazoezi."



Mshirikishe mwenzako...


Chanzo: BBC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…