MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Wakati Lemutuz akiwa anamalizia free trial ya mwezi mmoja kutoka gym fulani (jina kapuni),madaktari kadhaa wamecharuka na aina ya upigaji wake wa mazoezi na kudai mambo na mazoezi anayofanya si salama tena kwa umri wake.
Tofauti na upigaji mazoezi wa kawaida ambao mtu ubeba vitu vizito,Lemutuz yeye kaja na staili mpya ambapo huweka tumbo sakafuni kisha anawekewa vitu vizito mgongoni (mfano watu,madumu ya maji,matofali, mitungi ya gesi nk)
Madaktari hao wameshauri mmiliki huyo wa Gym kumkataza mara moja aina hiyo ya ufanyaji mazoezi au wamsimamishe mazoezi mara moja baada ya Free trial yake kuisha maana kuna uwezekano mkubwa wa kukatika kiuno na hivyo kusababishwa kufikishwa mahakamani kwa wamiliki hao.
Madaktari wengine walidai kuna uwezekano mkubwa mazoezi ya aina hiyo ikawa ni njia mpya ya uongezaji wa nguvu za kiume lkn wakiogopa kuthibitisha isije vijana wote wa Dar wakakimbilia mazoezi hayo.
Wakati hayo yakiendelea gym Lemutuz ameendelea kuwaumiza kichwa wasomi wa tabia za binadamu na saikolojia hasa baada ya kumstudy kwa miaka 10 lkn kushindwa kabisa kujua yeye ni aina gani ya binadam hasa.