Mazungumzo: Jinsi dijitali inavyoweza kukuza Demokrasia Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Tanzania ni moja ya soko linalokuwa zaidi barani Afrika kwenye nyanja ya dijitali, takwimu ya mwaka 2020 ikionyesha watumiaji wa internet wamefika milioni 28.5 kutoka milioni 25.8 mwaka 2019 huku idadi hiyo ikiwa sawa na asilimia 49 ya watu wake. Teknolojia iliyokuja inaruhusu wananchi kuweza kuwafikia viongozi wao moja kwa moja, kupanga na kufanya mijadala ya umma.

March 17 kutakuwa na mazungumzo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Sweden kuhusu eneo la dijitali kwenye demokrasia lengo lake likiwa kutoa jukwaa kwa watendaji wa Serikali na wasio wa kiserikali kuelezea demokrasia kupitia teknolojia na changamoto zake.

Mazungumzo yatafanyika nyumbani kwa balozi wa Sweden nchini, kuwa nami moja kwa moja kesho kuanzia saa tatu asubuhi.

===========

Balozi wa Sweden anatoa salamu za utangulizi na kuwashukuru wote waliohudhuria pia balozi ameongelea vita ya Ukraine na madhara yake kwa Ulaya na Ulimwengu kwa ujumla na kugusia umuhimu wa kulinda demokrasia. Kuhusu teknolojia, amesema Sweden wameona umuhimu wa teknolojia katika Demokrasia na maisha kwa ujumla akitolea mfano miaka kumi nyuma ilimgarimu muda kutafuta taarifa zake za kodi lakini kwasasa ni suala la dakika.

Maxence Melo.jpg

sweden 2.jpg
sweden.jpg

=====

Balozi @sjoberg_a : Haya ni Mazungumzo ya pili ya Demokrasia tunayafanya hapa > Novemba 2021 tulifanya Mjadala kama huu kuhusu Wanawake na ulifanikiwa sana > Nina furaha kubwa tunashirikiana na @JamiiForums kwenye Mazungumzo haya ya Demokrasia Kidigitali.

Tunafanya mijadala hii kwa lengo la kutazama maendeleo ya Demokrasia pamoja na changamoto zinazojitokeza Kwa sasa tunashuhudia Russian Ukrainian War, tunatakiwa kuilinda Demokrasia hapa kwani Dunia nzima itaathirika na Mgogoro huu.

Teknolojia imebadilika sana na kuleta urahisi wa mambo mengi. Licha ya faida zake pia inabidi tutazame hatari za mabadiliko haya Naamini hili litagusiwa kwenye Mazungumzo ya leo kwani zaidi ya Watu bilioni 4 Duniani wameunganishwa Kidigitali.

Tunahitaji kushikana Mikono ili kulea Taasisi zinazohimiza kulinda Demokrasia > Sisi @SwedeninTZ tutaendelea kulea na kutoa ushirikiano wetu hapa ili kuimarisha Demokrasia - @sjoberg_a , Balozi wa Sweden nchini Tanzania.

1647503327019.png

Picha: @sjoberg_a Balozi wa Sweden Nchini Tanzania

Deus Valentine: Mazungumzo haya ya #DemocracyTalkTz yanalenga kutengeneza sehemu salama kwa ajili ya kila mmoja wetu kutoa maoni na uzoefu wake kwenye Demokrasia ya Kidigitali Jopo la Wazungumzaji litaeleza yale waliyopitia kwenye Uwanja wa Demokrasia huku nasi tukiwatia Moyo.

Tutatazama ikiwa tunapewa uhuru wa kufuatilia na kufahamu yanayoendelea Mahakamani Vilevile, upanuzi wa Miundombinu ya Kidigitali je, unasaidia vipi kuongeza ushiriki wa Wananchi kwenye masuala ya Demokrasia?

Tanzania ina watumiaji wa intaneti takribani Milioni 30 mpaka sasa. Kampuni za simu zinaendelea kusajili Watumiaji wapya. Hii ina maana gani? Lengo letu leo sio kupata majibu ya kila swali lakini angalau kutengeneza usawa.

1647503950045.png

Picha: Deus Valentine

Geline Fuko: Naweza kuzungumza kupitia safari ambayo nimeipitia binafsi na kama Taasisi kwenye nafasi ya Kidigitali Tulipoanza kwenye Utendaji, Kazi yangu ilikuwa kuunganisha Sauti za Wananchi pamoja na Serikali ili iweze kutambua Watu wanazungumza nini - @geline_gee.

Tuligundua ukiwekeza Kidigitali inaleta faida na ilitufungua macho sana kwasababu kulikuwa na Sauti nyingi kutoka kwa Wananchi ikiwemo Wanawake Tulizidiwa sana kutokana na taarifa nyingi tulizokuwa tunazipata na baadhi ya taarifa zinaweza hata kufanya ukose usingizi.

Wakati wa mchakato wa Katiba tulikusanya taarifa nyingi kwasababu tulikuwa tukizunguka Nchi nzima Taarifa nyingi zilikuwa kwenye Changamoto ya Uwajibikaji, upatikanaji wa Huduma pamoja na mfumo Utawala mzima kwenye uwanja wa Demokrasia

Tulilazimika kutoa Elimu kwa Viongozi na Wadau mbalimbali kuhusu umuhimu wa nafasi za Kidigitali pamoja na faida zinazopatikana > Nina furaha kwamba tumefanikiwa kwenye hilo na Rais Samia ni mdau mkubwa wa Digitali na atatupatia ushirikiano mkubwa.

Haya ni Mafanikio makubwa tumeyapata kwasababu hapo awali ilikuwa ni ngumu Watu kuelewa kwamba Digitali ni mbinu mojawapo ya kutatua matatizo Kutoka Miaka 10 iliyopita hadi sasa tumeweza kupelekea mabadiliko ya sheria na Sera mbalimbali.

1647504418530.png
Katika picha: Ni Jopo la wazungumzaji katika mjadala wa #DemocracyTalkTz Geline @geline_gee , Maxence Melo @macdemelo na @simplyluca

Maxence Melo:Tulipoanza wengi walidhani Majukwaa ya Kidijitali ni kwaajili ya kupata au kusambaza Umbeya Mambo yalipoanza kuonekana ni ya kweli tumeweza kubadili mtazamo kuhusu nafasi ya Digitali. Sasa hivi tuna Watumiaji wa Intaneti zaidi ya milioni 30 - @macdemelo

Tulipoanza kuhangaika na Kesi dhidi ya @JamiiForums tangu 2016 nilikuwa naona Jaji anaandika maelezo kwenye Karatasi, wakati mwingine anakwambia rudia Hivi sasa hata Mahakama imeanza mchakato wa ‘Digitization’

Nyanja za Kidigitali sasa hivi zinatoa nafasi kwa Watu kutoa maoni yao. Tunaona hata Mamlaka za Serikali zikielekea huko kufahamu Wananchi wanasema nini Hata Kesi za Mahakamani, sasa hivi Watu wanaweza kuzifuatilia kwa kutumia Uwanja wa Digitali.

Maxence Melo: @JamiiForums tunafikia Watu zaidi ya Milioni 3 kwa Siku. Tumeshafanya kazi na Wadau wengi ikiwemo
@Twaweza_NiSisi Hapo awali haikuwa rahisi Jamii Forums kufanya kazi na Serikali lakini kwa sasa tuna makubaliano natakriban 3 na Taasisi za Serikali.

Tulipata changamoto sana kuhusu Sera yetu ya Faragha hata kufikishwa mahakamani lakini kwa sasa naona Serikali imesema wazi kuwa iko katika hatua za mwisho za uandaaji wa Muswada wa Ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za Watanzania.

1647504889600.png

Katika picha: Maxence Melo, Mkurugenzi wa Jamiiforums
Luca Neghesti: Nilipochaguliwa jambo la kwanza nililotaka kufanya ni kutengeneza tovuti kwaajili ya Halmashauri lakini vipingamizi vilikuwa vingi Mpaka sasa bado jambo hilo linaangaliwa na ni takriban Miezi 8. Hili halitakiwi kutufanya turudi nyuma.

Changamoto tunayoipata ni kwamba kwenye Serikali yetu Digitali sio ajenda kubwa sana Mitaa imepangwa hapa tuko vizuri lakini unaweza kukuta hatua chache kutoka hapa Mvua ikinyesha Watu Nyumba zao zinajaa Maji. Hii inaleta ugumu hata kwenye upangaji wa Bajeti.

Kama tunataka kutambua mchango wa Digitali pia tutambue mchango wa Viongozi wa Serikali za Mitaa Kuna taarifa nyingi sana kutoka kwa Wananchi zinakusanywa huko chini kupitia Viongozi hawa.

1647505206364.png

Picha: Aliyeshika kipaza sauti ni Luca Neghesti

Carol Ndosi: Tunahitaji kufanya ‘mapping’ ya kutambua tools za Kidigitali za Tanzania zinazoweza kutatua changamoto mbalimbali ili zifahamike na wengi Kazi yangu inahusika zaidi na Vijana hivyo swali letu kila wakati ni tunaongezaje ushiriki wa Vijana? - @CarolNdosi

Sijajua kama Wenzetu @JamiiForums wanaweza kutupatia taarifa za Vijana wangapi wanashiriki kwenye Mijadala kwenye majukwaa yao Tunaongezaje ushiriki wao? Inafaa kuwauliza ni kitu gani wanahitaji. Je, ni 'Mobile Apps' au nini ili waweze kuongea kupitia Digitali?

Deo Bwire: @macdemelo ametaja Mafanikio makubwa ambayo tumeyapata Kidigitali mpaka sasa Miaka 5 iliyopita ilikuwa hatuwezi kukutana kuongelea Mafanikio kwasababu Changamoto zilikuwa nyingi zaidi. Tusiache kuzungumzia ubadilishaji wa Sheria na Sera mbalimbali.

1647505638482.png

Picha: Deo Bwire

Ismail Biro (Tanzania Bora Initiative): Katika kazi zetu tunakusanya Maudhui mengi sana Kwenye hili, tumejifunza kwamba ni jambo moja kuwashawishi Watu washiriki kutoa maoni lakini ni jambo lingine kuwaelewesha kwanini washiriki kutoa maoni.

1647505721939.png

Picha: Ismail Biro (Tanzania Bora Initiative):

Ivan Atuyambe: Tunaweza kuzungumza Mafanikio mengi yanayokuja lakini sijasikia kuhusu hatari zinazoweza kujitokeza ili tuweze kulinganisha Kuna Watu wamepata madhara kwasababu hawajui kulinda Vifaa vyao vya Kieletroniki na wengine wamedhurika kwa kuongea Mtandaoni.

Idd Amin alisema 'Naweza kukuhakikisha Usalama wa kuzungumza ila siwezi kukuhakikisha Usalama baada ya kuzungumza' Tunatengeneza mifumo ya Kidigitali lakini je, tunajiandaaje kuwalinda Watumiaji?

Watu wa 'Born Before Computer' je, wanaelewa kile tunachokizungumza ili kuweza kushiriki? Kuna Watu hawajui kutumia Vifaa vya Kieletroniki na wengine hawana huduma za Intaneti. Jiulize, ukimpa Intaneti ni kitu gani anakwemda kukifanya huko?

Tunaambiana kuna Pasipoti ya Kielektroniki lakini utaratibu mzima wa kuipata haukamiliki Mtandaoni > Bado Mtu unalazimika kujaza fomu na kwenda kupanga foleni Ofisi za @UhamiajiTz

1647505899857.png

Picha: Ivan Atuyambe

Cecilia Assey (@WiLDAFTz ): Mimi nilikuwa Mwangalizi wa Uchaguzi 2010 na tulipewa namba ya kuripoti mambo tutakayoona hayaendi sawa Nakumbuka kutuma taarifa nyingi na nilitegemea hata baada ya Uchaguzi kwamba kuna hatua zingechukuliwa ila hakuna kilichofanyika.
1647506307560.png

Picha: Cecilia Assey

Mike @MikieMushi: Je, nafasi ya Kidigitali ni sehemu ambapo Watu wanapaamini? Mzee Majuto alipofariki Joti alizungumzia wa kwanza Mtandaoni na alishambuliwa sana kwamba anamuombea kifo lakini Uhuru Media walipotangaza kila Mtu akaanza kutoa pole kwa Familia.

1647506510123.png

Picha: Mike Mushi
Aidan Eyakuze @aeyakuze : Serikali ya Kidigitali sio Demokrasia ya Kidigitali. Ushiriki wa Watu Kidigitali nao haumaanishi Demokrasia China ni moja ya nchi zilizofanikiwa katika kutoa huduma kidigitali lakini je, hii inamaanisha Demokrasia?

Tunatakiwa kuifikiria Serikali ya Kidemokrasia katika Uwanja wa Kidigitali tunaoutengeneza Tunatakiwa kuzungumza kuhusu namna gani Serikali inaongoza Kidemokrasia kupitia Uwanja wa Kidigitali.

1647507734468.png

Picha: Aidan Eyakuze
Kiiya JK: Tuna utafiti kutoka UDSM ambao umefanyika Mwanza unasema takriban 30% ya Wanafunzi walioko Bweni huingia Mtandaoni kwa kutumia laini 1 ya Simu Je, wakiingia Mtandaoni wanakutana na taarifa gani?
1647507983230.png
 
Tanzania ni moja ya soko linalokuwa zaidi barani Afrika kwenye nyanja ya dijitali, takwimu ya mwaka 2020 ikionyesha watumiaji wa internet wamefika milioni 28.5 kutoka milioni 25.8 mwaka 2019 huku idadi hiyo ikiwa sawa na asilimia 49 ya watu wake. Teknolojia iliyokuja inaruhusu wananchi kuweza kuwafikia viongozi wao moja kwa moja, kupanga na kufanya mijadala ya umma.

March 17 kutakuwa na mazungumzo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Sweden kuhusu eneo la dijitali kwenye demokrasia lengo lake likiwa kutoa jukwaa kwa watendaji wa Serikali na wasio wa kiserikali kuelezea demokrasia kupitia teknolojia na changamoto zake.

Mazungumzo yatafanyika nyumbani kwa balozi wa Sweden nchini, kuwa nami moja kwa moja kesho kuanzia saa tatu asubuhi.

View attachment 2152906
Tutafuatilia
 
Hili ni jambo zuri sana, Upo umuhimu Mkubwa sana kwa Wananchi na Viongozi kujua vyema mchango wa dijitali katika kukuza demokrasia na kusimamia haki za binadamu kwa ujumla.

Kitu nachojiuliza hapa ni je viongozi wa serikali na wananchi wanafanya juhudi yoyote kujielimisha kuhusu digitali ili kujua namna wanavyoweza kukuza demokrasia kidijitali kuendana na kasi ya sasa?

Kama hakuna juhudi je nini kifanyike ili kuhakikisha tunaitumia kasi na maendeleo ya kidijitali kukuza demokrasia?
 
Kwa nini Viongozi wasiwe wanafungua mijadala ya moja kwa moja na wananchi wakasikia kero zao, maoni na mapendekezo kuliko kusubiri kuletewa na wawakilishi ambao pengine viongozi wanaweza wasifikishe zote?

Maana Digitali inaweza kutoa fursa ya kukuza Demekrasia kwa watu kuhoji, kukosoa utendaji wa serikali na viongozi, kutoa maoni yao na kusema vipaumbele vyao muhimu moja kwa moja bila kusubiri uwakiliahi bungeni. Hii itachangia viongozi kushtuka na kutekeleza wajibu wao.
 
Digitali ni kiungo muhimu katika kukuza Demokrasia wakati huu ambapo ukuaji wa sayansi na teknolojia unashika kasi hapa nyumbani na duniani kote

Mjadala huu wa 'Demokrasia Kidigitali' na mingine ya aina hii ni itatoa fursa ya kujifunza, kuelewa, kushiriki na kuwa sehemu ya mabadiliko

Natamani washiriki wahoji kitu kuhusu changamoto wazipatazo 'Digital Citizens' ambao wakati mwingine kosa lao pekee linakuwa kuchapisha maoni/ kusema ukweli kwa nia njema kabisa lakini wakaonekana wasaliti, wana nia ovu na wenye kukosa uzalendo!

Vilevile, tumejipangaje kuwafikia hata wa Vijijini kwenye Digitali? Serikali ina mikakati gani kwenye hili ili kuendelea kukuza Demokrasia? Maana hata Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema katika Mahojiano kadhaa kwamba wanasoma na kufuatilia yanayoendelea huko Digitalini
 
Hili ni jambo zuri sana, Upo umuhimu Mkubwa sana kwa Wananchi na Viongozi kujua vyema mchango wa dijitali katika kukuza demokrasia na kusimamia haki za binadamu kwa ujumla.

Kitu nachojiuliza hapa ni je viongozi wa serikali na wananchi wanafanya juhudi yoyote kujielimisha kuhusu digitali ili kujua namna wanavyoweza kukuza demokrasia kidijitali kuendana na kasi ya sasa?

Kama hakuna juhudi je nini kifanyike ili kuhakikisha tunaitumia kasi na maendeleo ya kidijitali kukuza demokrasia?
Kabisa, wanapaswa kwenda na wakati. Inasikitisha sana kukuta website za Serikali au Taasisi za Umma zina taarifa za nyuma sana.

Wanashindwa kusasisha taarifa kwa wakati ili wananchi wapate taarifa sahihi na mapema.
 
Tanzania ni moja ya soko linalokuwa zaidi barani Afrika kwenye nyanja ya dijitali, takwimu ya mwaka 2020 ikionyesha watumiaji wa internet wamefika milioni 28.5 kutoka milioni 25.8 mwaka 2019 huku idadi hiyo ikiwa sawa na asilimia 49 ya watu wake. Teknolojia iliyokuja inaruhusu wananchi kuweza kuwafikia viongozi wao moja kwa moja, kupanga na kufanya mijadala ya umma.

March 17 kutakuwa na mazungumzo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Sweden kuhusu eneo la dijitali kwenye demokrasia lengo lake likiwa kutoa jukwaa kwa watendaji wa Serikali na wasio wa kiserikali kuelezea demokrasia kupitia teknolojia na changamoto zake.

Mazungumzo yatafanyika nyumbani kwa balozi wa Sweden nchini, kuwa nami moja kwa moja kesho kuanzia saa tatu asubuhi.

View attachment 2152906
Ongezeko la watumiaji linamaanisha ndipo dunia inapokwenda, kama ongezeko ni kubwa viongozi na mamlaka watambue kuwa uwanja wa demokrasia nao unatakiwa kukua, haiwezi kubaki vilevile wakati watumiaji wanaongezeka.

Wasipokubali kwenda na mabadiliko ndipo hapo inakuwa ngumu kuwa na maelewano baina ya pande mbili.
 
Kwa sasa Digitali imekuwa kichocheo kikubwa cha kukuza Demokrasia nchini, hili haliwezi kukwepeka tena maana dunia ya kidigitali ndiko ilikotupeleka kwa sasa.

Kwa siku za hivi karibu makampuni ya mawasiliano yalipandisha maradufu gharama za vifurushi na hasa vya Intaneti na kupelekea baadhi ya watu kushindwa kumudu gharama hivyo kupelekea baadhi kuacha kujiunga na wengine kutumia muda mchache kwenye mtandaoni.

Je, Serikali, Mamlaka zake husika na makampuni ya mawasiliano hayaoni sababu za makusudi kupunguza gharama za vifurushi viwe rafiki ili kuongeza idadi zaidi ya watumiaji wa intaneti ili kukuza Demokrasia Kidigitali?
 
Hizi kampuni ni za kina Rostam na Lowasa + CCM wengine
 
Tanzania ni moja ya soko linalokuwa zaidi barani Afrika kwenye nyanja ya dijitali, takwimu ya mwaka 2020 ikionyesha watumiaji wa internet wamefika milioni 28.5 kutoka milioni 25.8 mwaka 2019 huku idadi hiyo ikiwa sawa na asilimia 49 ya watu wake. Teknolojia iliyokuja inaruhusu wananchi kuweza kuwafikia viongozi wao moja kwa moja, kupanga na kufanya mijadala ya umma.

March 17 kutakuwa na mazungumzo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Sweden kuhusu eneo la dijitali kwenye demokrasia lengo lake likiwa kutoa jukwaa kwa watendaji wa Serikali na wasio wa kiserikali kuelezea demokrasia kupitia teknolojia na changamoto zake.

Mazungumzo yatafanyika nyumbani kwa balozi wa Sweden nchini, kuwa nami moja kwa moja kesho kuanzia saa tatu asubuhi.

===========

Balozi wa Sweden anatoa salamu za utangulizi na kuwashukuru wote waliohudhuria pia balozi ameongelea vita ya Ukraine na madhara yake kwa Ulaya na Ulimwengu kwa ujumla na kugusia umuhimu wa kulinda demokrasia. Kuhusu teknolojia, amesema Sweden wameona umuhimu wa teknolojia katika Demokrasia na maisha kwa ujumla akitolea mfano miaka kumi nyuma ilimgarimu muda kutafuta taarifa zake za kodi lakini kwasasa ni suala la dakika.

=====

Balozi @sjoberg_a : Haya ni Mazungumzo ya pili ya Demokrasia tunayafanya hapa > Novemba 2021 tulifanya Mjadala kama huu kuhusu Wanawake na ulifanikiwa sana > Nina furaha kubwa tunashirikiana na @JamiiForums kwenye Mazungumzo haya ya Demokrasia Kidigitali.

Tunafanya mijadala hii kwa lengo la kutazama maendeleo ya Demokrasia pamoja na changamoto zinazojitokeza Kwa sasa tunashuhudia Russian Ukrainian War, tunatakiwa kuilinda Demokrasia hapa kwani Dunia nzima itaathirika na Mgogoro huu.

Teknolojia imebadilika sana na kuleta urahisi wa mambo mengi. Licha ya faida zake pia inabidi tutazame hatari za mabadiliko haya Naamini hili litagusiwa kwenye Mazungumzo ya leo kwani zaidi ya Watu bilioni 4 Duniani wameunganishwa Kidigitali.

Tunahitaji kushikana Mikono ili kulea Taasisi zinazohimiza kulinda Demokrasia > Sisi @SwedeninTZ tutaendelea kulea na kutoa ushirikiano wetu hapa ili kuimarisha Demokrasia - @sjoberg_a , Balozi wa Sweden nchini Tanzania.

View attachment 2153752
Picha: @sjoberg_a Balozi wa Sweden Nchini Tanzania

Deus Valentine: Mazungumzo haya ya #DemocracyTalkTz yanalenga kutengeneza sehemu salama kwa ajili ya kila mmoja wetu kutoa maoni na uzoefu wake kwenye Demokrasia ya Kidigitali Jopo la Wazungumzaji litaeleza yale waliyopitia kwenye Uwanja wa Demokrasia huku nasi tukiwatia Moyo.

Tutatazama ikiwa tunapewa uhuru wa kufuatilia na kufahamu yanayoendelea Mahakamani Vilevile, upanuzi wa Miundombinu ya Kidigitali je, unasaidia vipi kuongeza ushiriki wa Wananchi kwenye masuala ya Demokrasia?

Tanzania ina watumiaji wa intaneti takribani Milioni 30 mpaka sasa. Kampuni za simu zinaendelea kusajili Watumiaji wapya. Hii ina maana gani? Lengo letu leo sio kupata majibu ya kila swali lakini angalau kutengeneza usawa.

View attachment 2153765
Picha: Deus Valentine

Geline Fuko: Naweza kuzungumza kupitia safari ambayo nimeipitia binafsi na kama Taasisi kwenye nafasi ya Kidigitali Tulipoanza kwenye Utendaji, Kazi yangu ilikuwa kuunganisha Sauti za Wananchi pamoja na Serikali ili iweze kutambua Watu wanazungumza nini - @geline_gee

Tuligundua ukiwekeza Kidigitali inaleta faida na ilitufungua macho sana kwasababu kulikuwa na Sauti nyingi kutoka kwa Wananchi ikiwemo Wanawake Tulizidiwa sana kutokana na taarifa nyingi tulizokuwa tunazipata na baadhi ya taarifa zinaweza hata kufanya ukose usingizi.

Wakati wa mchakato wa Katiba tulikusanya taarifa nyingi kwasababu tulikuwa tukizunguka Nchi nzima Taarifa nyingi zilikuwa kwenye Changamoto ya Uwajibikaji, upatikanaji wa Huduma pamoja na mfumo Utawala mzima kwenye uwanja wa Demokrasia

Tulilazimika kutoa Elimu kwa Viongozi na Wadau mbalimbali kuhusu umuhimu wa nafasi za Kidigitali pamoja na faida zinazopatikana > Nina furaha kwamba tumefanikiwa kwenye hilo na Rais Samia ni mdau mkubwa wa Digitali na atatupatia ushirikiano mkubwa.

Haya ni Mafanikio makubwa tumeyapata kwasababu hapo awali ilikuwa ni ngumu Watu kuelewa kwamba Digitali ni mbinu mojawapo ya kutatua matatizo Kutoka Miaka 10 iliyopita hadi sasa tumeweza kupelekea mabadiliko ya sheria na Sera mbalimbali.
Tuko pamoja
 
Sidhani kama demokrasia imepewa kipaumbele hapa nchini kwetu zaidi ya ukandamizaji tu sijui tunakwenda wapi
 
Back
Top Bottom