Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Wajumbe wa Urusi na Wajumbe wa Ukraine wanatarajiwa kukutana leo kwa mazungumzo nchini Belarus ikiwa ni mara ya pili ya mazungumzo ya ana kwa ana tangu Urusi ilipoivamia Ukraine kijeshi siku nane zilizopita.
Ripoti zinasema kuwa Wawakilishi wa pande zote watakutana katika eneo la Brest nchini Belarus linalopakana na Poland.
Katika hotuba ya video kwa Taifa la Ukraine leo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewahimiza Waukraine kuendelea kupambana lakini hakutaja kama Warusi wamekamata miji yoyote.
Urusi leo imekiri kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi huu kwamba karibu Wanajeshi 500 wa Urusi wameuawa katika mapigano na karibu 1,600 wamejeruhiwa huku Idara ya dharura ya Ukraine ikisema zaidi ya Raia 2,000 wameuawa.
Pia soma:Ukraine yakubali mazungumzo ya amani na Urusi, ni leo Jumatatu