Mazungumzo kuhusu mgogoro wa DRC na M23 ni unafiki na uoga tu. Wawaambie Rwanda na Uganda ukweli

Mazungumzo kuhusu mgogoro wa DRC na M23 ni unafiki na uoga tu. Wawaambie Rwanda na Uganda ukweli

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Mgogoro wa Congo DR hatuhitaji mazungumzo ili kupata suluhu,

Maadui wa Congo DR ni wajumbe wa huo mkutano ni wazi kuwa ni Kagame na Mseveni, Sasa hawa ndo wapo kinafiki ati wanashauri mbinu za mapatano.

Yaani wakuu wa nchi wanaitisha mazungumzo dhidi ya waasi wa M 23 Kwa maana wameshindwa kutuma majeshi kuwafyekelea mbali hao waasi.

Wawambie wazi washirika wa M 23 ambao ni Rwanda na Uganda kuacha huo mpango wao mara 1

EAC haina nguvu kabisa, kama nchi zenyewe zinavamiana wao Kwa wao

Kenya Sasa anaingia Congo kuungana na Rwanda na Uganda kuleta machafuko na kuchota madini, Kenya hajacheza na fursa. Hapo msamalia ni Samia na Ndayishimye tu
Hakuna suluhu Congo DR huo ni unafiki
 
Hivi Wacongo wenyewe wameshindwaje kumalizana na maadui zao?

Mbona kule Afghanistan wataliban waliwafyeka wamarekani bila msaada wa waarabu wenzao?

Kule vietnam nako wamarekani walikimbizwa na jeshi la Vietnam bila msaada wa Jeshi kutoka external countries?

wakongoman kama mafala vile... kazi kukata mauno tu kama mangese..
 
Mashabiki mwa Congo DR ni pagumu Kuna giants Rwanda na Uganda kupambana Nazo ni ngumu na Sasa Kenya anaingia kuchota madini
 
Iko wazi kuwa kweli banyamulenge wana haki ya kuwa raia wa Congo na kupata haki zao zote za msingi kama raia wa nchi hiyo

Lakini Je inapofikia raia hawana uzalendo tena na nchi ambayo kimsingi ni yao na wanaonesha mapenzi na utii kwa kiongozi wa Taifa hasimu tena mwenye asili yao hao bado ni raia au wahaini?kuna cha kujadili hapo?Hao wakongo gani ambao miaka yao yote wako royal kwa utawala wa Rwanda ni raia wema kweli hawa?

Serikali ya Congo wa si jeshi...Congo na watu/wanacongo wawe serious na nchi yao vinginevyo ni aibu kubwa na mwishowe ni laana

Kama kweli viongozi wa SADC na EA pamoja na vyombo vyote vya usalama nia yao ni kuleta amani kweli wameshindwa na M23 pamoja na jeshi la Rwanda?

Ni aibu kwa vizazi vijavyo kwa viongozi wa Africa kushindwa kushughulikia mgogoro wa ndani wakati akina Lumumba ,Nyerere,Nkwame Nkuruma walikutana na mazingira magumu zaidi

AU na jumuiya zote za Africa kweli zimeshindwa kuichukulia hatua Rwanda?

Ni kwa mantiki hiyo hiyo Africa tuko nyuma ,viongozi wetu hawawezi kuchukua hatua,sababu kubwa pia wao si safi,kumbe mtu ambae hawezi kufanya maamuzi ya kujenga lau sehemu ya kujihifadhi akijisaidia/kuchimba choo...huyo ataweza kujenga barabara,reli,na miundo mbinu mingine kama ya elimu na afya bila kuamuliwa na wengine?

Mungu atuhurumie Africa,lakini atusamehe kwa sababu tunaifedhehesha race ya Africa ulimwenguni kote ,kwa kusema au kumwambia Mungu alituumba dhaifu

Nenda Africa Kusini,America,Brazil nk asili ya mtu mweusi imekua kama laana
 
Mashabiki mwa Congo DR ni pagumu Kuna giants Rwanda na Uganda kupambana Nazo ni ngumu na Sasa Kenya anaingia kuchota madini
kaka twende makumbusho tukale bia
hizi mambo kumbe ni ngumu sana kumaliza.

Hapo bado wazungu nao wako wanachota minerals kimya kimya
 
Mashabiki mwa Congo DR ni pagumu Kuna giants Rwanda na Uganda kupambana Nazo ni ngumu na Sasa Kenya anaingia kuchota madini
Hayo madini Kenya atayasafirisha kwa ndege za mizigo kutoka Goma mpaka Nairobi?
 
waCongo walioko Lubumbashi aka Katanga yote, waliopo Kinshasa, Maniema, Kisangani nk waende kule mashariki wakalitetee Taifa lao dhidi ya wavamizi.

Watanzania Kwa maelfu walikwenda Uganda kulitetea Taifa lao dhidi ya Nduli IDI Amin dada,

Watutsi na RPF waliingia Kigali kuukomboa Utaifa wao dhidi ya Hutu, mpaka leo Tutsi wanaheshimika.

Heshima unaijenga mwenyewe, haijengwi kwa kuonewa huruma na wengine na kusaidiwasaidiwa.
 
Hivi Wacongo wenyewe wameshindwaje kumalizana na maadui zao?

Mbona kule Afghanistan wataliban waliwafyeka wamarekani bila msaada wa waarabu wenzao?

Kule vietnam nako wamarekani walikimbizwa na jeshi la Vietnam bila msaada wa Jeshi kutoka external countries?

wakongoman kama mafala vile... kazi kukata mauno tu kama mangese..
Hamna watu wanafiki kama wacongo,unafiki na njaa zao ndio zinazofanya ile vita kuwa ngumu,maana hata hayo mataifa yaliyopo kule kuwasaidia kijeshi ni wacongo wenyewe ndio uwa wanawachoma kwa waasi
 
waCongo walioko Lubumbashi aka Katanga yote, waliopo Kinshasa, Maniema, Kisangani nk waende kule mashariki wakalitetee Taifa lao dhidi ya wavamizi.

Watanzania Kwa maelfu walikwenda Uganda kulitetea Taifa lao dhidi ya Nduli IDI Amin dada,

Watutsi na RPF waliingia Kigali kuukomboa Utaifa wao dhidi ya Hutu, mpaka leo Tutsi wanaheshimika.

Heshima unaijenga mwenyewe, haijengwi kwa kuonewa huruma na wengine na kusaidiwasaidiwa.
Well said
 
Back
Top Bottom