Mazungumzo kuhusu nyungu na chanjo ya COVID-19

Mazungumzo kuhusu nyungu na chanjo ya COVID-19

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
MIMI NA YEYE

Yeye: Wewe endelea kuwatetea wazungu. Sisi ni matajiri na wao wanatuonea wivu. Hayo machanjo yao wasituletee.

Mimi: Kuna chanjo ngapi unazojua tunapewa na zinatoka kwa wazungu?

Yeye: Zipo nyingi lakini mbona wameshindwa kutengeneza chanjo ya UKIMWI?

Mimi: Unajua ARV na CONDOMs zinatoka wapi?

Yeye: Wewe ndio huelewi. Hii Corona imetengenezwa itumiwe kama njia ya kutulazimishia chanjo. Tunapiga nyungu.

Mimi: Kwa hiyo WAZUNGU wameamua kutumia gharama kubwa kutengeneza kirusi kuwaua Waafrika, kirusi ambaye anakufa kwa kunywa malimao na tangawizi? Sasa chanjo atauzaje? Si hasara? Hebu niambie kwa takwimu, nyungu imethibitishwa kwa ubora wa kiasi gani kupambana na corona?

Yeye: Nyungu imethibitishwa na Mungu. Nakuambia Mungu wetu ni mkuu ametupigania corona haitusumbui.

Mimi: Unamwamini Mungu na unaamini kuwa anatukinga na corona?

Yeye: Wewe unapinga kila kitu. Nilidhani mtu wa maana, unatufundisha kila siku neno la Mungu, ina maana humwamini Mungu?

Mimi: Kabla sijajibu natamani kujua ni Mungu yupi unayemzungumzia? Mungu huyu wa kwenye Biblia ambaye WAZUNGU walitufundisha na kumtumia kutufanya watumwa, au mungu wa mlimani na kwenye miti mikubwa ambao babu zetu walikuwa wakimwabudu?

Yeye: Ndio maana tunapiga Nyungu, wengi imewasaidia.

Mimi: Unaposema WENGI unamaanisha nini? Marafiki zako fb wanaoitangaza nyungu, marafiki zako mtaani wanaosema kijiweni kuwa wametumia nyungu, au familia yako inayotumia nyungu? Kuna uthibitisho UPU kuhusiana na WENGI kutumia nyungu?

Yeye. Ndio, WENGI,
Ndio, Mungu anatusaidia.

Mimi. Ok. Kwa hiyo tunakubali kuwa chanjo na dawa za WAZUNGU TUNAZITAKA (isipokuwa tu ya corona) kwa kuwa WAZUNGU wanaotupa hizi sio wale wanaotutengenezea chanjo ya corona

Tunakubali kuwa Mungu tuliyeletewa habari zake na MZUNGU, tumshikilie, kwa kuwa walikuwa wanatupenda sana na wakati huo tulikuwa MASKINI sana wakatuonea huruma, wakatuletea NENO la Mungu ili mtajirike... Na sasa mmetajirika bado mnamshikilia.

Sasa ikiwa TUNAAMINI wazungu HAWAKUKOSEA kutuletea MUNGU anayeweza kuiondoa CORONA, tunaamini kuwa wazungu wanatupenda hadi kutuletea ARV na condoms,
Ila ni chanjo ya CORONA tu ndio ina matatizo, mengineyo yapo shwari kabisa....

Hivi tumeshawahi kuchunguza kama Mungu waliyetuletea HAWAKUTUDANGANYA? Ama ARVS na chanjo za watoto tumethibitisha BILA SHAKA kuwa zinafaa?

Yeye: typing.....

Mimi: waiting...

Unaweza ukamsaidia kujibu
✍🏼️ Kwa hisani ya BHWJ
 
Mungu siku zote anatumiwa na wajinga kujiliwaza, ndio maana hili bara lipo hapa lilipo kwasababu ya mawazo mgando, wakati werevu wanajiongeza sisi tunabaki na Mungu, halafu ghafla tunaambiwa sasa tupo level 4 ya maambukizi hapo tunaanza kuwatukana waliotujulisha matokeo ya ujinga wetu.
 
Kwanza wewe umethibitisha kua huo ugonjwa wa korona upo? Na hizo chanjo wanazoleta umethibitisha ubora wake? Nan alitumia akapona?
Umezungumzia ukimwi, mbona wao hauwatesi kama sisi? Hawafanyi ngono? Nani anaongoza kwa kurekodi Porn? Arv haiwezi kua biashara?

Hata wewe unaweza kua ni mweupe kichwani ila hujijui, and that is too bad.
 
Back
Top Bottom