Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAZUNGUMZO MAFUPI NA KITUKUU CHA ABUSHIRI BIN SALIM AL HARITH
Leo jioni nimeingia katika duka moja.
Baada ya salaam kijana aliyekuwa pale dukani nyuma ya counter akanishukuru kwa kumwandika babu yake.
Mimi nikamuulia, ''Babu yako gani niliyemwandika?''
Kijana akanijibu, "Abushiri bin Salim.''
Nikashtuka nikamuuliza, ''Abushiri ni babu yako?''
"Naam ni babu yangu kwa upande wa kikeni kwangu bibi yangu Abushuri ni babu yake.''
Nikamuuliza kama hakuwa hafanyi maskhara.
Hapo huyu kijana akinitajia jina la mama yake na likaenda na kuishia kwa Abushiri.
Hapo nikatulia na yeye akawa katulia nikaanza kuuliza maswali ikiwa anajua historia ya huyu babu yake mkuu.
Alinijibu kuwa Abushiri katokea Zanzibar na alikuwa na wake wengi ambao wote walizaa watoto.
Tukaendelea na mazungumzo mimi nikitaka kujua kama kuna kumbukumbu yoyote katika familia yao kuhusu Abushiri.
Kijana akaniambia kuwa bibi yake kamfahamisha kuwa ardhi ambayo wanayo hivi sasa Zanzibar ni ya Abushiri.
Akaendelea kunifahamisha kuwa Abushiri babu yake mkuu alikuwa mtu tajiri sana Zanzibar na aliacha mashamba makubwa ambayo baada ya kuuliwa yalitaifishwa na Wajerumani ila ardhi kidogo iliyoachiwa familia.
Kijana akaniongezea akanambia kuwa kuna uvumi kuwa Abushiri alizika hazina kubwa katika ardhi yake na huko nyuma baada ya kifo chake kulikuwa na majaribio ya kutaka kuitafuta hazina hii lakini familia ilisimama kidete kupinga kuingiliwa faragha yao.
Ardhi hii imebaki katika familia hadi hivi sasa.