Mazungumzo na Kabangu: Simba nimeanza kuwaelewa

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Hivi karibuni kuna mwandishi mmoja wa habari za michezo aliandika kuwa eti Simba inasajili sana sana Uganda na Yanga inasajili Congo. Kukatokea viandishi uchwara vikataka kuanza kupandikiza mind kwa watu wa Simba kuwa wao wanastahili kusajili sehemu yoyote hasa Uganda ila si Congo.

Walifika mahali wakaanza kusema eti Yanga inapendwa Congo ndio maana Pepe Kalle aliimba wimbo ambao hadi sasa unaishi kuisifia Yanga.Lakini huku wakijisahau kuwa Pepe Kalle alikuwa mpenzi wa soka na aliwahi kuimba wimbo wa Roger Miller. Huu wa Yanga Gulamali alitoa pesa ili aimbwe na alicheza kete nzuri ambapo hadi leo hata sisi washabiki wa Simba tunaupenda.

Simba nimewaelewa kwa sababu Congo imejaliwa watu wenye vipaji na spirit ya kujituma kutodharau kazi.Hiyo spirit ni muhimu sana kuliko kujua mpira pekee.

Yanga msiwaone wana base sana Congo mkafikiri wajinga.Hawa wacongo wanauwezo wa kuoambana bila kukata tamaa.Si watu wanaoridhika na kuwa na kiburi linapofika suala la kazi.Ni watu nawaekewa sana.

Nawasihi Simba msiingie kwenye mtego wa hawa waandishi ambao akili zao ni za kawaida tu lakini wanataka kutumia media kutengeneza mind za wanasimba kuwa wao na Congo eti hawaendani.Kuna baadhi ya washabiki walishaanza kusema eti Simba na Congo wapi na wapi. Simba angalieni sana hizi propaganda.
 
Kinacho haribu mpira wa tz ni siasa za ccm kupenyezwa kwenye mpira, wewe angalia uchaguzi wa urais tff ndio utaelewa vizuri.
 
Wanamsimbazi/Mikia/Wamatopeni fanyeni usajili kwa kadri muwezavyo hatutaki kelele baadae.
 
Kelele zetu sisi ni kushangilia vikombe,tofauti na kelele za jirani ambaye amezoea kulia anaonewa na TFF.Ameshiriki CECAFA wakalia na waamuzi eti wanaonewa.
Sasa mnaenda CAF huko ndio mtajua hamjui maana huwa mnacheza ujinga mwingi sana katika ligi na mnabebwa
Wanamsimbazi/Mikia/Wamatopeni fanyeni usajili kwa kadri muwezavyo hatutaki kelele baadae.
 
Hivi yule Deo Kanda ni Mganda?Na Patrick Mafisango Marehemu alikuwa Mganda?
 
Huna ulichoandika. Km viongoz wangekuwa usemavyo si wasingeongeza mchezaji. Lkn unafahamu kuwa Mugallu ni m congo?
 
Wacongo ni wavivu sana trust me!nawajua wacongo live na sio kwenye mitandao!ndio maana kazi za wanaume wengi wa congo ni Saluni za kike na kujichubua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…