Mazungumzo na Maggid Mjengwa wasifu wa Julius Nyerere: prof. Haroub Othman ns prof. Ahmed Mohiddin

Mazungumzo na Maggid Mjengwa wasifu wa Julius Nyerere: prof. Haroub Othman ns prof. Ahmed Mohiddin

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAZUNGUMZO NA MAGGID MJENGWA WASIFU WA JULIUS NYERERE: PROF. HAROUB OTHMAN NA PROF. AHMED MOHIDDIN

Prof. Haroub Othman naamini ndiye mtu aliyetaka sana uandikwe wasifu wa Mwalimu Julius Nyerere na hii nasema kwa kuwa aliniambia kuwa baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes kuna maswali mengi yalimtatiza.

Prof. Haroub hakuwa anajua kwa undani uhusiano uliokuwapo baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere katika mengi kubwa ikiwa suala la kuasisi chama cha TANU na hili nadhani yeye lilimtaabisha kwa kukosa kujua ni vipi Nyerere aliingia katika uongozi wa TAA na mwishowe kuwa kiongozi wa TANU.

Bila shaka Prof. Haroub alitaabishwa kama wengi walivyokuja kuhangaishwa na historia hii.

Prof. Haroub alionana na Mwalimu kuhusu yeye kuandika maisha yake kwa kuwa alimsisitizia Mwalimu kuwa kuna mimi na Ali Muhsin Barwani tumeandika mengi kuhusu yeye ambayo si wengi wanayajua na ni muhimu ulimwengu ukasikia upande wake.

Prof. Haroub alitaabishwa na ile fikra ni nani huyu Abdul Sykes katika maisha yake Nyerere na katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Prof. Haroub alitambua kuwa kwa mimi kuandika maisha ya Abdul Sykes na yote yaliyopitika katika historia ya TANU ni muhimu na yeye Mwalimu akaeleza historia yake.

Mwalimu alimkubalia lakini kitabu hakikupata kuandikwa.

Nimemtembelea Prof. Taji Ahmed Mohiddin nyumbani kwake Kikambala.

Prof. Mohiddin kwa kinywa chake kanieleza jinsi aliyokuwa kipenzi cha Mwalimu wakikubaliana katika mengi katika siasa ya Ujamaa.

Prof. Mohiddin ana kanda za Nyerere kanda zenye hotuba zake kuanzia miaka ya 1950 wakati wa kupiganiahistori uhuru hadi mwisho wa maisha yake.

Kanda hizi amezihifadhi ndani ya jokofu kwa ubaridi ili zisiharibike na baadhi ya kanda hizi ziko katika ''reels'' na ana mashine ya kuzicheza.

Prof. Mohiddin akanifahamisha kuwa Mwalimu mara ya mwisho alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Msasani alimuomba amsaidie kuandika kitabu cha maisha yake na yeye alikubali.

Prof. Haroub akimpenda sana Mwalimu na alipenda sana aache nyuma kumbukumbu iliyokaa sawa.

Haukupita muda mrefu, hata mwaka mmoja Mwalimu akafariki.

Prof. Haroub angekuwa hai angefurahi sana kuona kuwa fikra yake aliyompa Mwalimu ya kuandikia kitabu cha maisha yake imetekelezwa kwa vitendo.
 

Attachments

  • PROF. MUHIDIN NA LENIN.jpg
    PROF. MUHIDIN NA LENIN.jpg
    71.4 KB · Views: 5
  • PROF. MUHIDIN NA MOHAMED MAKTABA.jpg
    PROF. MUHIDIN NA MOHAMED MAKTABA.jpg
    16.2 KB · Views: 4
  • PROF. MUHIDIN NA MWALIMU.jpg
    PROF. MUHIDIN NA MWALIMU.jpg
    22.5 KB · Views: 5
  • PROF. MUHIDIN NA MOHAMED SAID.jpeg
    PROF. MUHIDIN NA MOHAMED SAID.jpeg
    61.5 KB · Views: 5
System imeamua kuacha kabisa kuandika Ukweli wa Historia ya Nchi hii ,
Sijui kwa madhumuni gani, Lakini inavyoonesha watu wamekusudia kufuta kabisa ukweli na kuandika ubunifu wao wa uongo na kumkweza Nyerere.
Kama ambavyo hawataki kusema loote kuhusu Historia ya Zanzibar na mchangowa Tawla z Kisultani na Zile z kienyeji hapa Zanzibar.

Nadhani kuna Namna Nchi hii ya Ubaya Unaopikwa.
 
Sh. Mohammed Said, sijakufahamu hapo!

Ina maana huyu Prof. Muhiddin ndio ameandika kitabu hicho cha maisha ya Nyerere? Au unazungumzia kile cha akina Shivji?
 
Back
Top Bottom