Mazungumzo ya biashara huria kati ya Kenya na Marekani yakabiliwa na utata mkubwa

Mazungumzo ya biashara huria kati ya Kenya na Marekani yakabiliwa na utata mkubwa

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
81a7-ivwfwmp7557951.jpg



Mazungumzo kuhusu biashara huria kati ya Kenya na Marekani yaliyopangwa kufanyika tarehe Mosi mwezi huu yameahirishwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hadi baada ya kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA. Rais Kenyatta amesisitiza mara kadhaa kuwa mazungumzo hayo hayatakiwi kuharibu maslahi ya AfCFTA, lakini kutokana na sera ya “Marekani Kwanza” inayofuatwa na serikali ya sasa ya Marekani, ni vigumu kwa Kenya kutimiza malengo yake kama ilivyotarajia.

Vilevile inahofiwa kuwa makubaliano hayo yakisainiwa, yataharibu umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wa Afrika nzima, na kupelekea nchi za Afrika kuingia kwenye mtego wa kusimamiwa moja moja na Marekani.

Mapema mwezi Februari mwaka huu, rais Kenyatta alipokuwa ziarani nchini Marekani, pande hizo ziliamua kujadili kusaini makubaliano ya biashara huria, ili kupanga mpango kwa ajili ya biashara kati ya nchi hizo baada ya “Sheria ya Ukuaji na Fursa barani Afrika, AGOA” kumalizika mwezi Septemba mwaka 2025. Kwa upande wake, Kenya inataka kuvutia teknolojia na uwekezaji wa Marekani ili kusaidia kufanikisha Ruwaza ya 2030, na pia kujiongezea nguvu za kuwachagua wenzi wa kibiashara.

Lakini kwa upande wa Marekani, AGOA ni sera inayonufaisha upande wa Afrika tu, hivyo inataka kusaini makubaliano ya biashara huria ya pande mbili ili kuuza bidhaa zake kwa wingi zaidi nchini Kenya na kugeuza pengo la biashara lililopo sasa.

Marekani iliwahi kusema katika mazungumzo ya awali kuhusu makubaliano hayo kuwa katika miaka kumi ijayo thamani ya mazao ya kilimo yatakayoagizwa na Kenya kutoka Marekani yanatakiwa kufikia dola za kimarekani milioni 470. Lakini kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana mwaka jana, thamani hiyo kwa miaka 10 ni dola za kimarekani milioni 270 tu. Hii inamaanisha kuwa, Marekani inaitaka Kenya kuagiza mazao ya kilimo mara dufu kutoka kwa Marekani, jambo ambalo litailetea Kenya hasara kubwa haswa kwenye sekta ya kilimo nchini Kenya.

Akizungumzia hilo, mwanauchumi wa Kenya ambaye pia ni mkurugenzi wa Mtandao wa Uchumi wa Kikanda Bw. James Sikwati amesema, “Kenya ina changamoto kubwa, kwa sababu viwanda vyake haviwezi kulingana na vya Marekani, na wakulima wa Kenya hawawezi kushindana na wakulima wa Marekani wanaotumia mashine na kemikali.”

Imefahamika kuwa Marekani pia inataka kujishughulisha kwenye sekta nyeti kama nguo na teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA, na kuitaka Kenya ipunguze kutoa ruzuku kwa kampuni za taifa. Hii pia itazuia utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya uzawa.

Takwimu zimeonesha kuwa mwaka 2017, Marekani ilikuwa nchi ya tatu kwa kuuza bidhaa kwa wingi nchini Kenya, na nchi ya saba kwa Kenya kuagiza bidhaa kwa wingi. Lakini kwa upande wa Marekani, Kenya ilishika nafasi ya 96 tu miongoni mwa wenzi wa kibiashara wa Marekani.

Hii inamaanisha kuwa, Kenya inaitegemea zaidi Marekani kiuchumi, na Marekani ina karata nyingi zaidi katika mazungumzo hayo, kwa hivyo kwa Kenya, fursa ya kufanya mazungumzo kwa usawa ni ndogo. Bw. Sikwati amesema, “Tukiingalia kwenye mapato kuangalia nani atanufaika zaidi, tunaona Marekani ndio watanufaika zaidi, na wakenya hawatanufaika sana.”

Mbali na shinikizo la ndani ya nchi ya Kenya, makubaliano ya biashara huria kati ya Kenya na Marekani pia yanakabiliwa na changamoto katika bara la Afrika. Pengine Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na kamati inayoshughulikia mambo ya AfCFTA wanaona kuwa makubaliano hayo yataleta athari mbaya kwa Umoja wa Afrika.

Takwimu zinaonesha kuwa biashara kati ya nchi za Afrika imechangia asilimia 18 tu ya biashara za jumla za Afrika, na nchi za bara hilo zimetambua umuhimu wa kupanua masoko ya ndani na kuongeza uzalishaji wa ndani ili kutimiza maendeleo ya Afrika. Lakini kusaini makubaliano na nchi fulani ya Afrika inaweza kusababisha ushindani mbaya kati ya nchi za Afrika, na huenda baadhi ya nchi zitapunguza vigezo ili kujipatia fursa ya kusaini makubaliano na Marekani, jambo ambalo litaleta hasara kwa maslahi ya jumla ya nchi za Afrika.

Mtafiti wa kiuchumi na maswala ya kisera kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Profesa Haji Semboja anaona kuwa, vitendo vya Marekani vinakwenda kinyume na moyo wa EAC na AfCFTA, na nchi za Afrika zinatakiwa kusonga mbele kwa pamoja.

“Kenya imepiga hatua kimaendeleo, (Wamarekani) wanaweza kuanza kushirikiana na Kenya, lakini sio kama wanataka kuisaidia na kuiendeleza Kenya, bali ni kuizuia Kenya isiendelee zaidi na bara la Afrika lisiendelee. Kwa kawaida kabisa Marekani haina marafiki, lakini wanakuwa na hoja zao au maslahi yao ambayo wakati mwingine sio rahisi kwa sisi kutambua kwa haraka na kujua kwa uhakika.” Amesema nchi za Afrika zinatakiwa kuimarisha ushirikiano wao wa kiuchumi na kisiasa na pia kuongeza ushirikiano na nchi nyingine nje ya Afrika.

Pia kuna uchambuzi kuwa katika kusaini makubaliano ya biashara huria na Kenya, dhamira ya kisiasa ya Marekani ni kubwa zaidi ya ile ya kiuchumi. Kwa mujibu wa utamaduni wake, baada ya kuingia kwenye soko la Kenya, Marekani inatarajiwa kuondoa ushirikiano wa nchi nyingine na Kenya.

Hivyo jinsi ya kuweka uwiano katika uhusiano wake na Marekani na nchi nyingine, na kuepuka kuwa karata ya Marekani ya kujitafutia maslahi yake, pia itakuwa changamoto kubwa kwa Kenya. Juu ya hilo, Bw. Sikwati anasema, “Marekani inatafuta fursa ya kurudi kwenye kiti cha uongozi katika sehemu ya Afrika Mashariki. Ni lazima Kenya itafute njia ya itakayohakikisha kuwa inanufaika. Kama hatutatafuta uwiano mzuri basi hapo tunaweza kujikuta kwenye mazingira kama ya ‘wanapopambana mafahari wawili, ziumiazo ni nyasi’ sisi ndio tutakuwa nyasi.”
 
"Marekani inatafuta fursa ya kurudi kwenye kiti cha uongozi katika sehemu ya Afrika Mashariki. Ni lazima Kenya itafute njia ya itakayohakikisha kuwa inanufaika. Kama hatutatafuta uwiano mzuri basi hapo tunaweza kujikuta kwenye mazingira kama ya ‘wanapopambana mafahari wawili, ziumiazo ni nyasi’ sisi ndio tutakuwa nyasi.”

Ikumbukwe kuwa Marekani ilishashindwa kuwa na mkataba wa kiuchumi baina yake na East african Community ndio maana sasa imeamua kuingilia mlango wa Kenya ikijua fika kuwa itapata soko kubwa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki...Muungano huu haufai na sio rafiki kabisa unafaa kupingwa.
 
Natamani uhuru atie sign kwenye hio mikataba ya biashara.
 
Mungu asamehe upuusi wako wa kutokuelewa implications zifuatanazo na huo mkataba
 
Back
Top Bottom