Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAZUNGUMZO YA BURIANI OCTOBER 1968
Hapo chini Aisha ''Daisy'' Sykes anaeleza mazungumzo ya buriani, mazungumzo ya kuagana kati ya baba yake Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwa Mwalimu Msasani.
Ilikuwa mwezi October 1968 wakati huo Daisy mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam.
Msikilize:
''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.
Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Dar - es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Kleist Abdallah Sykes.
Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanye utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.
Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.
Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.
Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.
Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.
Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.
Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.
Allah amghufirie madhambi baba yangu na amuingize peponi.''
PICHA:
Aliyesimama ni Abdul Sykes na aliyekaa ni Julius Nyerere.
Picha hii imepigwa Ukumbi wa Arnautoglo katika hafla ya kuuaga Nyerere safari ya pili UNO 1956.
Aisha ''Daisy'' Sykes kama alivyo hivi sasa.
TANBIHI:
Ilikuwa Jumamosi Abdul Sykes na bint yake Daisy walipokwenda kuonana na Mwalimu Nyerere.
Jumamosi iliyofuatia Abdul Sykes akafariki dunia.
Mara ya kwanza Abdul Sykes kuonana na Nyerere ilikuwa mwaka wa 1952 Nyerere alikwenda nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu akiongozana na Joseph Kasella Bantu.
Siku ya mwisho watu hawa kuonana ilikuwa mwaka wa 1968 Abdul Sykes amekwenda kuonana na Julius Nyerere Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msasani akiongozana na bint yake Aisha "Daisy" Sykes ambae Mwalimu akimjua toka utoto wake.
Historia kubwa sana ya TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere imehifadhiwa katika vifua vya watu ambao huwezi hata kuwadhania.