Mazuri yanayoweza kuja kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Mazuri yanayoweza kuja kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Tukirejelea msemo wa "Hata katika hali mbaya kunaweza kupatikana mazuri ukitazama kwa bidii" haya yanaweza kuwa mazuri yatakayotokana na vita vya Russia nchi Ukraine.

1. Mapinduzi makubwa ya kilimo Afrika
Vita hii imeonyesha jinsi gani sehemu kubwa ya dunia maskini hasa Afrika ni tegemezi kwa Russia na Ukraine kwenye ngano na kwa jinsi gani msukosuko wowote mkubwa kwenye mataifa hayo hauwezi kuacha kuifikia Africa. Ngano ni zao linaloweza kustawi maeneo mengi Africa ikiwepo Tanzania, ni aibu kwa bara kubwa kama hili kuagiza ngano kutoka nje.Kuna uwezekano mkubwa wa wafanyabiashara wa Ulaya, Marekani na Asia wakaichukua hii kama fursa na kuja kufanya uwekezaji mkubwa wa kilimo Africa.

2. Mapinduzi makubwa katika sekta ya Nishati mdalala
Uvamizi wa Russia umeonyesha udhaifu mkubwa wa Ulaya kutegema gesi na mafuta ya Urusi. Katika muda mrefu wa kati ya miaka 5 hadi 10 Ulaya wataichukua hii kama changamoto na funzo muhimu kufanya vyanzo vya nishati mbadala kuwa chanzo kikuu cha mahitaji yao ya nishati. Wanayo teknolojia na mitaji ya kufanya hivyo, kilichokuwa kikosekana kwa muda mrefu ni utashi wa kisiasa.

3. Mabadiliko makubwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa(UN)
Katika uvamizi huu UN imedhihirisha udhaifu mkubwa sana. Hakuna jambo lolote la maana UN imeweza kufanya mpaka sasa kuisadia Ukraine, sababu kubwa ni Urusi na China kuwa kati wanachama watano wa kudumu wenye kura turufu kwenye baraza la usalama la UN.
 
Back
Top Bottom