Mbabe wa barabarani, wengine ni hamna kitu

Labda muwe mnapita mapori ya kamsamba huko.

Ila kwa hizi barabara tunazopita kila siku? Hiyo BMW inakuacha mbali sana.

Hizo gari zipo barabarani na tunazitumia.

Tena kuna golf kibao huko barabarani zinawachapa tena hazina hata nguvu ya maana ila zinawakalisha.

Kuna wakati nilikuwa nasafiri na Vanguard, naanza kile kijangwa cha same ikanipita benz c180. Ile gari ilinisumbua mpaka tunafika mwanga, pona yangu ilikuwa kwenye matuta, ikipunguza speed ndo naikaribia. Hata nikiwa 170kph huifikii hata kidogo.

Gari za mjerumani msizidharau kiasi hiko. Nina mifano mingi sana ya mabalaa yake hayo magari. Na huwa nasafiri nazo tena za kawaida sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ujasiri wa kukimbiza mjini mnautoa wapi?

Hata unipite na 200 sihangaiki na wewe. Ila kama tunasafiri kwenda mf arusha, nikishapita ile round about ya bagamoyo. Nakupelekea moto labda uwe na gari imenizidi uwezo. Nakuwa mpole, nakufuata nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye ligi za hapa bongo cha muhimu ni dereva wa chombo cha moto, hata uwe na BMW sijui twin turbo cc 9000. ukikutana na dereva wa bodaboda halafu kapiga k vant au kiwingu cha kutosha ukianza naye ligi yeye hana cha kupoteza ni mwendo wa mbwa atakupita kama umesimamaπŸ’
 
Ndio mazingira yenyewe mkeka wa mandela road unakuwaga msafi sana kuanzia ngoma 4-5 hapo trafic lights zinaenda sleep mode!
 
Hahahahahahah mjerumani ana balaa ila kipigo anakula vizuri tu kama una mashine ya maana! 2GR ijaribu siku ukipata wasaa tena ikiwa na 260kph ndio mwake
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Eti macho madogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…