Mbabe wa Ulaya kujulikana leo kwenye fainali ya UEFA

Mbabe wa Ulaya kujulikana leo kwenye fainali ya UEFA

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za weekend wadau wa soka na wapenzi wa kandanda barani Africa na Tanzania kwa ujumla nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania:–

Leo majira ya saa 4–usiku watakutana muamba ya ulaya kwenye UEFA champions league ambapo Real Madrid atatoana jasho na Borussia Dortmund katika uwanja wa Wembley. Real Madrid wanawania kushinda taji lao la 15 la UEFA champions league huku Borussia Dortmund wakilitafuta taji lao la pili la UEFA champions league baada ya miaka 27 tangia mara ya mwisho walipochukua taji hilo mwaka 1997.

Kocha wa Borussia Dortmund hii ndio fainali yake ya kwanza kama kocha mkuu baada ya kuwa assistant coach na technical director kwenye vilabu kama west ham United na besiktas kwa mda mrefu. Kocha wa real Madrid (Ancelotti) ameweka rekodi ya kuchukua UEFA champions league akiwa kama mchezaji na akiwa kama kocha mkuu mara nne mara mbili akiwa na Ac Milan na na mara mbili akiwa na Real Madrid.

Real Madrid ndio kinara wa kutwaa kombe hilo mara 14 akifuatiwa na Ac Milan mara 7 huku liverpool na Bayern's Munich wakitwaa mara 6 kila mmoja na Barcelona akitwaa mara 5. Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa real Madrid Christian Ronaldo ndio kinara wa kupachika mabao kwenye michuano hiyo akifunga bao 141, akifuatiwa na messi bao 129, Lewandowski 94
Benzema 90, Raul Gonzalez 71 na van nistelrooy 60.

Real Madrid wamecheza UEFA champions league final mara 17 wamepoteza mara 3 tu wakati Borussia Dortmund wamecheza mara mbili na wamepoteza moja dhidi ya Bayern's Munich 2013 Leo hii Real Madrid wanaenda kucheza final yao ya 18 huku Borussia Dortmund wakiwa wanaenda kucheza final yao ya 3 katika historia yao. Leo katika dimba la Wembley Ancelotti mwenye miaka (64) anaenda kukutana na Ediz Terzic miaka ( 41) wataoneshana mbinu na kubadilishana uzoefe majira ya saa 4–usiku.

Leo usiku ni mara ya mwisho kuwaona toni kroos na Marcus reus wakiwa wamevaa jezi za team zao kwani wote wametangaza kuwa hii UEFA champions league final ndio kwa mara ya mwisho wataonekana katika club zao hizo walizozitumikia kwa muda mrefu hatimaye wameamua kuwaaga rasmi mashabiki wa soka na wa team zao usiku wa leo.

Nani anakaa leo pale Wembley karibuni kwa maoni na ubashiri.

Alamsik
 
Dortmund tupeni surprise please
Mkuu Dortmund kitakachowaangusha ni uzoefe maana kuna mechi moja ya champions league carlo Ancelotti alizidiwa mbinu na mpinzani akawatoa Marcelo na Tony kroos wamshauri nini cha kufanya maana ilikuwa washakaa tayari akainuliwa bwana mdogo rodrigo na kweli akaenda kuokoa jahazi yaani Dortmund kuanzia kocha mpaka wachezaji uzoefe wa UEFA champions league ni mdogo ila ngoja tuone maana kwenye mpira lolote linaweza kutokea.
 
Akili inagoma inaniambia kuwa wakulima wa miwa leo wanachukuwa ubingwa...akili inakataa kabisa kuona Madrid wakiwa mabingwa
 
Tunaupenda mpira kwasababu ya moments tusizozitarajia
 
Akili inagoma inaniambia kuwa wakulima wa miwa leo wanachukuwa ubingwa...akili inakataa kabisa kuona Madrid wakiwa mabingwa
Kiufupi team zote mbili hazina wamaliziaji angekuwepo benzema na haland game ingekuwa imeisha mda sana.
 
Back
Top Bottom