ada ya mja hunena muungwana vitendo
semeni wazi kuwa hamumpendi jk
mbona wakati wa bm hamkuthubutu kusema????
Mzee rukhsa alilizika azimio la arusha mbona hamsemi
chakufahamu hapa ni hata kama sisi wana jf wote hatumtaki pamoja na wasomao magazeti lakini mjue kuna mamilioni ambao wako nyuma yao jee hao wote ni wajinga??????
Hivi ni raisi gani amewahi kuthubutu kuwapeleka mahakamani idadi kubwa ya viongozi tangu tupate uhuru???? Au mlitaka awahukumu kwa kuwaweka kizuizini kama zile enzi???????
Kwanza kabisa, kwamba mwizi mmoja kaiba na hajakamatwa haihalalisha kwa mwizi wa pili kuiba, na akikamatwa hawezi kusema "mbona fulani hamjamkamata".Huu si utetezi, ingekuwa hivyo justice system isingeweza kufanya kazi maana ili kumkamata mwizi mmoja ingebidi kukamata wezi wote, kitu ambacho hakiwezekani. Two wrongs do not make a right.
Pili, wewe unaongelea Mkapa na Mwinyi gani? Mbona tumewasema sana sio hapa tu, kuanzia Nyenzi, Tanzanet BCS, YA mpaka Jamboforums na sasa Jamii Forums, wewe unaongelea hawasemwi wapi?
Of course kwa sasa Kikwete atasemwa zaidi kwa sababu yeye ndiye rais na mtu mwenye responsibility ya mwisho Tanzania.
Watu wanamsema huyo golden boy wa propriety bongo, Julius KAmbarage, itakuwa huyu muhuni asiyejua kujifuta kamasi za kisiasa Jakaya Kikwete?
Forget about marais, watu wanamsema huyo mungu mwenyewe, itakuwa hawa binadamu?
Kuhusu kupeleka watu mahakamani, tatizo si kuwapeleka mahakamani, tatizo ni nini kinafanyika baada ya hizi sarakasi za mahakamani? Na kama kweli anataka kupeleka watu mahakamani anasubiri nini kuwapeleka kina Chenge na Mkapa?