Mbadala wa JK


Nyerere pia alimpeleka waziri wake mahakamani. If I am not wrong, aliiambia mahakama kazi yake ni kusikiliza shauri lake na kutambua kama ana hatia, halafu kazi ya kumhukumu waiachie serikali. Mahakama ilipothibitisha, Nyerere akaamuru kwa kosa la kudai na kupokea Rushwa jamaa achapwe fimbo 12 hadharani halafu awekwe ndani.
Binafsi nasema JK amejitahidi, na ana kifua kwelikweli. Hawa wanaopiga makelele ni malimbukeni tu maamuzi ya kumchukua partner wako na kumpeleka mahakamani siyo mzaha ati!? Can you imagine, akina Mgonja, Mramba amefanya nao kazi, kakaa nao kwenye baraza moja la mawaziri halafu siku nyingine anawapeleka mahakamani. Is not an easy thing. Tuwe realistic! Tuongee kuhusu kushindwa kumanage uchumi lakini si kupambana na ufisadi. Huyu jamaa ameonyesha uthubutu. Tumuunge mkono, badala ya kumsakama kila kukicha. Toka Nyerere, Jk is the second kuonyesha utayari wa kupeleka wala Rushwa mahakamani. Tumpe support wakuu!
 
Tusiponde mapendekezo ya wanachama wa JF pasipokuwa na hoja pia sababu hawafai waliopendekezwa. Mimi kwa ufahamu wa timu nzima ya wanaCCM naona afadhali Magufuli. Sababu hasa ni historia ya utendaji wake, haionyeshi mapungufu mengi. Amekuwa mtu makini sana kusimamia mabadiliko (reforms) ndani ya sekta anazoongoza. Bahati mbaya mabadiliko hayo kila yanapowalenga wakubwa mheshimiwa Magufuli huishia kuhamishwa ili wakubwa wasipoteze. Mfano, alipokuwa ardhi, alisimamia matatizo makubwa ya wilaya ya Kinondoni na fukwe mbalimbali ambazo kisheria hazikutakiwa kujengwa, ila wakubwa walikuwa wamejimilikisha na alivyolifanyia kazi hilo haraka kabisa alihamishwa.

Ameenda huko mifugo, bado amekuwa imara tuendesha mabadiliko yenye nia ya kuboresha sekta husika, lakini tatizo wakubwa wamejimilikisha lanchi za Taifa. Si muda mrefu anaweza kuhamishwa. Hivyo, kwa kuzingatia uimara wake katika kusimamia mabadiliko mbalimbali yenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania kunampa nafasi kwangu kumupendekeza kama itabidi kumrithi mkuu wa nchi wa sasa.
 
Hii sasa ni chuki isiyo kichwa wala miguu, kwani baba yake alikuwa na ubaya gani?Isitoshe yeye ni Hussein na baba yake ni Hassan.
 
tatizo la Tanzania anayemuweka raisi ni system (UWT) na wala sio raia, kwa asilimia mkubwa Bwana EL kaikama system na ndio anayeelekea kuwa raisi wa nchi hii, ile sendoff yake walijaa watu ambao hata kwenye zile sherehe Za uhuru pale Taifa hawakuweko watu mashuhuri kiama wale,

tukitoa mambo hayo ya system, Bwana john Pombe Magufuli kwa sasa ndio atleast anaonekana anweza kututoa kwenye huu ujinga kutokana na misimamo yake yenye maslahi kwa taifa, ingawa kama binadamu anamapungufu yake, lakizi sio zaidi au sawa na ya muungwana.

kama mungwana kaweza, kweli magufuli atashindwa nini wakati kichwa kimetulia kuliko cha muungwana
 

The helm of mediocrity, tunaanza kuangalia situations na kuchagua jinsi ya kuapply sheria.

Unafahamu maana ya maneno rule of law?

Uliona post niliyoweka kuhusu Fidel Castro alivyosaini hati ya kuuawa rafiki yake kipenzi (Jenerali wa Cuba ambaye alikutwa na hatia ya kushiriki biashara ya madawa ya kulevya) waliyepigana vita vya ukombozi Cuba na kina Che Guevara in the 50's kumuondoa Batista?

Kwani Castro alikuwa hajui kwamba huyu ni rafiki? Lakini mbona aliacha sheria ifuate mkondo?

JK anapiga sarakasi tu, ana mark time anasubiri mda wake uishe wakati kesi hazieleweki, aende kujipumzikia kwao na protection ya ex presidaa.

Hana nia hata chembe ya kufanya kweli, angekuwa na nia tungeona. Tanzania is too top down for a daring president to not be able to deal with these fisadis.
 

mbona hampeleki ROSTAM huko unakoita mahakamani.maana akifanya hilo ndo tutamuona yuko realistic...sio kesi za akina mramba ambazo its obvous watashinda maana serikali imekurupuka
 

Asiyeniogopa mimi atakuwa hafai kuwa kiongozi!!!

Nadhani kuwa mtu wa maana hapa ni yule ambaye hatatoka chama chochote cha siasa, kwa vile mtu wa namna hiyo hatakuwa na watu wa kulinda, na endapo atakuwa nao basi watakuwa ni wachache sana ukilinganisha na wanaolindwa na chama.

Binafsi ningempendekeza mtu mzee sana ambaye hajawahi kuwa mwasiasa kusudi atusafishie nchi hii katika kipindi cha miaka mitano tu kabla hatujarudia vijana; huyo ni Profesa Geofrey Mmari
 
waziri gani Nyerere alipeleka mahakamani akachapwa viboko mtaje?
 
Tunataka Mchapa Kazi wa namna hii ili kama kuna wanaoenda kwa kubebwa bebwa wakae pembeni, Magufuli ndiyo chaguo hasaaaaa.
 
Mkuu KISIKI.
kama hatoweza unampendekeza nani basi atakayeweza??
 
wote hao mnaowataja hamna kitu.

mie nampendekeza edward ngoyai lowasa. kijana katulia yule, wanaomuita mzee wanampakazia tu, ni mjasiri amali mzuri, ana bonge la hekima, hata baada ya wenye wivu kumchukulia uwaziri mkuu wake katulia anapanga mahesabu, tena msipoangalia anaingia 2010.

bi sophia si kishawaambia dume la shoka a.k.a la mbegu lile, kwa nini hamsikii????
 
mkuu unachemka
unaposema msipoangalia ataingia madarakani ina maana hata wewe unaona hafai thus unampigia upatu huku nafsi haitaki.

Mie nasema SITTA Samweli anafaa kuongoza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…